Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Wangefunga mipaka ya nchi kwanza.....kufunga shule na colleges naona nikama ku overate covid 19, hapa kwetu kwanza naona wanafunzi wako salama kubaki mashuleni, kuliko kuwaruhusu wazurule mitaani na kuchangamana na watu wengi......

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly yes, hivi vitoto kuwa shule chini ya uangalizi makini wa waalim ni kinga tosha kuliko kuwaacha wazurure mitaani,

Kwan waathirika wa virus kuingia shule ni nadra sana, ila humo mitaani wanaweza kuwa wengi

Hivyo mtaani na shule, mtaani waliko n hatari sanaaaa kuliko shule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suali zima la kufunga shule, vyuo vya kati na vyuo vikuu wakati mipaka bado iko wazi inashangaza sana. Kila mtu alijua zamani kuwa ugonjwa haupo Tanzania, na njia pekee ya ugonjwa huo kuingia Tanzania ni kwa watu kuwasilini na ugonjwa kutoka nchi nyengine hususan china, lakini Serikali yetu imekataa kabisa kuzuia wachina kuingia nchini na pia watu kutoka nchi mbali mbali wanaruhusiwa kuingia nchini baada ya tu kupimwa wanapowasili. Sote Tumekuja gundua kuwa either vifaa vinavyotumiwa kupima wanaowasili nchini aidha havifanyi kazi sawia au wapimaji hawajui kuvitumia, maana mgonjwa wa mwanzo Tanzania akitokea ubelgiji alipimwa uwanja wa ndege na kupewa all clear ilhali huko alikotoka alikaa katika nyumba ambayo ilipata mgonjwa. Tumesahau ule msemo tahadhari kabla ya athari.
 
Walikuwa wanawacheka wachina walipojenga hospital haraka haraka kwa siku 10 kwa ajili ya huu ugonjwa..hawakujua utafika mpaka huku
Leo wanaomba hiki kikombe kiwapite!. Kipo kwenye menu sasa, kazi ni kwao kuipooza au kunywa ikiwa ya moto.
 
"Nyoka anapoingia nyumbani, kabla ya kuanza kupambana na nyoka huyo kwanza, siyo busara kuanza kubishana nyoka amepitia wapi, nani alizembea, tufanyeje asiingie tena."
-- H. E. Yoweri Museveni, miaka imepita aliposema hayo. paraphrased.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha masomo kwa vyuo vikuu na vya kati nchini kuanzia leo March 18, 2020 ili kujikinga na virusi vya Corona, waliofunga wametakiwa kutorudi vyuoni “vyuo vya ualimu vilitakiwa kufanya Mitihani mwezi May, Waziri afanye marekebishisho ya ratiba yao”

View attachment 1391653









========Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa walikuwa wamesitisha masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari zote nchini.Lakini leo serikali imeongeza kusitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vukuu vyote nchini."Sasa leo tunaendelea kuongeza vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu vyote nchini, navyo pia tunasitisha kuendelea na masomo.Tunatambua vyuo vikuu wanafunzi wengi wako likizo na sasa tunawataka kutokurudi kwenye vyuo vyao, na wale wachache waliokuwa wamebaki kwa ajili ya mitihani nao waondoke mara moja ili kuondoa misongamano kwenye maeneo hayo ya vyuo.Tunavyo zungumzia vyuo vya kati tunazungumzia vyuo vya ufundi na vyuo vya ualimu, tunatambua wanafunzi wa vyuo vya ualimu walitarajia kufanya mitihani mwezi mei mwaka huu, namwagiza waziri wa elimu kufanya marekebisho kwenye mihula yao, kama ambavyo tulimtaka kufanya marekebisho kwenye mihula ya shule za sekondari kidato cha sita."
Free Mode

See Photos
Habari Njema.........nisaidie ku SHARE
-China imefunga hospitali yake ya mwisho ya Corona Virus. Hakuna maambukizi mapya ya kutosha kufanya hospitali hizo ziendelee kuwepo.
- Madaktari nchini India wamefanikiwa kutibu maambukizi ya virusi vya Corona. Mchanganyiko wa dawa uliotumika ni Lopinavir, Retonovir, Oseltamivir pamoja na Chlorphenamine.Wanatarajia kupendekeza matumizi ya dawa hizi duniani kote.
-Watafiti wa kituo cha Erasmus Medical Center wanadai kuipata kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
-Mkongwe wa miaka 103 kutoka Nchini China amepona kabisa maambukizi ya COVID-19 baada ya kutibiwa kwa siku 6 mjini Wuhan, China.
- Kampuni ya Apple imefungua ofisi zake zote 42 nchini China.
-Kliniki ya Cleveland imetengeneza kipimo cha COVID-19 chenye uwezo wa kutoa majibu ndani ya masaa kadhaa, na sio siku.
-Habari njema kutoka Korea Kusini ambapo maambukizi mapya yameendelea kupungua.
- Italy imeathiriwa zaidi, wataalamu wanadai kwamba hii imetokana na kuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye umri mkubwa kuliko nchi zote barani Ulaya.
-Wanasayansi huko nchini Israel wanatarajia kutangaza utengenezwaji wa Kinga ya Corona.
- Wagonjwa watatu wa maambukizi ya Corona mjini Maryland wamepona kabisa maambukizi hayo na wapo fiti kurudi katika mihangaiko ya kila siku.
- Jopo la wanasayansi wa nchini Canada wamefikia hatua nzuri ya utafiti wa COVID-19
- Kampuni ya San Diego Biotech kwa kushirikiana na chuo cha Duke na Chuo cha taifa cha Singapore, wanatengeneza chanjo ya COVID-19.
-Mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 katika jimbo la Tulsa amepona. Mgonjwa huyo alipimwa mara mbili na majibu kuwa hasi, kiashiria kwamba amepona.
-Wagonjwa wote 7 waliokua wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Safdarjung mjini New Delhi wamepona.
- Utegili(Plasma) ya mtu aliyepona maambukizi ya COVID-19 inaweza kutumika kuwatibu wagonjwa wenye maambukizi mapya.
NA MGONJWA WA AWALI NCHINI UFILIPINO, AMEPONA.
Kuna mtu ameandika na nimeipenda.
Kwahiyo, Sio kila wakati tunapata habari mbaya❤.. Tuendelee kupeana tahadhari...
.
https://free.facebook.com/upgrade/?...0398733:1302236903305257&refid=52&__tn__=EH-R



https://free.facebook.com/ufi/reaction/profile/browser/?ft_ent_identifier=1302236903305257&refid=52
 
Back
Top Bottom