Serikali yatangaza ajira za ualimu kwa mwaka 2024 zaidi ya nafasi 11,000

Serikali yatangaza ajira za ualimu kwa mwaka 2024 zaidi ya nafasi 11,000

Wakuu Kwa wazoefu WA kuomba Kazi ajira portal ,....

Kipi Bora katika barua ya maombi ,kutumia kiswahili au kiingereza ....?

Tulikuwa tushazoe mfumo wetu WA oteas uliokuwa unatuambia kabisa tuandike barua Kwa mkono Tena ya kiswahili ...
 
Set namna hii..

Kama wewe ni Mwalimu wa Mathematics halafu kipindi upo Chuo kozi yako iliitwa Bachelor of Science with/in Education lakini ukaspecialize kwenye Mathematics.

Sasa hapo Ajira portal andika BACHELOR OF EDUCATION IN MATHEMATICS kwenye sehemu ya professional qualification.

Ukimaliza pale apply hutapata shida tena.

Pia kama ulisoma masomo mawili ya kufundisha andika (mfano)

Bachelor of Education in Geaography and Kiswahili

Bachelor of Education in Physics and Mathematics

Bachelor of Education in Chemistry and Biology

n.k
Mkuu mwl wa certificate akiweka chet kwenye academic qualifications kinagoma maana hawana transcript ya chuo wana cheti chenye matokeo kama form four
 
Wakuu Kwa wazoefu WA kuomba Kazi ajira portal ,....

Kipi Bora katika barua ya maombi ,kutumia kiswahili au kiingereza ....?

Tulikuwa tushazoe mfumo wetu WA oteas uliokuwa unatuambia kabisa tuandike barua Kwa mkono Tena ya kiswahili ...
Barua andika kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili. Hii sio Muhimu Sana

Ila vitu ambavyo usije kuthubutu kusahau.
1. Kuweka Picha yako.
2. Kuandika anuani iyoelekezwa.
3. Barua yako ya maombi kusaini.
4. Vyeti vyako vyote kuwa certified.

Ukisahau kimoja kati ya hivyo hautaitwa interview.
 
Mkuu mwl wa certificate akiweka chet kwenye academic qualifications kinagoma maana hawana transcript ya chuo wana cheti chenye matokeo kama form four
Tafuteni msaada kwa PSRS, piga simu eleza hiyo changamoto
 
Lakin bado nina kigugumiz juu ya usaili. Kuna mtu kamaliza 2015 na hata sehem ya kujitolea kufundishq alikosa akaamuq kujikita kwenye bodaboda, Leo unatangaza ajira na unamuingiza kwenye usaili na Graduate wa 2023 fresh kabisaa kutoka chuo, kichwa bado cha moto. Freshers ananafasi nzuri zaidi ya kupita kwenye usaili na kupata ajira huku yule wa 2015 akiendelea kufukuza upepo
Ndo weakness kubwa ya ajira portal,,anaenufaika ni yule ambae amamaliza juzi lakin wale wa miaka ya nyuma ni ngumu kutoboa maana vitu vingi wamesahau ,mm naona tamisemi palikua panafaa zaidi maana wao ni wengi na ninajua PSRSS Hawawez kumudu usaili wa watu 250,000
 
Diploma hakuna GPA....Ndo maana nauliza au za sasa zinakua na gpa?naomba wenye diploma ambao wamefanikiwa kujisajili wanisaidie hili jambo. Kwenye certificate tunaweka nini...na pale kwenye transcript tunaweka kitu gani....na hiyo GPA inatoka wapi?
Za sasa zina GPA
 
Hapa wewe ulivyoshindwa kujua hizo kozi ndio ndio mfano hai kujua huo mfumo unashindwa kujua kilichopo ndani ya kozi kwamaana masomo yakufundishia
PPM =Project planning Management
 
Wakuu Kwa wazoefu WA kuomba Kazi ajira portal ,....

Kipi Bora katika barua ya maombi ,kutumia kiswahili au kiingereza ....?

