Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Nziku,

Yaani wanajichanganya kweli kwenye suala la wanafunzi waliokamatwa na hiyo ya kifo cha mama mja mzito. Kuna taarifa kuwa wanafunzi wawili wa sayansi ya jamii hawajulikani walipo.

Inawezekana wameua zaidi ya mtu mmoja hapa!

Inawezekana Mkuu, ila habari nilizozisikia mimi ni kwamba wanafunzi 39 walikamatwa na 38 wamefikishwa mahakamani leo. ila hawakusema huyo wa 39 yupo wapi.
 
Sasa Prof Maghembe anataka kuingia katika Kundi la Mafisadi, maana kuwanyima watu haki yao ya Msingi tena wanafunzi tunao wategemea waje kuchukua au kuongoza taifa in future ni kitu cha kusikitisha na kisicho ingia akili kwa mtu mwenye akili kama wewe, labda ukiwa umepata Denge lua. Please acha kusikiliza taarifa Potofu za Prof Mkandara.
Plse Maghembe Raise up to you Status Mzee.
Kwa Mfano wanafunzi hawapatiwi maji kisa Pump mbovu kumbe ni creation ya mradi wa watu ili wa-supply maji. Ni jambo zuri, mbona shida zingine tunajitakia? au ndio njia za kuongeza ajira na Mabilionea wa Ari mpya?

Wamezoea kuwa watanzania watakuwa kimya kama kawaida yao na sasa wanafikia hatua ya kuua watu bila haya hata kidogo.
 
Tena kuna habari nyingine kuwa wanafunzi 38 waliokamatwa jana wamefikishwa mahakama ya kisutu, wanakabiliwa na kesi 3 tofauti. wengine wamepata dhamana, wengine wamepelekwa mahabusu

Mpitanjia,

fuatilia source zako vizuri. Taarifa zinasema kuwa ni wanafunzi 39 walikamatwa na sio 38. Huyo mmoja bado hajulikani aliko. Isije kuwa Kikwete amejenga jela za siri kama zile za Sadam kule Iraq.
 
Inawezekana Mkuu, ila habari nilizozisikia mimi ni kwamba wanafunzi 39 walikamatwa na 38 wamefikishwa mahakamani leo. ila hawakusema huyo wa 39 yupo wapi.

Nziku ni kweli kuwa hawajasema bado huyo wa 39 yuko wapi. Nina wasiwasi kuwa Kikwete amejenga jela za siri kama zile za Sadam Hussein kule Iraq
 
Serikali hii ya kifisadi inasikitisha sana. Wakati huwa wepesi mno kuchukua uamuzi wa kuwafukuza wanafunzi lakini mafisadi wa bilioni 288 za BoT, Kiwira Coal Mining, Richmond, Rada wote bado hawajaguswa wala hakuna dalili kama wataguswa. Serikali imeoza tunataka ijiuzulu ili kufanyike uchaguzi mpya hakuna haja ya kusubiri mpaka mwaka 2010. Wananchi hatuna imani na serikali iliyopo madarakani.
 
inasikitisha sana aisee, kama serikali ingekuwa kali namna hii kwa mafisadi, tungekuwa mbali sana.yani washafunguliwa na kesi!!! ila inawezekana wakawa wanachokonoa kitu kitakachowashinda, hivi itakuwaje wanafunzi waliobaki nao wakigoma na kuanzisha sekeseke la kuwatetea wenzao!!?? nao wote watafukuzwa!!?? kwa sababu its a likely outcome, au hawakufkiria kitu kama hicho!
 
Habari hii imewekwa katika kina chake mahali ambapo "we bring you the news first"... zote mbili za kufikishwa mahakamani na wanafunzi kufukuzwa.
 
inasikitisha sana aisee, kama serikali ingekuwa kali namna hii kwa mafisadi, tungekuwa mbali sana.yani washafunguliwa na kesi!!! ila inawezekana wakawa wanachokonoa kitu kitakachowashinda, hivi itakuwaje wanafunzi waliobaki nao wakigoma na kuanzisha sekeseke la kuwatetea wenzao!!?? nao wote watafukuzwa!!?? kwa sababu its a likely outcome, au hawakufkiria kitu kama hicho!

