Tetesi: Serikali yashindwa kulipa wakandarasi, mradi wa SGR Mwanza wasimama

Tetesi: Serikali yashindwa kulipa wakandarasi, mradi wa SGR Mwanza wasimama

ze jj

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
497
Reaction score
592
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
 
Mradi wa sgr mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa
Kwahiyo source yako ni kibarua? Kama amefukuzwa kazi atakwambia?
 
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
Alafu wakute majukwaani huku Ndio utajua
CCM ni watoto wa Mjini
 
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
Wakamilishe ya Morogoro kwanza ianze kazi
 
Hicho si kipande nilisikia kinajengwa kwa mkopo na benk flan ya watu wa china?..... si ni kwamba serikali haiusiki na malipo au mimi ndo sikuelewa?
 
Haya niliyahisi mapema mnooo, huku bandarini nako DPW keshaanza kutia jamba jamba kupandisha charges za port, siku si nyingi tutaanza kumuelewa Mwabukusi
 
Ni kweli hakuna kinachoendelea hapa Mwanza katika ujenzi wa SGR.
 
Nilisema mapema miradi ya Mwanza itasimama,Airport Mwanza na daraja la Busisi vimesimama pia. Vipi huko kwingine lakini tusikate tamaa ndiyo mwaka wa fedha unaanza
 
Muda siyo mrefu utasikia tumekopa trillioni kadhaa kwa ajili ya SGR. Watasema mikopo bado ni himilivu. Tufike mahali mikopo tunayopata ithamanishwe na miradi iliyotekelezwa na mikopo hiyo. Muda siyo mrefu mikopo itatiririka. Hii yote ni mzigo kwa wananchi.
 
Kuna wale mumiani wanaimba mapambio ya record za kupikwa makusanyo ya TRA kama kasuku.

Huo mradi umesimama kitambo tu,ni tuta pekee ndiyo linaweza kuwa zaidi ya 80% illhali mkataba ilikuwa mkandarasi akabidhi Juni 2024.

Hata Makutu-Tabora ni juzi tu Waturuki wamepiga barua wafanyakazi warudi kwao hakuna hela.
 
Matumizi yanapozidi mno mno makusanyo! Wachumi wetu huko mipango sijui wanasemaje!
 
Back
Top Bottom