Serikali yatenga Shilingi Bilioni 34 kujenga Makumbusho ya Marais Dodoma

 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.

Hii habari ipo kwenye ilani ya CCM 2020-2025?
Au ni kipaumbele cha serikali?
 
mh! kuna muda mnatuchanganya sana!..
mnaendaga huko nje kufata mikopo ili mje mfanye mambo yenye kuleta tija maana nchi yetu bado ipo ktk ombwe la umasikini,hatujafika hizo hatua za kuweka makumbusho ya marais kwa gharama za mabillion ya pesa!.
ikiwa bado tunashida lukuki zakutatua kwanini pesa hizo zisipelekwe kwenye miradi yenye tija kwa jamii..?
tukianza kuwasema hovyo mitandaoni mtuteke,mtunyanyase kwa kutubinya kendelelo!.

WTF!
 
Kwanza swali la msingi la kujiuliza, hivi hiyo proposal imepita Bungeni??

Au ndiyo kama kawaida yake Mama, kugawa pesa za walipa Kodi wa nchi hii kama njugu?🙄

Kama anavyofanya wakati huu za kulipa magoli ya Simba na Yanga, milioni 5 Kwa pesa zetu walipa Kodi!😭
 
Kwanza swali la msingi la kujiuliza, hivi hiyo proposal imepita Bungeni??

Au ndiyo kama kawaida yake Mama, kugawa pesa za walipa Kodi wa nchi hii kama njugu!🙄
Hii nchi ni ngumu kwa kweli👋
 
Mchungaji ameona mbali na huu ni ukweli 100%
 
Hakika hii nchi inakokwenda ni kubaya sana!

Kama wakubwa wanaamua kufuja Kwa hali ya juu kiasi hicho, pesa zetu za walipa Kodi, basi ni hatari sana!😭
 
34B kujenga makumbusho safi sana lakini je, ni kipaumbele chetu kwasasa?
Mahitaji tunayo mengi tena sana ni muhimu kuanza na ya lazima kisha yafuate ya muhimu!
 

Hawa viongozi ni bure wenzao maktaba za maraisi zinatokana na michango na sio pesa za serikali
 
Vimiradi visivyo na maana ndio vinapewa pesa.

Makumbusho ya Taifa ipo Kwa nini hao Marais kumbukumbu zao zisitunzwe kule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…