Serikali yasema haiwezi kubadilisha kila kitu kwenye Sheria ya Habari

Serikali yasema haiwezi kubadilisha kila kitu kwenye Sheria ya Habari

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1688663248885.png

Naibu Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano, Kundo Mathew amewataka wadau wa habari kutosheka na maboresho ya Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 akisema ni hatua kubwa imepigwa.

Ameyasema hayo leo Julai 6, 2023 alipokuwa akifunga mradi wa ‘Boresha Habari’ wa taasisi ya Internews, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mabadiliko hayo.

Juni 13, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari, ambapo kati ya mambo 22 yaliyoletwa na wadau, mambo tisa yalikubaliwa.

"Wapo wanaosema hakuna kilichofanyika. Hatuwezi kubadilisha kila kila kitu. Sheria zinapotungwa hazikamiliki ndio maana zinapitiwa kulingana na mahitaji yaliyopo," alisema.

Amesema awali sheria hiyo ilileta mazingira magumu kwa vyombo vya habari, lakini Rais Samia aliona haja ya kuibadilisha.

"Sera na sheria ni sawa na kujenga nyumba, leo unajenga halafu unaona kuna kasoro unarekebisha. Fundi mzuri ni yule anayeweza kujisahihisha mwenyewe, unaweza kujenga halafu ukasema hapo palipopinda nipanyooshe," amesema.

Kutokana na maboresho hayo, Mathew amesema Serikali sasa itaanza kutoa matangazo kwa vyombo vya habari kwa kuzingatia ushindani.

Pia alisema Serikali inakusudia kuja na sheria ya habari moja itakayounganosha wadau wote na kutekeleza yote yanayotakiwa katika maboresho ya Sheria ya Huduma za habari.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mathew amezungumzia kuondolewa kwa tozo za miamala ya simu akisema: “Ni hatua za kujisahihisha kwa serikali. Sasa kuna mtu atasema najitekenya halafu nacheka mwenyewe, sawa. Kama naweza kujisahihisha mwenyewe kwa nini nisubiri mtu mwingine.”

"Uongozi wa Rais Samia ni down-up (chini kwenda juu), sisi tunapeleka mapendekezo, yeye anaangalia kisha anapitisha, kama ni lawama mtulaumu sisi. Kama ni kujitekenya niko tayari kujitekenya," amesema.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema miongoni mwa maboresho yaliyofanywa ni pamoja vifungu vinavyomwondolea mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo uwezo wa kuchagua vyombo vya habari vya kuwapa matangazo.

"Sisi tunaovaa viatu ndio tunajua wapi panabana," amesema.

Akizungumzia mradi wa Boresha Habari, Mkuu wa mradi huo, Agnes Kayuni alisema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa zaidi ya waandishi wa habari 5,000.

Mkurugenzi wa Nukta Afica, Nuzulac Dausen ambaye taasisi yake ilipata ufadhili, amesema wamefanikiwa kutoa mafunzo ya uandishi wa takwimu kwa zaidi ya waandishi wa habari 1,500.

Wanufaika wengine ni pamoja radio za jamii na vyombo vya habari vya mitandaoni.
 
Back
Top Bottom