Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Serikali yasitisha masomo kwa vyuo vya kati na vyuo vikuu kuanzia tarehe 18/03/2020 ili kupambana na Corona

Kilichonisikitisha tu ni kuruhusu wageni waingie na wakifika airport wanapimwa temperature kisha ukiwa sawa unaambiwa jichanganye uko salama.

Kama yule mama asingejishtukia,angekuwa mtaani,na maisha yangekuwa yanaendelea tu.

Jiulize ni wangapi waliokubaliwa kuingia kwa kupimwa temperature tu?

Nimetoka stand sasa hivi nimeshangaa wanafunzi wa sekondari wanavyohangaika,kuna mvua,ticket wamekosa,msongamano mkubwa,na hakuna maji ya kunawa wala sanitizer

Hata hivyo nina kila sababu ya kuamini Mungu ndiye pekee anatulinda,kwani hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ni nyingi na nyingine hazitekelezeki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko kote ni bure bila kufunga mipaka na viwanja vya ndege. Ona wote waliogundulika navyo hapa nchini,wote wametokea nje. Je tungekuwa tumefunga viwanja vya ndege na mipaka mapema?. Kuna uwezekano tungekuwa self kwa muda mrefu au bila hiyo kitu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atawalisha nani uko karantini
Ok!
Tukiwa na vijiswali hafifu namna hii ni rahisi sana kupukutika wote.

Unawezaje kujenga reli standard gauge ushindwe kununua dona na maharage.
 
Serikali tulivyokuwa tunavuta subra mkatusema kwamba tunazembea, sasa tumeanza kuchukua hatua mnakuja tena kusema hakukuwa na ulazima.

Kwa nini nyinyi kwa nyinyi Wanainchi msikae chini mkaelewana kwanza ndio mje hadharani? mnatuchanganya sana sisi Wanasirikali ati.
 
Serikali imefanya vizuri isipokuwa kwa wale wa bweni naona wangrbaki na kuwekwa karantini. Sababu hivi sasa wanahangaika kwenye mabasi hiyo si hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndicho kipindi ambacho hao wana chuo wata gongwa sana kimasikhraa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Corona inaingizwa nchini haijaanzi nchini kuwanusuru watanzania ni kutoruhusu wageni kuingia au wakiingia wswekwe chini ya uangalizi kwa wiki 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangefunga mipaka ya nchi kwanza.....kufunga shule na colleges naona nikama ku overate covid 19, hapa kwetu kwanza naona wanafunzi wako salama kubaki mashuleni, kuliko kuwaruhusu wazurule mitaani na kuchangamana na watu wengi......

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzazi tekeleza wajibu wako. Ukimwachia mtoto azurule hiyo shida yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afazali mikusanyiko yote isiyo ya lazima imefutwa na yale maharusi na send off zote futilia mbali

Kuna dada yangu mtoto wa mama mdogo amenikalia kooni kila kukicha mchango wa sendoff 200,000

Nazani korona imenisaidia sana no mchango wala waowane kimya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ile mikesha na maombezi ya manabii na mitume wenye mipako itaendelea kama kawaida?
 
Back
Top Bottom