John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa Tozo ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi. Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).