Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Haya yameelezwa leo April 15,2024, Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkenge, Florent Laurent Kyombo aliyeuliza msimamo wa serikali baada ya baadhi ya nchi kuruhusu matumizi ya bangi kama tiba.
Serikali imesema jambo la kutoa kibali cha kuruhusu kilimo na matumizi ya bangi ni suala ambalo halitakiwi kufanyiwa maamuzi ya haraka, inabidi serikali ijipe muda kufanya tafiti za kutosha ili ifanye maamuzi yenye tija.
"Tunachokifikiri sisi ni kuanza kuwasiliana na vyuo vyetu kuanza kufanya hizo tafiti lakini mjadala wa kuikubali nchi iingie katika kibali cha kutumia bangi na utafiti wa namna moja au nyingine ni lazima tuwe na makubaliano ya pamoja,"alieleza Mhagama."
Ni lazima kama nchi tufanye kwanza tafiti ili tuweze kufanya maamuzi hayo. Waheshimiwa Wabunge bangi mpaka sasa kama taifa tunaiona ni dawa ambayo ina madhara makubwa sana,inaharibu sana afya za vijana wetu."
Mhagama ameeleza suala la bangi kuruhusiwa katika matumizi ya tiba lilifanyika ulimwenguni kupitia Kamisheni kuzuia madawa ya kulevya ambapo nchi nyingi wanachama zilipiga kura na kukubali jambo hilo.
Pia soma
Bangi ihalalishwe, Sheria zinazotumika kuhusu Bangi. Ziende kudhibiti Ushoga
Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa
Kassim Majaliwa: Bangi ya 'Cha Arusha' pamoja na 'Skanka' inafanya watumiaji kuwa vichaa
Serikali iruhusu kilimo cha bangi na ipunguze masharti ya uingizaji wa fedha nchini ili kukabili uhaba wa dola