Kama walifikia hatua ya kuleta FFU na kupiga watu bila mpangilio hadi kuna habari kuwa wameua mama mjamzito ambaye ni mwanafunzi hapo chuoni (ingawa mkandara anadai kuwa ni mimba tu ndiyo imetoka) unategemea kuwa wanafikiri hawa?!
 
Mpitanjia,

fuatilia source zako vizuri. Taarifa zinasema kuwa ni wanafunzi 39 walikamatwa na sio 38. Huyo mmoja bado hajulikani aliko. Isije kuwa Kikwete amejenga jela za siri kama zile za Sadam kule Iraq.

Nimeyaona majina 38 ya wanafunzi waliofikishwa mahakamani kisutu, huyo wa 39 kwa kweli hata mimi ananishangaza lakini hawataweza kukataa kwa sababu hata maghembe anasema walikamatwa 39
 
namna hii, hatutafika mbali, THE SILENT MAJORITY WILL SOON TAKE ACTION!! its a ticking bomb, its just a matter of time!!
 
Wanafunzi wa UDSM simamieni haki yenu bila woga. Na labda hamjui tu, lakini nguvu yenu na ushawishi wenu katika jamii ni mkubwa ajabu. Wanafunzi wa vyuo vikuu huko Indonesia waliweza kuuondoa madarakani utawala wa kifisadi miaka ya 80/90.
 
Aisee, thats true, wasimame kidete kuwatetea wenzao.wasipo take action watakua wame-bow down kwa utawala wa fear na intimidation wakati hizi si zama za hayo mambo.wanafunzi mkikaa kimya next time mtashindwa kudai haki zenu za msingi kwa kuogopa kufukuzwa, this is the time to react agaisnt such old type ruling system of fear and intimidation.GET UP, STAND UP, STAND UP FOR...............
 
Wameingilia uchaguzi, wamefukuza viongozi, wamepiga mabomu wanafunzi bila sababu yoyote, kuna habari kuwa wameua mwanafunzi mjamzito, wamekamata wanafunzi usiku wa manane, hii ni hitimisho la udikiteta, ufisadi na "uuaji" wa Mkandara (ambaye ni mshauri wa Kikwete wa masuala ya siasa).

nakubaliana na hoja zote za CCM kuingilia mambo UDSM,lakini nadhani inabidi tufikiri kwa bidii sana ili tuone mambo tukiwa ndani kiini cha jambolenyewe

Zamani Chuo kikuu kilikuwa kimoja na chenye hadhi inayostahili na ndiyo maana wakati mwingi mwalimu alitumia kwenda Mlimani kupata changamoto (catalyst)na Sai (Challenge) kwa fikra zake alizozisimamia.

Lakini sasa Chuo chetu hiki kipendwa kina mambo mengi ya ajabu huwezi kufikiri kupatikana kwenye taasisi nyeti ya elimu kama ile.kwanza kuna wanafunzi walioingia pale kwa kununua mitihani,pia wapo wengine wanaotumia vyeti vya kughushi kabisa

lakini wapo wakurufunzi wasio na uwezo wa kufundisha vyuo vikuu na wapo pia wanakwezwa madaraja kwa vigezo vya ukabila na hata wakati mwingine udini

wapo wanafunzi wanaosoma pale bila kuwa na haki wala sifa ya kuwa mlimani lakini kutokana na udhaifu wa usimamizi mbovu wa management ya chuo hayo yote yanawezekana.

wapo pia vibaraka sugu wa watawala wetu na CCM,ambao wanaona kuwa ndani ya CCM eti kuna "vihiyo" wengi hivyo kusoma kwao kutawasaidia kupanda ngazi ndani ya System na hatimaye kuja kujichotea vijisenti vya walala hoi wa nchi hii huko mbele ya safari.

ukichanganya na wale wanaopata marks au digrii kwa kufanya ngono na wahadhiri unakutana na kundi kubwa la wasomi wasio na mwelekeo. Hao hao wanaogoma leo kesho wakiambiwa wanakwenda kuonana na Kikwete Diamond Jubilee watagombania fulana kama simba wanaogawana Swala!
 
