tatizo lipi? matatizo yaliyopita kwa taarifa yako most of the yalipatiwa suluhu kwa njia hii hii ya mgomo. Kwa hili la sasa tatizo halijawekwa bayana so suluhu itapatikanaje?
kulindana? inaonyesha wewe ndio uyelijua sana hili ni vyema ungesema tu ukweli unamlinda nani.
Wewe ulikuwepo UDSM hiyo 1990s, acha kukomalia mambo bila kujua kiini. Haya kumbusha kilichowakuta kina Mbatia na uwataje hao wenzie ni kina nani.
kuitana majina sio nia njema, hao unaowaambia waache UNAZI unafikiri wanafurajia kuitwa hivyo? then unawataka waseme, waseme nini ilhali wewe unajua kila kitu na unachokijua wewe ndio sahihi? usiwafanye watu wajinga hapa, kukaa kimya sio kushindwa hoja, sometimes ni kuepuka kupewa jina.
Mambo ya kufichana yamepitwa na wakati mtu kama ni Mnazi nitamuita mnazi mpaka kieleweke.Ni kama walivyo kwa mafisadi kama ni fisadi ni fisadi hakuna tasifida hapa.
Matatizo gani wewe unayosema yamepatiwa ufumbuzi??? MAMA acha kuhadaa watu.
statistics toka mwaka 2000 udsm wameshagoma na kusimamishwa zaidi ya mara NNE na wamegoma mfululuzo zaidi ya miaka 3 kutokea leo na ukirudi nyuma.Sasa wewe unasema yamepatiwa ufumbuzi yepi hayo??
endelea na makala hii kutoka majira
Habari za Tanzania Ijumaa Apr 25, 2008
Imetolewa mara ya mwisho: 25.04.2008 0127 EAT
Tatizo Chuo Kikuu ni Mukandala - TAHLISO
Habari Zinazoshabihiana
Chuo Kikuu sasa wamwangukia Kikwete 03.05.2007 [Soma]
Uongozi Chuo Kikuu waijibu DARUSO 09.05.2007 [Soma]
Sitta ateua wajumbe Baraza la Mitihani 17.10.2007 [Soma]
*Wampa siku nne kurejesha wanafunzi waliofukuzwa
* Wengine 62 watimuliwa
Na Gladness Mboma
UMOJA wa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) umemjia juu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala kwa madai kuwa ndiye kiini cha kupotea amani chuoni hapo.
Wanafunzi hao pia wamemtaka Prof. Mukandala kuhakikisha anawarejesha chuoni wanafunzo wote waliofukuzwa ifikapo Aprili 27 mwaka huu.
Mbali na hilo, TAHLISO imemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe afute kauli yake ya kuwafutia udahili na kuwanyima mikopo wanafunzi wanaotuhumiwa kuhusika na mgomo sambamba na kutaka wasidahiliwe katika chuo chochote nchini.
Wanafunzi hao walidai kauli ya waziri huyo ni ya kibabe, kiburi na ukatili dhidi ya vijana wa nchi hii kwani kwa kiasi kikubwa mgogoro ulioibuka chuoni hapo umechangiwa na uongozi wa chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Chitage Edwin, alisema kuwa taasisi hiyo inathamini zaidi amani na haki kuliko kile alichoita 'umamluki' wa Prof. Mukandala.
"Uchunguzi wa TAHLISO umebaini kuwa Prof. Mukandala ndio chimbuko la kuvunjika kwa amani mara kwa mara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tunamtaka Mukandala awarejeshe wanafunzi wote ifikapo Aprili 27. TAHLISO inathamini zaidi amani amani na haki kuliko umamluki wa Profesa Mukandala," alisema na kuendelea kuwa;
"Tunalaani kitendo cha utawala wa chuo kuingilia mchakato wa uchaguzi. Kitendo cha uongozi wa chuo kuandika barua kusitisha uchaguzi na kubandika katika kuta na mbao za matangazo pasipokujadiliana na tume ya uchaguzi ni kinyume cha kanuni za uchaguzi chuoni hapo.
Kwa utafiti tuliofanya kulikuwa hakuna hali yoyote ya hatari kwa kipindi hicho, hivyo chuo hakikuwa na sababu yoyote ya kuingilia utaratibu tena bila hata kuvihusisha vyombo mahususi kama Tume ya uchaguzi,"alisisitiza Bw. Edwin
Bw. Edwin pia aliwataka wakuu wa vyuo wenye tabia hiyo, kuwaacha vijana wajifunze utamaduni wa demokrasia kwa kufanya chaguzi huru na haki pasipokushinikizwa na kutishwa.
