Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

Uwanja una giza sana, hili nilishalisema sana. Ni kwamba watanzania tumezoea kukaa kwenye giza (barabara zetu hazina taa za kutosha, bar nyingi watu wanakaa gizani na majumbani pia) kwa hiyo wengi hawakuona tatizo ila quality ya video za mechi za usiku ndiyo ilikuwa inaathirika.

Hapa ni lazima gharama za tiketi ziongezeke na makato yanayoenda BMT, TFF na kwingine yapungue ili pesa nyingi ibaki kuendesha uwanja na nyingine kwa timu husika. Ikibidi iundwe taasisi maalumu ya kusimamia huo uwanja na mapato yabaki mikononi mwa taasisi hiyo ili kupunguza ukiritimba. Pia shughuli zisizo za mpira zipunguzwe katika uwanja au gharama za kuukodisha ziongezeke sana kufidia uchakavu unaotokana na matumizi. Ile sehemu ya kukimbia wanariadha imechakaa bila hata kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa na hili limechangiwa na hizo shughuli zisizo za michezo zinazofanyika pale.
 
Ukarabati ni Jambo zuri, Ila najiuliza tu 30 bil zote zitatumika kukarabati au ndo mambo ya 10%? Je! Viti na taa zitakazotolewa hapo zitaenda kufungwa kwenye viwanja vingine ambavyo hali yake ni duni?
 
Mbona nasikia ukarabati ulianza kitambo kwa makubaliano maalumu kati ya Simba SC kama washiriki wa African Super League na CAF ambapo CAF wangerabati ili uwanja ufikie vigezo vya African Super League?

Vv
 
Huu upuuzi wa majitu yasiyo na akili yanajifungia na kuja na Mapendekezo ya kijinga ndio inasababisha Serikali inadharauliwa.

Rais zuia huu mkataba hauna Tija ,ndio sababu watu wanasema hakuna Uongozi kama pesa za walipakodi zinachezewa kirahisi hivi.
Huyo anayetakiwa ku zuia anajali?
 
SELIKALI inashindwa kujenga kiwanja Dodoma kwa Dola Milioni 600

Hela wanazotuibia hakuna Cha maana wanacho fanyia.

LAANA TU.
SHETANI.
Hii ya dodoma tulionesha hadi sketch ya 3d na mwendazake sijui iliishia wapi?
 
Ukarabati ni maagizo ya CAF watanzania tunapenda sana filimbi
 
Ukarabati ni Jambo zuri, Ila najiuliza tu 30 bil zote zitatumika kukarabati au ndo mambo ya 10%? Je! Viti na taa zitakazotolewa hapo zitaenda kufungwa kwenye viwanja vingine ambavyo hali yake ni duni?
Vitavyotolewa hapo vitauzwa kwa mnada kama skrepaz
 
nampongeza sana mama kwa kundelea kutushika mkono katika sekta ya michezo tanzania
 
Mbona nasikia ukarabati ulianza kitambo kwa makubaliano maalumu kati ya Simba SC kama washiriki wa African Super League na CAF ambapo CAF wangerabati ili uwanja ufikie vigezo vya African Super League?

Vv
Ni kweli, Simba pia anahusika katika mchakato huu ila naona kama inaongelewa chini chini. Na huu uwanja ni kama wa Simba maana Rais Mkapa aliujenga baada ya kushtushwa na mafanikio ya Simba kimataifa.
 
Watanzania tunapenda kulalamika sana

Hiyo gharama ni reasonable kabisaa
 
Hivyo viti vina shida gani mpaka wavitoe? Ukarabati ulitakiwa kufanyika kwenye miundombinu ya maji, vyooni, kupaka rangi, na kuendelea kuiboresha pitch.

Halafu hiyo TV iliwahi kufanya kazi tangu ilipofungwa? Na kwa nini walioiweka wasiwajibishwe kwa utapeli?
TV za kisasa huko kwa wenzetu ktk viwanja huwa ni kama 1b za kitanzania, tena hapo inafungwa mpya. Sembuse kufanya repair hapo? Mbona kipindi cha nyuma ilkuwa inafanya kaz? Cost za pale ni repair ndogondogo tu.

Kuna watu hii mada imewazidi upeo, ni bora wangekaa kimya. Nakubali kuwa marekebisho yote hayo yamkini haizid 5b.
 
Back
Top Bottom