Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo amesema wamekutana na wafanyabiashara wa Kariakoo na kutoka sehemu nyingine Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo, Majid Mbwana baada ya mapema kutokea Mgomo wa Wafanyabiashara ambapo Biashara zilifungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024. Pamoja na Chalamila kuwasili Kariakoo katika jitihada za kutatua mgogoro huo jitihada zake ziligonga mwamba Baada ya Chalamila kuondoka Kariakoo, bado Wafanyabishara waliendeleza mgomo wa kufunga maduka.

Waziri Kitila amesema changamoto zilizofanya wafanyabiashara kutaka kufunga biashara zao zipo katika maeneo matano ambayo ni:-
  1. Changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususan bandarini inayosababisha makadirio ya kodi yasiyo sahihi.
  2. Changamoto ya ukokotoaji ya kiwango cha kodi ambacho wanalipa.
  3. Suala la uwepo wa machinga katika maduka ambayo wanauza
  4. Suala la kamatakamata ambalo limekuwa likiendeshwa na mamlaka ya mapato(TRA)
  5. Changamoto kwenye sheria ya muswada wa fedha(Finance Bill)
Baada ya majadiliano ya kina Serikali imekubaliana mambo yafuatayo
  1. Kuanzia Julai 1, 2024 mamlaka ya mapato Tanzania itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri zaidi katika kuhakikisha wafanyabiashara wanapata makadirio ambayo ni sahihi.
  2. Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) inasitisha operesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka mfumo mzuri zaidi wa kukusanya mapato.
  3. Suala la ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria, Serikali imelichukua na inaendelea kuliangalia ili kuboresha zaidi mfumo wa ukokotoaji wa kodi hususani bandarini.
  4. Kuendelea kuwapanga wamachinga kama ambavyo Rais aliagiza ili wakae katika maendeo sahihi ambayo hayaingilii biashara za watu wenye maduka ili kila mtu aweze kufaidika, wamachinga na wenye maduka katika eneo la Kariakoo.
  5. Serikali imewataarifu wafanyabiashara kuwa muswada wa sheria ya fedha(Finance Bill) ya mwaka 2024 bado haujapitishwa na sasa uko katika majadiliano bungeni na kamati ya bunge la bajeti imeita wananchi wote waweze kutoa maoni ikiwemo wafanyabiashara hivyo imewaalika yale maoni ambayo wanayo wayapeleke kwenye kamati ya Bunge na wabunge watazingatia maoni yao kabla sheria haijapitishwa.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3cz
Screenshot_20240624-153814.jpg
 
Chalamila anapenda kulichafua Jeshi letu kwa kulihusisha na operesheni zake za kindezi. Wakati wa maandamano ya Chadema alitaka kulitumia Jeshi kuwatishia, leo tena anataka kulitumianJeshi kuwatishia wafanyabiashara wa Kariakoo, akome kabisa kulidhalilisha Jeshi letu kana kwamba halina kazi maalumu ya kufanya.
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Pumbavu. Mpaka wabanwe mbavu ndiyo wanatikisika?
 
Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3czView attachment 3024811

Nani alikuambia udikteta uliwahi kufanya matokeo chanya?

Hao wote uliowataja ni vichaa ndio maana wao kila maamuzi walitumia/wanatumia nguvu pasina akili.

Mgomo bila vurugu ni haki kikatiba muwe mnaelewa vitu.

Hapo serikali imepoteza mapato ambayo ndio kodi mnazomsifia huyo malkia wa anga kuwa katoa mabilioni kwenye mradi fulani.
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Ni jambo jema.
 
Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3czView attachment 3024811

Lunatic wewe. Majeshi yetu yana kazi nyingi za muhimu kushinda huo upuuzi mliokua mnataka kuwambia wafanye ...hio list kuukaribia hata uwaziri mkuu sahau, mmoja ashakufa hapo. Ubabe hausaidii. Kalisha mapumbu hapo nyuma ya keyboard ukisubiria hizo rangi ambazo wataona wafanyabiashara
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Serikali imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Umewahi kujiuliza kwanini Samia anakimbia situation kama hizi.
 
Back
Top Bottom