Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Walipe Kodi,wanapenda faida kubwa,risiti hawatoi,wakitoa wanaandika mauzo 20% ya walichouza,Kama ukilipa Kodi faida hakuna,katafute shughuli nyingine
Hizo kodi zinazopigwa na Mafisadi wa CCM na kununulia MaV8?!

Kama Viongozi wenyewe wanakula kwa urefu wa kamba waacheni nao waibe.
 
Punguza roho mbaya
That’s just cheap.

Waziri anazungumza TRA wawataarifu wafanyabiashara nyaraka za kuwa nazo kwenye tax estimates. Wakati hayo maelezo yapo kwenye VAT na Income Tax acts.

Hakuna kitu TRA wanafanya nje ya sheria na ni jukumu la mfanyabiashara pia kuzijua hizo sheria.

Sasa watu wanalalamika hawajui nyaraka za kuwa nazo badała ya kuwaelekeza kwenda kwenye vifungu vya sheria, unataka TRA itoe maelezo; uoni shida kubwa hapo ni hao wafanyabiashara kuzoea kufanya kazi kiholela kama hawajui hata sheria gani zinawataka watunze nyaraka gani au wawe nazo.
 
Ukiachana na kupaniki Kwa Chalamila ila Kuna sehemu alikuwa na point,kasema changamoto nyingine ni za kisheria huwezi tatua leoleo.Hapo ndo naona Tatizo lilipo.Wakati Sheria zinapitishwa na bunge Kila mtu huwa anasifia,zikishaanza kufanya kazi ndo tunastuka.Wenzetu wakenya wanazistukia kabla Sheria hazijapitishwa
 
Mwigulu ni economist sio accountant...
Mtazamo wangu hata mtu awe vipi masuala ya kikodi ni masuala ya kikodi.

Wanasiasa wetu wana upungufu siyo wa usomi bali dhamira. Hata mtu aliyesomea uandishi wa habari anaweza kuwa Waziri bora wa fedha kama akiwa amejawa dhamira njema kwa taifa letu.

Wataalam wa wizara wengi Wana weledi kwenye nyanja mbali mbali kuhusu utawala na Usimamizi wa fedha. Tatizo watunga sera wanataka nini!?

Usomi wa mtu huzidiwa na mitizamo ya kisiasa...
 
Ukisikiliza malamimiko ya kodi sehemu kubwa ni kutoka kwa wafanyabiashara wadogo ambao hawana access za accountants au wataalamu wa kodi.

Shida sio waziri (labda mitizo yake kwa wananchi), Iła kwenye biashara 90% ya malalamiko ni uelewa mdogo wa maswala ya tax administration.
 
Bila shaka wewe ni mmojawapo wa watumishi wanaowakandamiza wafanyabiashara kwa kisingizio cha uelewa mdogo wa wafanyabiashara.
 
🤣🤣 chalamila akaenda kuwatisha kwa kutumia mifano ya Manji na Congo.
 
Bila shaka wewe ni mmojawapo wa watumishi wanaowakandamiza wafanyabiashara kwa kisingizio cha uelewa mdogo wa wafanyabiashara.
Ukiwasikiliza tu na kama unaelewa nchi zingine wanavyofanya mambo, unaona shida ipo kwenye elimu ya wafanyabiashara.
 
Cha Ra mirror angekuwa na akili angetajirika kama wenzie kina makonda na sabaya. Wao walijitoa akili Ili wanufaike
 
Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3czView attachment 3024811
Rais samia yeye anachoangalia ni 2025 hata kama hii nchi itapigwa mnada. Yeye hataki kuwavuruga wapigakura wake wa 2025. Wafanyabishara hawataki kulipa kodi na bado wanasikilizwa na wanapewa wanachotaka.

Hii nchi Samia ataiingiza kwenye matatizo makubwa sana kwa tamaa ya madaraka.

Angekua Magu hakuna mtu angeleta huo ujinga.
 
Shida ni kwamba wewe pimbi uko ofsini unafanya kazi chini ya kiyoyozi ma mwisho wa mwezi unalipwa mshahara ndiyo maana unaandika pumba hapa.

Ungekuwa umewahi kufanya biashara ukajuwa namna TRA wanavyo wavizia wafanyabiashara badala ya kuwaeleimisha usingeandika huo utumbo.
 
Wacha kutukumbusha huyo Magu aliyeiba kura zote za mwaka 2020 kwa kuogopa kushindwa uchaguzi. Usiturudishe kwenye ule utawala wa kumwaga damu na kunyang'anya fedha za wafanyabiashara kipitia TASK FORCE.

Muache Rais Samia atumie charisma yake ya kutawala nchi. Siasa za kuua na ubabe tulizizika na Magufuli mwenyewe March 2021
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…