Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

Viti 60,000 kila kiti kimoja ni 70,000.

Mashine za ukaguzi eneo la kuingilia uwanjani.

Mashine za ukaguzi eneo la kuingilia majukwaani.

Kuondoa Pitch yote.

Marekebisho kwenye mifumo mizima ya umeme, taa mpya, CCTV za kisasa.

Mifumo ya Maji, Vizuizi katika ya Jukwaa moja na jingine.

Marekebisho kwenye Run ways.

Marekebisho kwenye sehemu za kukaa wachezaji na benchi la ufundi.

Urekeibishaji wa Paa nk.

Hiyo Bil 5 unanunua VITI TU bila hata kufungwa na ukumbuke hapo hakuna VAT.
 
Mkuu hii mada imekuzidi upeo, ungetulia na kubaki kuwa msomaji.
Ile tv inafika mpaka Dola laki Saba unusu,bado mifumo,vitu elfu 60,wafumue pitch, generator mbili nk...unadai mada imenizidi upeo,hebu tupe gharama zako
 
Serikali imetangaza kuanza Ukarabati wa Uwanja wa Taifa "Uwanja wa Mkapa" kwa gharama ya Tshs. Bilioni 30. Uwanja huo haujakarabatiwa kwa miaka 16 tangu uzinduliwe mwaka 2007.

Chanzo kimeeleza kuwa, Marekebisho makubwa yamepangwa kufanyika ikiwemo kubadilisha viti vyote, kubadilisha mifumo ya Taa, Stadium TV Screen, Eneo la kukimbilia na kuweka Mabenchi ya Kisasa ya Wachezaji.

Lengo la marekebisho hayo ni kuboresha miundombinu ya Uwanja kuendana na wakati wa sasa ili kutoa burudani stahiki kwa Wadau wa Soka Nchini na walioko Nje ya Nje.

Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na zaidi ya Tshs Bilioni 137.
 
Kujenga -Bilioni 60

Ukarabati - Bilioni 30..,

Hata kama pesa imeshuka thamani, sio kihivyo, ibeni kwa akili mbwa nyie!! Ubadilishe viti vyote kwani vyote vimevunjika?
 
Huu uwanja ubinafsishwe, kwanini serikali itumie kodi zetu kuukarabati uwanja ambao ni kitega uchumi kizuri cha kuingiza mapato?

Wizi mtupu.
 
 
Justification ya matengenezo tunaiona ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ maana kwa mvua hizi za dar zinawahumbua tuu mbona
 
Huu mkataba umesainiwa July 2023, hivi sasa ni November 2024, uwanja bado unakarabatiwa! muda huo uliotumika ungeweza kujenga uwanja mpya na kuumaliza๐Ÿšฎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