Serikali yataka umakini na tafiti juu ya kuruhusu matumizi ya bangi

Serikali yataka umakini na tafiti juu ya kuruhusu matumizi ya bangi

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Haya yameelezwa leo April 15,2024, Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkenge, Florent Laurent Kyombo aliyeuliza msimamo wa serikali baada ya baadhi ya nchi kuruhusu matumizi ya bangi kama tiba.

Serikali imesema jambo la kutoa kibali cha kuruhusu kilimo na matumizi ya bangi ni suala ambalo halitakiwi kufanyiwa maamuzi ya haraka, inabidi serikali ijipe muda kufanya tafiti za kutosha ili ifanye maamuzi yenye tija.

"Tunachokifikiri sisi ni kuanza kuwasiliana na vyuo vyetu kuanza kufanya hizo tafiti lakini mjadala wa kuikubali nchi iingie katika kibali cha kutumia bangi na utafiti wa namna moja au nyingine ni lazima tuwe na makubaliano ya pamoja,"alieleza Mhagama."

Ni lazima kama nchi tufanye kwanza tafiti ili tuweze kufanya maamuzi hayo. Waheshimiwa Wabunge bangi mpaka sasa kama taifa tunaiona ni dawa ambayo ina madhara makubwa sana,inaharibu sana afya za vijana wetu."

Mhagama ameeleza suala la bangi kuruhusiwa katika matumizi ya tiba lilifanyika ulimwenguni kupitia Kamisheni kuzuia madawa ya kulevya ambapo nchi nyingi wanachama zilipiga kura na kukubali jambo hilo.

Pia soma

Bangi ihalalishwe, Sheria zinazotumika kuhusu Bangi. Ziende kudhibiti Ushoga

Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa

Kassim Majaliwa: Bangi ya 'Cha Arusha' pamoja na 'Skanka' inafanya watumiaji kuwa vichaa

Serikali iruhusu kilimo cha bangi na ipunguze masharti ya uingizaji wa fedha nchini ili kukabili uhaba wa dola
 
Gongo nayo iruhusiwe, kuna watu wanaingiza kipato kizuri sana ila kwa kujificha.
 
Sijui ni nani alimloga mtu mweusi muafrika?

Tumbaku ni SUMU, inasababisha magonjwa ya saratani n.k

Bangi, ganja, msubaa, kijiti, cha ukucha, cha arusha ni DAWA

Serikali na watawala hawataki watu wajue ukweli kuhusu Bangi ili waendelee kuwatawala na kuwaswaga kama makondoo kirahisi.

UKOMBOZI WA NCHI HII UTAPATIKANA PALE WALIOLALA WAKIAMKA NA KUTAMBUA MATUMIZI SAHIHI YA BANGI.
 
Hata kama hairuhusiwi lakini imejaa tele mtaani Sasa wanazuia nini
 
Mambo yanaanza kidogokidogo kesho utasikia ushoga nao uruhusiwe kwa sababu nchi nyingine zimeruhusu!
 
vijana wengi mitaani wamepanguka akili kwa Bangi, wacha waone ni mzaha tu.
 
Sijui ni nani alimloga mtu mweusi muafrika?

Tumbaku ni SUMU, inasababisha magonjwa ya saratani n.k

Bangi, ganja, msubaa, kijiti, cha ukucha, cha arusha ni DAWA

Serikali na watawala hawataki watu wajue ukweli kuhusu Bangi ili waendelee kuwatawala na kuwaswaga kama makondoo kirahisi.

UKOMBOZI WA NCHI HII UTAPATIKANA PALE WALIOLALA WAKIAMKA NA KUTAMBUA MATUMIZI SAHIHI YA BANGI.
Oyaaa umenena🔥🔥
 
Mambo yanaanza kidogokidogo kesho utasikia ushoga nao uruhusiwe kwa sababu nchi nyingine zimeruhusu!
Actualy, ushoga ni optional lakin weed nchi jirani zinatumia kama zao la biashara, yaan ndani hawatumii lakini wana export na inaliingizia taifa faida ni suala la regulations
 
Back
Top Bottom