Every year au every other year haya mambo yanatokea...why? Ndivyo Tulivyo au...? Maana tokea niko shule ya msingi yanatokea...ina maana hawajajua namna ya kutatua matatizo yao au ni Ndivyo Tulivyo and there's nothing we can do about it?
 
Nakubaliana nawe katika hili mkuu

Lakini mkuu, hii si sababu ya kuhalalisha kuingilia uchaguzi, kufukuza wanaopigania haki, kuleta FFU na kupiga watu bila sababu, kutumia mabavu kwenye mambo ya wanafunzi, na kufikia hatua ya kufukuza wanafunzi haraka hivi wakati hadi leo Dowans wanalipwa mabilioni.

wapo wanafunzi wanaosoma pale bila kuwa na haki wala sifa ya kuwa mlimani lakini kutokana na udhaifu wa usimamizi mbovu wa management ya chuo hayo yote yanawezekana.

wapo pia vibaraka sugu wa watawala wetu na CCM,ambao wanaona kuwa ndani ya CCM eti kuna "vihiyo" wengi hivyo kusoma kwao kutawasaidia kupanda ngazi ndani ya System na hatimaye kuja kujichotea vijisenti vya walala hoi wa nchi hii huko mbele ya safari.

Haya pia bado si sababu ya udikiteta na ufisadi uliofanywa na Mkandara kwenye hii issue ya wanafunzi.

ukichanganya na wale wanaopata marks au digrii kwa kufanya ngono na wahadhiri unakutana na kundi kubwa la wasomi wasio na mwelekeo. Hao hao wanaogoma leo kesho wakiambiwa wanakwenda kuonana na Kikwete Diamond Jubilee watagombania fulana kama simba wanaogawana Swala!

Si kweli kwamba haya yanatokea kila siku. Mambo ya ngono yapo hata Harvard na sio sababu tu ya kudiscrediti wanafunzi nakisha kuwapiga mabomu.
 
Sasa Prof Maghembe anataka kuingia katika Kundi la Mafisadi, maana kuwanyima watu haki yao ya Msingi tena wanafunzi tunao wategemea waje kuchukua au kuongoza taifa in future ni kitu cha kusikitisha na kisicho ingia akili kwa mtu mwenye akili kama wewe, labda ukiwa umepata Denge lua. Please acha kusikiliza taarifa Potofu za Prof Mkandara.
Plse Maghembe Raise up to you Status Mzee.
Kwa Mfano wanafunzi hawapatiwi maji kisa Pump mbovu kumbe ni creation ya mradi wa watu ili wa-supply maji. Ni jambo zuri, mbona shida zingine tunajitakia? au ndio njia za kuongeza ajira na Mabilionea wa Ari mpya?

No doubt about Maghembe kuwa Fisadi maana ana save kwenye serikali ya kifisadi sasa hata Wabunge hawasemi kwamba Rais wa CCM ni muadilifu .So unategemea nini ?
 
Every year au every other year haya mambo yanatokea...why? Ndivyo Tulivyo au...? Maana tokea niko shule ya msingi yanatokea...ina maana hawajajua namna ya kutatua matatizo yao au ni Ndivyo Tulivyo and there's nothing we can do about it?

Ngabu hapa inabidi kweli usemi wako utumike tena.

Yaani huuyu Mkandara na wenzake hapo wamefanya kitu ambacho wanajua kuwa wanafunzi hawatakubali hata kidogo na inakuwa kama vile wamefanya makusudi au kwenye usemi wako - ndivyo walivyo.

Utashangaa kusikia kuwa huyu Mkandara ni rafiki ya karibu wa Kikwete na mshauri wake wa kisiasa. No wonder nchi inakwenda kuzimu.

Yaani wanakimbilia kupiga wanafunzi, kuwafukuza chuo, na kuwaweka ndani wakati richmonduli bado wanalipwa mabilioni ya pesa na kina Chenge na Karamagi wakidunda mtaani kama hawana akili nzuri vile.
 
Back
Top Bottom