milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.
Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salaam leo September 30,2024 wakati akizindua kitabu cha Sokoine (Maisha na Uongozi wake).
"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi, kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mumba na tumetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma kwahiyo hili tunalifanyia kazi" — Rais Samia.
Chanzo; Millard Ayo
Pre GE2025 - Ujumbe Muhimu kwa Rais Samia Kutoka Majimbo ya Uchaguzi Chunya na Lupa Mkoa wa Mbeya.
Ninatoa wito kwa Rais Samia na serikali yake kuchukua hatua za haraka kuhusu hali ya maendeleo katika Jimbo la Chunya na Lupa, Mkoa wa Mbeya, kulingana na ilani ya CCM ya 2020-2025. Ni jambo la kusikitisha kwamba, licha ya kuwa na madiwani wote na wabunge wawili kutoka CCM, hakuna miradi ya...