Pia amewakumbusha wakuu wote wa vyuo kuongoza vyuo vikuu kitaalamu na waepuke umamluki au upiga debe wa propaganda chafu za kisiasa na kwamba ni lazima wakumbuke wakati wote kuwa chuo kikuu si jimbo la uchaguzi.
"Tunautaka utawala kusitisha mara moja hujuma kwa mwanafunzi kutoka Uganda aliyekuwa mgombea wa urais, uwaachie wao ndio wataamua kupitia sanduku la kura kama anawafaa au hawafai
Nchi hii haikujengwa katika misingi ya ubaguzi wa aina yoyote ile,tunauonya uongozi wa chuo wasiwe vinara wa kupanda mbegu ya ubaguzi. Kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Wanafunzi hakuna kipengele kinachomzuia raia kutoka nje ya Tanzania kuwa kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi,"alisema Bw. Edwin
Bw. Edwin alisema kuwa inashangaza kuona kila kukicha Bw. Odongo Odwa wa Uganda anahujumiwa. Katika vyuo mbalimbali duniani imetokea viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka nchi tofauti na kwamba inashangaza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumkana mwanafunzi ambaye wao walimdahili na kuhoji shutuma hizo kuibuliwa wakati wa uchaguzi.
Pia Bw. Edwin aliushangaa uongozi wa chuo kumsimamisha masomo kwa siku 30 badala ya kumpa ruhusa yenye muda wa kutosha kuwasilisha vyeti hivyo.
Alisema kuwa TAHLISO inaamini kuwa jamii bora hujengwa kwa maridhiano na sio kwa nguvu za polisi, mahakama na vitisho na kwamba mtindo wa kuwatisha, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha vijana wasomi utaipeleka nchi pabaya.
"Tunamshauri Bw. Rwambow (Jamal, Kamanda wa Polisi Kinondoni ) kuwa ni vema angetumia nguvu hizo kuwakamata mafisadi na kuwapeleka mahakamani badala ya kuwaonea vijana hawa wahanga wa umaskini na utawala mbya wa nchi hii
Naye Reuben Kagaruki anaripoti kuwa wanafunzi 62 wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamefukuzwa masomo na wengine 415 wanachunguzwa kufuatia vurugu zilizoibuka chuoni hapo tangu Jumatatu, wiki hii na kusitisha shughuli za masomo.
Uamuzi huo ulitangazwa ana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mukandala, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zilizochukuwa na uongozi kufuatia vurugu zilitokea chuoni.
Alisema wanafunzi waliofukuzwa masomo wataruhusiwa kuomba upya udahili iwapo watashinda kesi zao zinazowakabili mahakamani.
Alitaja kundi la kwanza la wanafunzi waliofukuzwa kuwa ni 15 ambao walihusika na vurugu zilizotokea chuoni hapo na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja.
Profesa Mukandala alitaja kundi jingine la wanafunzi waliofukuzwa kuwa ni 38 ambao walihusika kwenye vurugu za Jumatatu ambao walifikishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Alisema makundi hayo mawili ya wanafunzi wataruhusiwa kuomba upya udahili pindi wakisha kesi zao.
Wanafunzi hao 38 walisomesha shitaka kula njama kufanya vurugu lakini walikana shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bw. Said Msuya, shitaka ambalo wote walilikana.
Wanafunzi wengine wanne wamefutiwa udahili kabisa baada ya kubainika waliingia darasani na kumfanyia fujo mhadhiri. Wanafunzi hao ni Bw. Stephano Owawa, Bw. David Silinde, Bw. Ally Selleman na Bw. Ally Salum.
Alisema wanafunzi watano waliokamatwa wakivuta bangi nao wamefutiwa udahili na wataruhusiwa kuomba kudahiliwa upya iwapo watashinda kesi zao. Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Godson Emmanuel, Adili Mwang'onda, Batenga Jimson, Joshua Mwanjwango na Soka Eliphance.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Profesa Mukandala kutoa uamuzi wa chuo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bw. Deo Daud, alisema hatua hiyo ni ya kibabe kwani uongozi wa chuo hicho ulikuwa na nafasi ya kukaa nao na kuzungumza.