Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
SERIKALI YATAJA SARATANI TANO ZINAZOSUMBUA WANANCHI KANDA YA ZIWA, MBUNGE KABULA SHITOBELA AHOJI BUNGENI
Serikali imetaja aina tano za saratani zinazoongoza Kanda ya Ziwa ambazo ni ya kibofu cha mkojo, mji wa uzazi wa uzazi, damu, macho na figo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ameliambia bunge Jumatatu Aprili 14, 2025 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Kabula Shitobela aliyeuliza "Ni lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa ili kubaini visababishi vya saratani iliyokithiri"?
Dk Mollel amesema Serikali imefanya utafiti wa kina nchi nzima wa kusaidia kutambua kuwa ni saratani zipi zinaongoza katika kanda ya ziwa.