Serikali yatangaza Ijumaa Oktoba 17, 2025 kuwa Sikukuu ya kitaifa ya kumuenzi Odinga

Serikali yatangaza Ijumaa Oktoba 17, 2025 kuwa Sikukuu ya kitaifa ya kumuenzi Odinga

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Serikali ya Kenya imetangaza Ijumaa, Oktoba 17, 2025 kuwa sikukuu ya umma kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga, aliyefariki dunia Oktoba 15, 2025 akipatiwa matibabu nchini India. Katika tangazo maalumu la gazeti la Serikali Na. 15007 iliyochapishwa mapema Oktoba 16, 2025, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, Kipchumba Murkomen, ametangaza tamko hilo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Likizo ya Umma (Sura ya 110).

Mazishi ya kitaifa yatafanyika katika uwanja wa Nyayo siku ya Ijumaa. Bendera kote nchini Kenya zimekuwa zikipepea nusu mlingoti tangu Jumatano baada ya habari za kufariki kwa Odinga zilipothibitishwa, huku vitabu vya rambirambi vikifunguliwa katika ofisi za Serikali, balozi na ofisi za chama cha ODM. Raila Odinga (80), aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya mwaka 2008 hadi 2013 chini ya Serikali ya Muungano kufuatia uchaguzi wa urais wa 2007 uliokumbwa na utata. Odinga, pia alikuwa mgombea urais mara tano na kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM).
 
Bendela zinapepea nusu mlingoti kwa kuwa aliwahi kuwa waziri mkuu,tofauti na hapo angezikwa na familia pamoja na chama chake pekee pasipo serikali kuhusika. Ivi odinga ndiye aliyekuwa anapigania bangi ihalalishwe nchini kenya
 
Back
Top Bottom