John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Serikali imechelewa kuzifuta tozo mbalimbali ilizojiwekea kwani ni kikandamizaji dhidi ya wananchi wake na zilipitishwa na bunge bila kuangalia athari kwa jamii.Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine, Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa Tozo ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi. Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
View attachment 2134065
Mwenye gari nae ni mnyonge?Serikali ya wanyonge inavyojali wanyonge wake
Inapotezaje billion 30 wakati hizo ni pesa zetu walikua wanatuibia??????
Walikurupuka kuweka hii tozo kandamizi kisa tu waliona bei za mafuta zimeshuka wakaona tunafaidi sana kumbe punguzo hilo lilitokana na soko la dunia kuporomoka kwasababu ya Korona.
Kuna mnyonge,asiyetumia petrol,disiel na mafuta taa?Kama hana gari,atapanda bodaboda pikipiki,bajaji,daladala,atakula samaki wanaovuliwa kutumia mashine zinazotumia petrol.Atatumia kuni,mkaa bidhaa mbalimbali,bidhaa za sokoni:nyanya,nazi,ndimu,limau,bamia nk vinavyobebwa na magari yanayotumia dizeli.Mafuta ya taa ,atatumia kwenye taa,kutumia jiko la mafuta,kuwasha moto wa kuni au mkaa.Wanasitishiana tozo za matajiri tu za wanyonge zinaachwa palepale
Mafuta hayatumiki kwa wenye magari tu,hata asiye na gari anayatumia,ukipanda pikipiki bodaboda,ukipanda bajaji,ukipanda daladala, bus,unatumia mafuta.Ukinunua bidhaa yoyote ujuwe mpaka imekufikia wewe karibu yako,kumetumika mafuta.Ukiona nyanya,kitunguu,nazi,pilipili,mchicha,sembe,ngano nk,vimefika ulipo,ni.mafuta yametumika kwa ajili ya wewe uvipate.jengo lolote,unalotumia kwa makazi,masomo,afya,kumetumika usafiri wa kufanya liwepo hapo ilipo.Mwanao,ndugu,wewe mwenyewe,shule uliyosoma bila mafuta isingekuwapo hapo ulipo.Mwenye gari nae ni mnyonge?