Tulikuwa tushazoe mfumo wetu WA oteas uliokuwa unatuambia kabisa tuandike barua Kwa mkono Tena ya kiswahili ...
Tumia lugha yeyote ile kati ya kiswahili au kingereza hakuna shida ila hakuna usahili kwa lugha ya kiswahili ni mwendo wa kula yai tuuu!
 
HII NIDA ishatumika,mara nyingi inatumika mara moja,utakuwa ulifungua akaunti ukasahu au kuna mtu kaitumia kufungua akaunt ajiraportal
Hapana hakuna anayeweza kutumia nida ya mwenzie utumishi hasa ajira portal! Hapo ni wazi alishafungua account na akaweka nida sasa anataka kufungua nyingine baada ya kusahau taarifa za mwanzo! Namshauri awapigie utumishi wampe taarifa zake maana awezi kufungua nyingine
 
Wakuu nikibofya personal details nikiandika nida yangu wananiandikia hivi nifanyeje
Wewe Kazanazo ulishafungua account ajira portal na umesahau taarifa zako hivyo wapigie utumishi watakupa taarifa zako uendelee na kuomba kazi! Fanya fasta
 
Mitihani yao inakauje mkuu ,kama mwalimu WA hesabu wanauliza maswali ya kawaida(kisiasa ,kiuchumi na kijamii) au Wana base kwenye somo kabisa topic zilizomo kwenye somo ...mfano mathematics unaweza kutana na maswali ya integration,set , differentiation, , logarithmic,quadratic equations,algebra...😂

Au uandae somo ufundishe n.k ...

Nchi ishakuwa ngumu tayari
Utaulizwa kulingana na kazi uliyo omba! Kama ni mwalimi wa hesabu utaulizwa mahesabu na ya kwanza ni ya kuandika inafanyika kwa compute “aptitude test” wana set muda mnaanza kwa pamoja nchi nzima …muda ukiisha basi hawana haja ya kukwambia pens down! Halafu kuna practical ambayo itahusu uwezo wako wa kufundisha wanafunzi na watu halafu baadae kuna ya ana kwa ana na panel ambayo itahusu uwezo wako wa kuelewa, maswali yatapima uwezo wako! Swali la kwanzo “tell us about your self” or your academic back ground! Kwenye oral swala kubaa ni confidence na uwezo wa kuzingatia muda na kusikiliza vyema basi!
Kila la kheri!
 
Wewe Kazanazo ulishafungua account ajira portal na umesahau taarifa zako hivyo wapigie utumishi watakupa taarifa zako uendelee na kuomba kazi! Fanya fasta
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako japo nilishafanikisha(kuna alienipa muongozo kama huu wako hapo juu)

Sema kuna shida nyingine nimesoma Bed guco(guidance and counseling) kila somo ninalo apply linaandika failed nifanyeje mkuu
 
Tumia lugha yeyote ile kati ya kiswahili au kingereza hakuna shida ila hakuna usahili kwa lugha ya kiswahili ni mwendo wa kula yai tuuu!
Ht mwalimu wa Kiswahili nae lazima ale mkando kwa yai tuu 😂
 
Barua andika kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili. Hii sio Muhimu Sana

Ila vitu ambavyo usije kuthubutu kusahau.
1. Kuweka Picha yako.
2. Kuandika anuani iyoelekezwa.
3. Barua yako ya maombi kusaini.
4. Vyeti vyako vyote kuwa certified.

Ukisahau kimoja kati ya hivyo hautaitwa interview.
Hy picha anaweka kwenye barua?
 
Wakuu Kwa wazoefu WA kuomba Kazi ajira portal ,....

Kipi Bora katika barua ya maombi ,kutumia kiswahili au kiingereza ....?

Tulikuwa tushazoe mfumo wetu WA oteas uliokuwa unatuambia kabisa tuandike barua Kwa mkono Tena ya kiswahili ...
Andika lugha yoyote mkuu
 
Back
Top Bottom