Serikali yasaini mkataba ujenzi Daraja la Jangwani, Sh Bilioni 97.1 kutumika

Hivi wame shindwa kupata mkandarasi wa ndani anae jua hilo eneo vizuri zaidi hizo shilling bn 97 zibaki hapa hapa nchini,........college of civi Engineering Udsm haina product wa kujenga hilo daraja la robo kilomiter kweli?
Wakandarasi wa ndani hawa wanaoshindwa hata kutengeneza vidaraja vya mitaani!hapana aisee
 
Mji mkuu umehamishiwa Dodoma, inatosha. Kuhamishia Jiji Bagamoyo unamaansiha wananchi wa Dar tupelekwe Bagamoyo au unamaanisha nini?
Nilipoweka neno kuhamisha kwenye inverted quotes nilikuwa na sababu. Duniani kuna miji mingi tu ''imehamishwa'' na ukienda unakuta kuna mji mpya na mji wa zamani.
 
Panajengwa daraja sawa!, hizo barabara zilizopo zinabaki kama zilivyo na daraja linakuwa juu?..
 
Nchi ina matatizo mengi hii unadhani chadema ndio wangemaliza shida zote?
Ahaaa. Akili zako ni za kitanzania 100%. Ukisema CCM inafanya vibaya basi automatically wewe ni CHADEMA. Ujinga gani huu wa kukariri. Kinachotakiwa Tanzania ni mfumo mzuri na viongozi wenye upeo na waadilifu na siyo CHADEMA. Nchi zote zilizoendelea za dunia hii zainaongozwa na CHADEMA?
 
Nilipoweka neno kuhamisha kwenye inverted quotes nilikuwa na sababu. Duniani kuna miji mingi tu ''imehamishwa'' na ukienda unakuta kuna mji mpya na mji wa zamani.
Sawa, Dar kuhamishiwa Bagamoyo inamaanisha nini? Serikali imeshahamia Dodoma, sasa Bagamoyo kinahamia nini? Tubebe maghorofa toka Dar tuyapeleke huko au?
 
kuna kiumbe kasema 4R ndio zimesababisha ujenzi huo uje! Kwa vipi?
 
Hili daraja ndilo lilitakiwa kuanza kabla ya Tanzanite. Sielewi kwa nini walianza na la Tanzanite.
 
Hii nchi bhana kuna mda unajiuliza tu wakati wanaweka stend ya mwendokasi pale ina maana hawakuwaza mafuriko ya lile eneo 😂...

Nchi kama China ukifanya Uzembe kama huu ni kunyongwa tu hakuna kingine.
 
Hivi wame shindwa kupata mkandarasi wa ndani anae jua hilo eneo vizuri zaidi hizo shilling bn 97 zibaki hapa hapa nchini,........college of civi Engineering Udsm haina product wa kujenga hilo daraja la robo kilomiter kweli?
Nafikiri hizi kazi huwa ni maelekezo toka juu, hata ukiwa na bei ya chini bado tender yako itakataliwa.
 
Maigizo haya, Kwani deni la Kajima tuliisha maliza? Uchaguzi ujao na mapicha picha
 
Wakandarasi wa ndani hawa wanaoshindwa hata kutengeneza vidaraja vya mitaani!hapana aisee
Nakumbuka kuna mwaka mbongo mmoja alipewa kutengeneza hizi bara bara za mitaani.

Akawa anaishi gesti moja maeneo ya hapo hapo.

Alipomaliza kazi , baada ya miaka miwili tu ile barabara ni mashimo tu na ilikuja kurudiwa tena.

Wakandarasi wa ndani wanaweza kazi ila kuna wakati wanaharibu wenyewe.
 
Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na barabara za maungio zenye urefu wa mita 700 katika barabara ya Fire - Ubungo kwa gharama ya Shilingi Bilioni 97.1 ambapo kazi ya ujenzi itatekelezwa kwa miezi 24.

Mkataba huo umesainiwa leo Oktoba 22, 2024 Mkoani Dar es Salaam kati ya Wakala ya Barabara (TANROADS) na Mkandarasi wa Kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na viongozi wengine.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaondoa kero kwa wananchi na adha ya usafiri kutokana na eneo hilo kujaa maji mara kwa mara na kusababisha barabara kufungwa na kutopitika mvua zinaponyesha.

Bashungwa amemuelekeza Mkandarasi huyo kukamilisha maandalizi na kupeleka vifaa na mitambo ndani ya miezi mitatu katika eneo la Jangwani ili kazi iweze kuanza na kuhakikisha anajenga haraka kwa mujibu wa usanifu na mkataba kama ilivyopangwa.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaenda sambamba na ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi ambao utatekelezwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikiwa ni katika programu ya uendelezaji wa Bonde la Msimbazi.

Bashungwa amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 125 kwa ajili ya kurejesha miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam iliyoathiriwa na mvua za El-Nino ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigogo, daraja la Mpiji chini, daraja la Mtongani, daraja la Mkwajuni, daraja la Mzinga, daraja la Nguva na box kalavati la Mikadi, daraja la JKT – Ununio, daraja la Kisarawe, Amani, Gomvu, Geti jeusi, mifereji ya maji Kigamboni – Kibada na maeneo mengine.

Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi ni kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kusimamiwa na kampuni ya Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusini ikishirikiana na Afrisa Consulting Ltd ya Tanzania na Dong Myeong Engineering Consultants & Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini.

Naye, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hassan Zungu ameeleza kuwa utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Jangwani ni matokeo ya 4R za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka historia ya kuanza kutekeleza ujenzi wa daraja la Jangwani.

Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani Dar es Salaam kwa kuboresha barabara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya Usafiri.
Pia soma ~ Barabara ya Kilwa kipande cha Mbagala Mzinga kuja Kongowe mpaka Kisemvule iboreshwe kabla ya kuleta maafa
Maendeleo HAYANA CHAMA!
HONGERA ZAO!
 
Muda wa maandalizi umo katika Mkataba na hapakuwa na sababu ya waziri kutoa "maelekezo". Kama muda uliokuwemo kwenye mkataba ni zaidi ya hiyo miezi mitatu, mkandarasi atakuwa na haki ya kudai malipo ya ziada mara atakapo pokea maelekezo kutoka kwa mshauri wa mradi. Sio lazima waziri atoe maelekezo kila anapo simama kwenye jukwaa. Hiyo kazi awaachie wale walioainishwa katika mkataba kuwa ndio wenye mamlaka ya kutoa maelekezo.

Amandla...
 
Nakumbuka kuna mwaka mbongo mmoja alipewa kutengeneza hizi bara bara za mitaani.

Akawa anaishi gesti moja maeneo ya hapo hapo.

Alipomaliza kazi , baada ya miaka miwili tu ile barabara ni mashimo tu na ilikuja kurudiwa tena.

Wakandarasi wa ndani wanaweza kazi ila kuna wakati wanaharibu wenyewe.
Mkandarasi anaongozwa na mkataba katika utekelezaji wa mradi. Wa kulaumiwa ni wale waliotayarisha makabrasha ya mradi pamoja na wale waliokuwa wanamsimamia.

Amandla...
 
Hivi wame shindwa kupata mkandarasi wa ndani anae jua hilo eneo vizuri zaidi hizo shilling bn 97 zibaki hapa hapa nchini,........college of civi Engineering Udsm haina product wa kujenga hilo daraja la robo kilomiter kweli?
Serikali imejaza wajinga and no strategy people, barabara na madaraja ilikuwa sehemu nzuri ya kuajiri foreigners na sehemu ya kufanyia reverse engineering, tunapoteza billions unnecessary
 
Back
Top Bottom