Serikali yasitisha matumizi ya Fomu ya 2C inayotumika kuchukua dawa maduka ya nje

Serikali yasitisha matumizi ya Fomu ya 2C inayotumika kuchukua dawa maduka ya nje

View attachment 2278302
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuanzia leo Julai 1, 2022 Serikali imesitisha rasmi matumizi ya fomu ya 2C katika Hospitali zote za umma zinazotumia Bima ya Afya mara baada ya kuonekana kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.

Fomu ya 2C ni karatasi inayoandikwa dawa nakupatiwa mgonjwa akaitafute dawa hiyo nje ya Hospitali au vituo vingine tofauti na alipotibiwa mgonjwa.

Aidha, Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepanga kusimika mitambo 57 ya hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali zote za Rufaa za mikoa, Kanda pamoja na Hospitali za Wilaya nchini.

Hayo yamebainishwa leo Julai Moi, 2022 Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua mtambo maalum wa uzalishaji hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali ya kibingwa ya Benjamin Mkapa uliogharimu Bilioni 1.5 ambapo amesema kituo hicho kitazalisha mitungi 400.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dk. Alphonce Chandika amesema kabla yakufungwa mitambo hiyo kipindi cha mlipuko wa Uviko 19, Hospitali hiyo ilikua inatumia mitungu 200 kwa siku kwa kutumia gharama ya shilingi milioni 10 na ilikua ikifwatwa Dar es salaam kwakua wao hawakua na uwezo wakuzalisha hewa ya Oksijeni.

Pia soma: Serikali yazuia wanachama wa NHIF kwenda kuchukua dawa maduka ya nje kwa kufuta matumizi ya form 2c
Sasa mbadala wake ni upi? Maana huwa tunaambiwa dawa hakuna ndiyo tunakwenda huko.
 
Kama hiyo hospital au kitu cha afya hakina dawa magonjwa anafanyaje?
Hili swali inabidi aulizwe wazir ummy
Maana wao kutwa wanasema hospitality kuna madawa kedekede

Ova
 
Hapo waziri kafeli,labda NHIF watatupatia ela za kwenda kununua hizo dawa nje ya hospitali kwasabab tunajua tu hospital zetu za serikal baadh ya dawa hawana,
Sasa umuhimu wa bima upo wapi kama mgonjwa itamgharim tena kutumia pesa zake za mfukon kutafuta dawa ambazo atazikosa hospitalin..
 
View attachment 2278302
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuanzia leo Julai 1, 2022 Serikali imesitisha rasmi matumizi ya fomu ya 2C katika Hospitali zote za umma zinazotumia Bima ya Afya mara baada ya kuonekana kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.

Fomu ya 2C ni karatasi inayoandikwa dawa nakupatiwa mgonjwa akaitafute dawa hiyo nje ya Hospitali au vituo vingine tofauti na alipotibiwa mgonjwa.

Aidha, Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepanga kusimika mitambo 57 ya hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali zote za Rufaa za mikoa, Kanda pamoja na Hospitali za Wilaya nchini.

Hayo yamebainishwa leo Julai Moi, 2022 Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua mtambo maalum wa uzalishaji hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali ya kibingwa ya Benjamin Mkapa uliogharimu Bilioni 1.5 ambapo amesema kituo hicho kitazalisha mitungi 400.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dk. Alphonce Chandika amesema kabla yakufungwa mitambo hiyo kipindi cha mlipuko wa Uviko 19, Hospitali hiyo ilikua inatumia mitungu 200 kwa siku kwa kutumia gharama ya shilingi milioni 10 na ilikua ikifwatwa Dar es salaam kwakua wao hawakua na uwezo wakuzalisha hewa ya Oksijeni.

Pia soma: Serikali yazuia wanachama wa NHIF kwenda kuchukua dawa maduka ya nje kwa kufuta matumizi ya form 2c
Ikiwa una BIMA ya NHIF ili kuepuka kukosa dawa kwenye vituo vya afya vya umma ni kheri kwenda Hospital kubwa za Private tu.
 
Hakunaga bima ya Hovyo hovyo kwenye kujali wateja kama NHIF, mimi nina bima mbili moja ni NHIF (Kama mtegemezi) na ingine premium ya kampuni binafsi ila sikumbuki mara ya mwisho nimetumia lini hii NHIF, kero yangu ilitokana na kukataliwa dawa za kawaida kabisa eti zina bei….hawa watawala wakae wakielewa ile ni BIMA ambayo watumishi wanakatwa fedha. Sasa kama dawa hizo hazipo hospitali mgonjwa atafanyaje?

Ni kama watawala wanaona NHIF ni fadhila, ngoja tuone wanachotaka hatma yake ni nini!
 
Hivi kwa nini silika ya mtu mweusi ni wizi wizi tu nini kinaweza kufanyika
 
Itafeli tu ummi alidhani kwa kuwa yeye anakuwa kwa v8 kila mtu ana v8 tusibir huo mwez wa 9 ndo wanazuia kwa hospital za wilaya na huko ndo penye walalahuo wengi
 
Hii siyo haki kabisa,kama kuna udanganyifu wawatafute wanaofanya udanganyifu waadhibiwe kuliko kuwaadhibu watu wote Kwa makosa ya wachache. Hii inaondoa maana ya kuwa na bima. Huyu Waziri naye ni mkurupukaji sana.
Hilo lakuzuia ndo mwisho wa akili wa wasomi wetu.Hatunaga uwezo wakutafuta ufumbuzi wa changamoto zetu ndo maana tunakimbilia kukataza.
 
Back
Top Bottom