Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

TANZANIA TAJIRI SANA UJENZI BIL.60 UKARABATI BIL.30
20230728_103834.jpg
20230728_103849.jpg
 
Watanzania tukatae huu wizi wa mchana Mweupe,pesa hiyo inatosha sana kujenga Uwanja Mpya wa Ukubwa wa watu kuanzia 30,000
 
Uwanja wa MKAPA ulijengwa kwa BIL.60
LEO unafanyiwa UKATABATI kwa BIL.30 haya ni MAFANIKIO MAKUBWA inaonekana Nusu ya UWANJA unahitaji kufanyiwa UKARABATI
20230728_103834.jpg
20230728_103849.jpg
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, tarehe 27 Julai, 2023.View attachment 2701236
Hii nchi , twende tu sasa hafla ya nini, tunajiabisha sana kama taifa yani kukarabati kile kilichokuepo , tena unalipa pesa unafanya hafla?

Napendekeza kuanzia sasa angakau kubadili kwa dharula sheria zetu kwamba ukiondoa Rais , makam wa rais , waziri mkuu, watendaji wakuu kwenye wizara nyeti ,washauri wa rais kwenye mambo ya kimaendeleo na uchumi ,na mipango tuajiri watu toka nje katika nchi ambazo zimepiga hatua kwa mikataba kana ambavyo Tim za mpira wanafanya,

Sie Watanzania tunaaminiwa ila to wapumbavu ,wajinga, wabinfsi ,upumbavu gani huu, yani watu wapumbavu wanafanya wote tuwe wapumbavu na kua na haibu mbele za watu why
 
Tulizeni vikojoleo nchi ina wenyew... Nyie si mpo bize na DP world
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema Serikali ya [emoji1241] imetoa Tsh 30 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉 kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja wa Mkapa.

Amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo.

Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na Tsh 137+ 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉.

===
View attachment 2700662
View attachment 2700663
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja huo.

Alisema lengo la kukarabati huo ni kufikia viwango vya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili uendelee kuwa bora zaidi.

"Wito wangu kwa kampuni ya BCEG, hakikisheni kazi hii mnayoifanya iwe ya viwango vinavyowekwa iendane na ubora na viwango vya CAF na FIFA na ikamilike kwa wakati” amesema Dkt. Chana.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu amesema uwanja huo utafanyiwa marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji, chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo, ubao wa kuonesha matokeo, kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba, mfumo wa umeme, mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha, chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa, mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.

Aidha, Katibu Mkuu Yakubu ametoa wito kwa watumiaji wa uwanja huo wakiwemo mashabiki, kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uwanja huo ili iendelee kutumika kadiri ilivyopangwa na kuendelea kuwa eneo la watanzania kupata burudani wakati wa kuangalia mechi mbalimbali na nchi jirani wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.

Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo.
Nilishtuka usingizini Nilifikiri naota kumbe radio ilikuwa anasema hayo!
 
Nchi hii kuna watu wanaifaidi sana. Anyway, hivyo viti wanavyoving'oa, wavipake rangi vikawekwe katika viwanja viwili vya mikoani vya kuingiza watu 30,000 kila kimoja tupate viwanja vingine 2 wenye standard nzuri ya pitch na majukwaa.

Natumaini makubaliano na hao wachina yatajumuisha maboresho ya viwanja hivyo vingine viwili.
Hivyo viti vilivyotolewa kuna mwanasiasa atapewa kama sadaka mkuu
 
Back
Top Bottom