Serikali yatangaza ajira za ualimu kwa mwaka 2024 zaidi ya nafasi 11,000

Serikali yatangaza ajira za ualimu kwa mwaka 2024 zaidi ya nafasi 11,000

ivi barua inaandikwa kwa mkono au computer?
 
Somo la kemia lipo kwenye tangazo ila kwenye mfumo hakuna sehemu wanataka u apply mwalimu wa somo KEMIA
 
Mnieleweshe, tofauti ya mwalimu daraja la III B na daraja la III C.

Halafu pia, kwenye tangazo wamesema tuambatanishe na barua ILIYOSAINIWA.. Isainiwe na nani????
 
Mnieleweshe, tofauti ya mwalimu daraja la III B na daraja la III C.

Halafu pia, kwenye tangazo wamesema tuambatanishe na barua ILIYOSAINIWA.. Isainiwe na nani????
IIIB-Diploma
IIIC-Degree
Barua ya kikazi ukimaliza kule chini si unasaini mkuu. Ni hivo tu...saini yako ya mkono iwepo kule down chini(hata km utaichapa)print ....tia saini....then scan uipandishe
 
NAULIZA.!!
Nimesoma diploma ya ualimu wa sekondari-2011. Nikiingia ajira portal ktk acadwmic qualification...chuo hakipo kwenye orodha pale. Je ni sahihi niki click "OTHER" then niandike jina la hiko chuo manually?
2. Pale chini inadai niweke GPA, nimeshindwa kuelewa niweke nn..maana nina cheti tu cha NECTA kikiwa na matokeo ya jumla...hakuna GPA, Au diploma yangu ni outdated...za sasa zina GPA?
3. CV nayo inasainiwa pale chini?
GPA ILIYOPO kwenye transcript
 
Hivi unafikri walimu waliopo mtaani ni wachache? Yaani interview ya somo moja uwafanyie siku moja? Mfano walimu walisomea Kiswahili wapo 50000 utawafanyia interview siku 1, wafanye written, practical na oral kwa siku moja?
Mbona huwa inafanywa kila lep hivyo hivyo na kwa sasa mnafanya kwa computer
 
Tupo hapa tunabishana ,,,

Vyeti tunavyovi -upload kwenye mfumo ,,,

Ni hizi copy tulizo certify kutoka kwa mwanasheria na kuzi-scan ?? Au

Ni hivi vyeti vya kitaaluma ,, tulivyovi -scan ,, ?? ( Vyeti vilivyotumika katika mfumo wa or tamisemi )

Vipi hasa tunavipandisha kwenye mfumo ??..
Vyeti unavyo viweka ni ulivyo vi certify halafu una scan unaviweka
 
Lakin bado nina kigugumiz juu ya usaili. Kuna mtu kamaliza 2015 na hata sehem ya kujitolea kufundishq alikosa akaamuq kujikita kwenye bodaboda, Leo unatangaza ajira na unamuingiza kwenye usaili na Graduate wa 2023 fresh kabisaa kutoka chuo, kichwa bado cha moto. Freshers ananafasi nzuri zaidi ya kupita kwenye usaili na kupata ajira huku yule wa 2015 akiendelea kufukuza upepo
Ndio inavyokuwaga
Hata kazi zingine ni hivyo
 
Wakuu naweza peleka vyeti kwa mwanasheria kwa niaba ya watu?
Pia gharama ni kiasi Gani kupigiwa muhuri?
 
Wakuu naweza peleka vyeti kwa mwanasheria kwa niaba ya watu?
Pia gharama ni kiasi Gani kupigiwa muhuri?
Pelekeni mahakama ya mwanzo Elfu 10 tu.

Ukijichanganya kwa hawa vibaka wanajiita wasomi kila cheti wanataka wasaini elfu 10 na mtu una vyeti 5
 
Hivi unafikri walimu waliopo mtaani ni wachache? Yaani interview ya somo moja uwafanyie siku moja? Mfano walimu walisomea Kiswahili wapo 50000 utawafanyia interview siku 1, wafanye written, practical na oral kwa siku moja?
Sio kwamba saili zote 3 zinafanyika kwa siku 1...Mkishafanya written wanatoa matokeo wale waliofaulu watafanya practical siku nyingine watatoa tena matokeo watakaofaulu watafanya oral siku nyingine tena then mnasubiri kuitwa kazini sasa
 
Back
Top Bottom