Tetesi: Serikali yashindwa kulipa wakandarasi, mradi wa SGR Mwanza wasimama

Tetesi: Serikali yashindwa kulipa wakandarasi, mradi wa SGR Mwanza wasimama

Kuna wale mumiani wanaimba mapambio ya record za kupikwa makusanyo ya TRA kama kasuku.

Huo mradi umesimama kitambo tu,ni tuta pekee ndiyo linaweza kuwa zaidi ya 80% illhali mkataba ilikuwa mkandarasi akabidhi Juni 2024.

Hata Makutu-Tabora ni juzi tu Waturuki wamepiga barua wafanyakazi warudi kwao hakuna hela.
Mkuu tunakusanya mara mbili zaidi ya yule shujaa wenu hakuna mradi umesimama wanaosema hivyo ni sukuma gang tu wanatetea legacy.

Kabla hujanishambulia tafakari kidogo.
 
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
Hii Ni kweli..Serikali ni bora ingewapa wachina wamalizie mradi kwa mkopo!
 
Hicho si kipande nilisikia kinajengwa kwa mkopo na benk flan ya watu wa china?..... si ni kwamba serikali haiusiki na malipo au mimi ndo sikuelewa?
Export-Import Bank of China (EXIM) hawa ni nyoko mzee. Ulizia SGR Kenya.

China itakuja kumiliki nchi za Africa tuendako kwa kuendekeza mikopo.
 
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
Nasikia na bomba la mafuta lile la Uganda pesa zimekuwa changa moto
 
SGR Lot 2 na 3 haijaisha....mambo mengi sanaa....Yepi nao wamesimama....wale wa kusifu na kuabudu
 
Mradi wa SGR Mwanza umesimama baada ya serikali kushindwa kulipa wakandarasi. Mmoja wa vibarua kwenye mradi huo amenambia walitangaziwa na wakandarasi kuwa hakuna pesa hivyo shughuli zinasimama mpaka serikali itakapolipa.
Miradi mingi imesimama kwa changamoto ya pesa , hazina hakuna pesa, Kuna mikataba mingi ya ujenzi imesainiwa lakina ujenzi umesimama kwa vile wakandarasi hawajapewa pesa ya advance.
 
Back
Top Bottom