Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,149
- 6,994
Ukiwa mwizi,kila unayemuona,unafikiria ni mwizi kama ulivyo.Mimi nikishaona tu naniliu nakuwa nanusa harufu ya upigaji tu[emoji205]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiwa mwizi,kila unayemuona,unafikiria ni mwizi kama ulivyo.Mimi nikishaona tu naniliu nakuwa nanusa harufu ya upigaji tu[emoji205]
Mbona haijasainiwa na viongozi wa wizara husikaKutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa Tozo ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi. Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Ni wajinga tu ndio watasikiliza upuuuzi huo wanaotuambia. Mtu anakwambia anapunguza bei wakati waliongeza kilanguzi na sasa bei ya mafuta inapanda maradufu zaidi which means hiyo 100 wanayotoa ni unafiki tu hakuna nafuu yoyote maana bei itakuwa juu maradufu juu ya hiyo.Ni jambo jema!
Mafuta yameshapanda bei kwenye soko la dunia hapatakuwa na unafuu wowote!
Kwa kusitisha hadi huo mudanina maana wakija kuirudisha itakuwa Tsh 200!?Kutokana na kuendelea kupanda kwa Bei za Mafuta katika Soko la Dunia, Serikali imeondoa Tozo ya Tsh. 100 kwa kila Lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa zilizopaswa kulipwa kwa miezi mitatu zaidi, kuanzia Machi hadi Mei 2022
Kupanda kwa bei kumetokana na sababu mbambali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine. Serikali imesema Bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika Machi 02, 2022 zitazingatia marekebisho hayo
View attachment 2134074
Huu ni ujinga, yaani unaondoa chanzo ambacho Kiko committed kwenye kugharamia barabara za Tarura?Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa Tozo ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi. Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Umemjibu vizuri sana na kwa mifano hai, nakupongeza mnoKuna mnyonge,asiyetumia petrol,disiel na mafuta taa?Kama hana gari,atapanda bodaboda pikipiki,bajaji,daladala,atakula samaki wanaovuliwa kutumia mashine zinazotumia petrol.Atatumia kuni,mkaa bidhaa mbalimbali,bidhaa za sokoni:nyanya,nazi,ndimu,limau,bamia nk vinavyobebwa na magari yanayotumia dizeli.Mafuta ya taa ,atatumia kwenye taa,kutumia jiko la mafuta,kuwasha moto wa kuni au mkaa.
NonsenseKutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa Tozo ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi. Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Akili yako ya ajabu sana...yaani hujui hiyo vita ndio chanzo cha hayo mabadiliko????...Hizi ndizo HABARI MPASUKO, siyo mambo ya Vita vya ukabila vya wazungu!
Asante GENIUS akili iliyotukuka!Akili yako ya ajabu sana...yaani hujui hiyo vita ndio chanzo cha hayo mabadiliko????...
Hahahaha
Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Usishangae wameondoa mia, watapongeza mia tatu kwenye mafuta.Mafuta hayatumiki kwa wenye magari tu,hata asiye na gari anayatumia,ukipanda pikipiki bodaboda,ukipanda bajaji,ukipanda daladala, bus,unatumia mafuta.Ukinunua bidhaa yoyote ujuwe mpaka imekufikia wewe karibu yako,kumetumika mafuta.Ukiona nyanya,kitunguu,nazi,pilipili,mchicha,sembe,ngano nk,vimefika ulipo,ni.mafuta yametumika kwa ajili ya wewe uvipate.jengo lolote,unalotumia kwa makazi,masomo,afya,kumetumika usafiri wa kufanya liwepo hapo ilipo.Mwanao,ndugu,wewe mwenyewe,shule uliyosoma bila mafuta isingekuwapo hapo ulipo.
Telegramu "NISHATI". Mji wa Serikali -Mtumba,
Simu: (255)-26-2322018 Mtaa wa Nishati,
Nukshi: (255)-26-2320148 S. L. P. 2494,
Barua Pepe: ps@nishati.go.tz DODOMA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia
kunakosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine,
mwenendo wa bei za mafuta nchini umeathirika kwa bei hizo kuendelea kupanda.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya
Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa, zilizopaswa kulipwa na
watumiaji wa mafuta nchini kwa muda wa miezi mitatu zaidi kuanzia mwezi Machi
2022 hadi Mwezi Mei 2022 huku ikiendelea kutathmini mwenendo wa bei za mafuta
katika soko la dunia.
Pamoja na kwamba uamuzi huu utaipunguzia Serikali mapato ya kiasi cha Shilingi
bilioni 30 kwa mwezi, Serikali imeona ni muhimu kuendelea kuwalinda wananchi wake
dhidi ya athari za mabadiliko ya bei za mafuta ulimwenguni. Hii inatokana na ukweli
kwamba endapo uamuzi huu usingechukuliwa na Serikali, bei za mafuta nchini kuanzia
mwezi Machi na kuendelea zingekuwa za juu sana kutokana na sababu zilizoelezwa
hapo juu.
Kwa msingi huo, Mheshimiwa January Makamba (Mb), Waziri wa Nishati,
ameidhinisha na kusaini marekebisho ya kanuni inayohusika na Tozo hiyo ili kutimiza
uamuzi huu wa Serikali.
Uamuzi huu unaenda sambamba na maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoyatoa baada ya kikao na
Wizara na taasisi mbalimbali zinazohusika na suala hilo zilizokutana tarehe 5 Oktoba
2021 kujadiliana namna bora ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini na kupunguza
tozo mbalimbali zenye thamani ya Shilingi bilioni 102 kwa watumiaji wa mafuta nchini
Bei mpya za mafuta zitakazotangazwa na EWURA na kuanza kutumika tarehe 2 Machi
2022 zitazingatia marekebisho hayo ya kanuni yaliyofanywa na Waziri wa Nishati.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA NISHATI : source : Nishati | Publications