Serikali yasema Tanzania ina Diaspora Milioni 1.5

Serikali yasema Tanzania ina Diaspora Milioni 1.5

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Bunge la 12 Mkutano wa 11, Kikao cha Saba, Ijumaa Aprili 14, 2023

SERIKALI YASEMA TANZANIA INA DIASPORA MILIONI 1.5
Takwimu hizo za Diaspora ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi za Kibalozi za #Tanzania zilizopo nje ya Nchi

Naibu Waziri, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema Wizara inakamilisha mfumo wa kidigitali ambao unatarajiwa kukamilika Juni 2023 utakaowezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu za Watanzania wanaoshi nje ya Nchi
 
Wapo nchi gani?
Last time walisema Oman wapi laki nne.. UK laki 2.. USA laki na themanini...
Hao wengine wapo wapi?
Wataje Tujue Walipo Kama Mataifa Yaliyoendelea Yanavyojua Wapo Raia Wake
 
Kwa hivyo remittances zinatakiwa zisadifu hiyo figure
 
Wamehesabu na hawa mateja huku SOUTH AFRICA au? Ifike point diaspora isichukuliwe kama jina bali hii ni Status na ili uitwe hivyo ni lazima uwe na shughuli maalum huko majuu.
 
Wapo nchi gani?
Last time walisema Oman wapi laki nne.. UK laki 2.. USA laki na themanini...
Hao wengine wapo wapi?
Yaani wanakalibia idadi ywananchi ya Zanzibar!
 
Bongo ina wazamiaji zaidi milioni tano.
 
Wapo nchi gani?
Last time walisema Oman wapi laki nne.. UK laki 2.. USA laki na themanini...
Hao wengine wapo wapi?
Kila mmoja akitumia Dola kumi za marekani kwenye akaunti ya serikali ya diaspora,hatupati hela za madawati,matundu ya vyoo nk?
 
Mbona ni Uongo, maana idadi ya Passport ni chini ya 400,000 na hii ni taarifa ya Uhamiaji, je hao Watanzania hawana passport?
 
Mbona ni Uongo, maana idadi ya Passport ni chini ya 400,000 na hii ni taarifa ya Uhamiaji, je hao Watanzania hawana passport?
Diaspora ni pamoja na watoto wao labda waliozaliwa huko
 
Mbona ni Uongo, maana idadi ya Passport ni chini ya 400,000 na hii ni taarifa ya Uhamiaji, je hao Watanzania hawana passport?
Je hesabu hiyo ya passport laki 4 ni hizi mpya?Watu wameanza kusafiri nje ya Nchi miaka 60 iliyopita.
Kuna diaspora wana wajukuu.Nchi nyingi hawajajiandikisha na wengi hawana information ya nini cha kufanya.Balozi zetu ni lazima zijirekebishe ili kupata idadi kamili ya diaspora ili wakipewa status waweze kushiriki kwenye ujenzi wa Taifa bila hofu ya kusumbuliwa au kurushwa uwekezaji wao.
 
Bunge la 12 Mkutano wa 11, Kikao cha Saba, Ijumaa Aprili 14, 2023

SERIKALI YASEMA TANZANIA INA DIASPORA MILIONI 1.5
Takwimu hizo za Diaspora ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi za Kibalozi za #Tanzania zilizopo nje ya Nchi

Naibu Waziri, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema Wizara inakamilisha mfumo wa kidigitali ambao unatarajiwa kukamilika Juni 2023 utakaowezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu za Watanzania wanaoshi nje ya Nchi

Wana msaada gani kwa taifa hasa kwenye nyanja ya kiuchumi nadhani hii ndo ingekwa logical zaidi!!
 
Hati ya kusafiria tu kimbembe kuipata yani tunafanya mambo kizamani sana ndio maana Watanzania wengi hawasafiri nje ya nchi yao vikwazo lukuki kabla hata ya safari hata walioko nje ya Nchi wengi wao wako na Hati mbili za kusafiria maana washaukana Utanzania wao ingawa wanaficha hawaweki wazi uhamiaji waache kufanya kazi kwa mazoea wana kazi kubwa sana ya kufanya commissioner ana kibarua kikubwa sana
 
Back
Top Bottom