Serikali yasitisha matumizi ya Fomu ya 2C inayotumika kuchukua dawa maduka ya nje

Serikali yasitisha matumizi ya Fomu ya 2C inayotumika kuchukua dawa maduka ya nje

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Fomu ya C2.jpg

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuanzia leo Julai 1, 2022 Serikali imesitisha rasmi matumizi ya fomu ya 2C katika Hospitali zote za umma zinazotumia Bima ya Afya mara baada ya kuonekana kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.

Fomu ya 2C ni karatasi inayoandikwa dawa nakupatiwa mgonjwa akaitafute dawa hiyo nje ya Hospitali au vituo vingine tofauti na alipotibiwa mgonjwa.

Aidha, Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepanga kusimika mitambo 57 ya hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali zote za Rufaa za mikoa, Kanda pamoja na Hospitali za Wilaya nchini.

Hayo yamebainishwa leo Julai Moi, 2022 Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua mtambo maalum wa uzalishaji hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali ya kibingwa ya Benjamin Mkapa uliogharimu Bilioni 1.5 ambapo amesema kituo hicho kitazalisha mitungi 400.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dk. Alphonce Chandika amesema kabla yakufungwa mitambo hiyo kipindi cha mlipuko wa Uviko 19, Hospitali hiyo ilikua inatumia mitungu 200 kwa siku kwa kutumia gharama ya shilingi milioni 10 na ilikua ikifwatwa Dar es salaam kwakua wao hawakua na uwezo wakuzalisha hewa ya Oksijeni.

Pia soma: Serikali yazuia wanachama wa NHIF kwenda kuchukua dawa maduka ya nje kwa kufuta matumizi ya form 2c
 
Hii siyo haki kabisa,kama kuna udanganyifu wawatafute wanaofanya udanganyifu waadhibiwe kuliko kuwaadhibu watu wote Kwa makosa ya wachache. Hii inaondoa maana ya kuwa na bima. Huyu Waziri naye ni mkurupukaji sana.
 
Hawajali, Umi doesn't care.

Mwaka ule mama mzazi alipolazwa kcmc dawa nyingi tulinunua maduka ya nje, mfano ile dawa ya kupaka vidonda vya kutokana na kulala muda mrefu haikuwepo pale, tulinunua nje.

The same Mr. alipolazwa pale rufaa mbeya mkanichangia nauli humu, dawa alizoandikiwa tulinunua nje, kila siku elfu 50, daily.

All hapo was so sorry, Bwana Mungu akawachukua.

Kufuta huu utaratibu wa kununua dawa maduka ya nje ni mateso kwa watu wa bima.

Though they will not care.
 
nilijua lazima zoezi litafeli tu,kuna kigogo fulani ana pharmacy zaidi ya 20 zote zipo jirani na hospital.
Na ili la form 2c nalo linaenda kufeli vibaya.
:Adui wa serikali ni viongozi wake wenye vyeo vya juu ndio wanaomiliki biashara zote kubwa.
Huyo kigogo yupo serikalini?
 
Back
Top Bottom