Kwa wanaoomba kazi kupitia mfumo wa ajiraportal, ili iwe na assurance ya kwanza ya kuwa shortlisted ukiachana na vigezo vingine, hakikisha umezingatia haya kwenye mfumo (akaunti yako)
1. Umeweka vyet vilivyopigwa mhuri kwa mwanasheria kwa maana ya vyeti vyote vya kitaaluma (4,6, chuo, transcript plus chet cha kuzaliwa ni lazima)
2. Uwe umeattach documents/attachments zote kulingana na level ya elim ulizopita" hapa unakuta mtu kasoma chuo ila hajaweka transcripts " my dear expect nothing
3. Hakikisha barua yako ya maombi inazingatia vitu viwili vikibwa kwanza iwe imesainiwa na wewe mwombaji wa nafasi hzo, pili hakikisha barua iwe directed kwenye anuani husika kama ulivoelekezwa" usikosee hata kdogo anuani kitakulamba[emoji23]
4. Hakikisha mihuri ulopiga kwenye vyeti ni official syo umekutana na wakili uchwara tu kaokota mhuri huko ukapiga" itakucost
5. Hakikisha umeweka chet cha kuzaliwa ni mhim , usipoweka huwez kuwa shortlisted
6. Kama umefanya duplication ya certificates unakuta mtu kaweka same Bachelor kama mara 3 kakosea tu katika ujazaji" fanya jihad za kuichomoa ila isikupe wasiwas kikubwa kama haikulimit kuapply unaweza kuwa shortlisted ila fanya namna ya kuiweka Sawa
7. Hakikisha umeweka passport size,
8. Hakikisha umejaza wadhamin wako watatu na ni vizuri wasiwe ndugu, unakuta mtu jna lake ni PAUL JOHN, ukija kucheki wadhamini wote tunaona kina JOHN tu[emoji23] kdogo inaweza kuleta shda japo so sana
9. Hakikisha umeweka CV yako" na usitumie cv ile inayokuwa generated from ajiraportal account, tumia cv ya kawaida za kila sku tunazotengeneza
10. Hakikisha kama Kuna shida ya majina labda nida na majina yako haviendaniii , au chet cha kuzaliwa pia Kuna shda na majna yako halisi hakikisha ume attach affidavit/kiapo pale kwenye other attachments Kuna hyo sehem.
Above all" mkabidhi Mungu kwenye kila ktu