Serikali yasema haijapata taarifa ya Umoja wa Mataifa inayozungumzia kuuawa na kukamatwa kwa wapinzani

Serikali yasema haijapata taarifa ya Umoja wa Mataifa inayozungumzia kuuawa na kukamatwa kwa wapinzani

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Katibu mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome amesema Serikali haijapata taarifa hiyo, na kueleza kuwa watu hao wamekamatwa kwa mujibu wa sheria.

Taarifa iliyotolewa jana katika tovuti ya shirika la Umoja wa Mataifa na Kamishina wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Bi. Michelle Bachelet inadai kuwa viongozi wa upinzani na wafuasi wao 150 wa Bara na Zanzibar wamekamatwa tangu Oktoba 27, siku moja kabla ya wananchi kupiga kura. Bachelet alieleza kusikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani.

Hata hivyo serikali kupitia Profesa Mchome imesema bado haijapata taarifa hiyo na kama ni madai ya watu kukamatwa ni kwa mujibu wa sheria.

“Inawezekana kweli wanaongelea Watanzania, lakini inaweza kuwa ni umbea,” alisema Profesa Mchome.

“Kama watu wamekamatwa ni kwa kuvunja sheria na kama amekamatwa kutakuwa na kitu wametuhumiwa na kama ni hivyo wana nafasi ya kujieleza, waliomkamata wakiridhika wanamwachia. Huo ndio utaratibu wa kisheria.”

Taarifa ya Umoja wa Mataifa hii hapa.

 
“Kama watu wamekamatwa ni kwa kuvunja sheria na kama amekamatwa kutakuwa na kitu wametuhumiwa na kama ni hivyo wana nafasi ya kujieleza, waliomkamata wakiridhika wanamwachia. Huo ndio utaratibu wa kisheria".
Na wale waliouawa kipindi cha uchaguzi huko Pemba, Mtwara, Tunduma, Tarime, Rorya, nk, ni kwa mujibu wa sheria ipi tafadhali?!
 
Ni kama Mbowe tu ,unaangushwa na konyagi alafu unasingizia wasiojulikana, Lema na Nyalandu wamekimbizwa na madeni alafu wanasingizia wanataka kutekwa na Serikali.!
 
Back
Top Bottom