Serikali yasema baada ya miezi miwili itatangaza fursa ya uwekezaji Soko la Kijichi

Serikali yasema baada ya miezi miwili itatangaza fursa ya uwekezaji Soko la Kijichi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa Soko la Kijichi lililojengwa kupitia mradi wa uboreshaji wa Miundombinu ya Dar (DMDP) kwa mkopo wa Benki ya Dunia (WB), linaonekana kama limetelekezwa, DC na Mkurugenzi wa Temeke wametoa Ufafanuzi

Mbunge wa Jimbo la Mtoni, Abdulhafar Idrissa Juma ameuliza swali Bungeni kuwa ni lini Serikali itaanza kutumia Soko na Kituo cha Daladala cha Kijichi, Dar es Salaam?

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange amesema “Soko na Kituo havitumiki kwa ufanisi, hivyo Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wanakamilisha uhambuzi wa kubadilisha matumizi ikiwemo kutafuta mwekezaji atakayewekeza katika Mradi huo ili majengo yaweze kutumika.”

Alipoulizwa kuhusu upembuzi na uchambuzi unaofanywa utakamilika, amesema “Baada ya jitihada za kupeleka Wafanyabishara wadogo kutofanikiwa, andiko limeshawasilishwa kutoka Halmashauri ya Temeke.

"Andiko hilo ambalo linapendekeza kubadili matumizi na tayari Wataalamu wa Ofisi ya Rais wanalipitia, ndani ya miezi miwili tutakuwa tumepata majibu ya nini kinaenda kufanyika na baada ya hapo tutatangaza fursa ya nini kinaenda kufanyika kwa faida ya Wanatemeke na Nchi kwa ujumla.”

Julai 4, 2024, Mwanachama wa JamiiForums.com alisema soko hilo lililojengwa kupitia mradi wa uboreshaji wa Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kwa mkopo wa Benki ya Dunia (WB) na kuzinduliwa Septemba 2019 limetelekezwa.

Akatoa wito Serikali ichukue hatua kwa kuwa fedha za Serikali ndio zimetumika katika mradi huo na hakuna kinachoendelea.

Pia soma
~ Soko la Kijichi (Temeke) limejengwa kwa Mamilioni ya mkopo wa Benki ya Dunia lakini halitumiki, nini hatima yake?
~ Serikali yafikiria kubadili matumizi ya Miundombinu iliyojengwa kwaajili ya Soko la Kijichi (Temeke)
 
Back
Top Bottom