Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Mwafrika wa kike, ingawa wengine hapa JF wanakuona kama mwenye msimamo mkali lakini nimekukubali sana, what you say makes sense.
Hoja hapa si kuwalaumu wanafunzi eti ni vihiyo na digri za vichupi, etc. Kwani hao wanafunzi ni product ya nani au nini? Ya education system yetu, walimu wabovu since vidudu, kukosekana kwa vitendea kazi, walimu below standard, mitihani inayo-leak kila kukicha, etc! Kwa hiyo kuleta hiyo argument will not fly. Also they are entitled to choose leaders that they want.
Kumtetea Mukandala siwezi kwa sababu ni lazima atumie hekima. Wanafunzi duniani kote wanajulikana kuwa radicals, na dawa si kuwapiga na kuwafunga jela. That's unacceptable! Na kama hii issue ya mama mjamzito ni kweli, the government has to answer.

Naomba niwakumbushe tunapenda kusema "huwezi kushindana na serikali" lakini hii ni kutoka enzi za ujamaa na one party system, hivi sasa katika democratic system, the government is the people. What we giveth, we taketh. Let us prove this to CCM and taketh away their power to govern because clearly they have failed!
 
Fair iko wapi......kuwafukuza hata wasiohusika hiyo ndio fair..........kutumia nguvu kwa watu walio cafeteria (mwanafunzi mjamzito) hii ndio fair.......kuingilia uchaguzi wa wanafunzi hiyo ndio fair........hivi jamani tuko ktk era gani........hizi speculation za Mars kugonga Earth tutaziacha lini

........Yes hata ningekwa mimi tatizo lingekuwepo.......lakini hiyo ndio njia fair ya kutatua tatizo??......kupiga watu!!!!

......Wanafunzi wanaoleta fujo (kuvunja milango na vioo) si wanajulikana.......kwa nini hao wasichukuliwe hatua.....hii mambo ya ku-generalise mambo............ndio Upumbavu wa Maghembe.

"Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili"......na huu ndio upumbavu alioufanya Maghembe

Ogah,

ni kweli kabisa kuwa kama wanafunzi wamefanya fujo basi vyombo vya usalama ambavyo vimejaa hapo chuoni vingejua cha kufanya. Tatizo ni kuwa wanatumia zile fujo za mara ya mwisho mwezi wa pili nadhani ambapo wanafunzi walimfuata Mkandara nyumbani kwa vile kulikuwa na ukosefu mkubwa wa maji chuoni kuadhibu wanafunzi leo hii ambako wanafunzi wamefanya maandamano ya amani kabisa kudai haki zao.
 
Lakini Nyani kuna kauli ambazo angetoa ingawa ni za kisiasa , lakini zingekuwa na Positive effect, one kumuita Prof Mkandara na watu wake, pili kuongea na Viongozi wa Wanafunzi, tatu kupata taarifa toka kwa Usalama wa taifa na hata facts zingine angezipata toka kwa indepent side of the issue, maana hata magazeti wameandika, mfano suala la Maji kule mabibo kuwa Mradi wa Mtu kwa kusingizia Pump mbovu, suala la Lift kama ni ya kutengenezwa au kubadilishwa, na muda muaafaka wa kubadili ni upi.
Then basing on those ciorcumstance angewasiliana na Pinda na ikiwezekana Raisi, kabla ya kutoa hiyo taarifa ya serekali, kama ni kuunda tume ya kufuatilia madai ya pande zote, hiyo inge-create a cooling off period for both sides , wakati serekali inaufuatilia kwa undani zaidi huo mgogoro.na Muafaka wake uwe vipi.
Leo hii tusingekuwa tuna zungumzia Chuo kufungwa, bali situation ya kufuatilia matatizo ya hizo pande mbili.

Kweli kabisa August,

Uongozi wa chuo waliambiwa zamani kabisa na hata hapa JF tulitoa wito kwa fisadi, dikiteta na muuaji Mkandara kuwa wasiingilie huo uchaguzi wa wanafunzi ila wao wakaleta ubabe.

Katika hili hata Maghembe alijua vyema kabisa kuwa angekutana na wanafunzi na kuwaruhusu kufanya chaguzi zao kwa amani na haki zote.

Sasa hivi tuna lalamika tanzania kielimu tupo nyuma vis a vis majirani zetu, lakini bado tunaona majibu ya matatizo ya chuo ni kufunga chuo? Kwa mtindo huo tutafika kweli? Kuna Cost ya kifedha, adha za manyanyaso ya hao wanafunzi, hasa wa kike, kifedha etc etc

Unajua mtu ukiwa Msomi ulio bobea kama Prof Magembe analysis yako na maamuzi yako yanatakiwa yasiwe ya kukurupuka na ya muda mfupi, na madhara makubwa.na Hizi ni opportunity chache ambapo Msomi anaweza kuonyesha alivyo tofauti na mwana siasa asiye msomi au asiye na busara.

Hiyo kwenye font kubwa inajitosheleza kabisa mkuu
 
Mwafrika wa kike, ingawa wengine hapa JF wanakuona kama mwenye msimamo mkali lakini nimekukubali sana, what you say makes sense.
Hoja hapa si kuwalaumu wanafunzi eti ni vihiyo na digri za vichupi, etc. Kwani hao wanafunzi ni product ya nani au nini? Ya education system yetu, walimu wabovu since vidudu, kukosekana kwa vitendea kazi, walimu below standard, mitihani inayo-leak kila kukicha, etc! Kwa hiyo kuleta hiyo argument will not fly. Also they are entitled to choose leaders that they want.
Kumtetea Mukandala siwezi kwa sababu ni lazima atumie hekima. Wanafunzi duniani kote wanajulikana kuwa radicals, na dawa si kuwapiga na kuwafunga jela. That's unacceptable! Na kama hii issue ya mama mjamzito ni kweli, the government has to answer.

Naomba niwakumbushe tunapenda kusema "huwezi kushindana na serikali" lakini hii ni kutoka enzi za ujamaa na one party system, hivi sasa katika democratic system, the government is the people. What we giveth, we taketh. Let us prove this to CCM and taketh away their power to govern because clearly they have failed!

Kwi kwi kwi,

Susuviri katika hili ni kweli lazima niwe na msimamo mkali maana ni aibu kabisa kuleta FFU na kupiga mama mjamzito kwa sababu ambazo hazina msingi kabisa.

Huyu fisadi, dikiteta na muuaji Mkandara anachukua uongozi wa chuo back to the days za Msekwa ambapo chuo kiligeuzwa kama taasisi ya chama.

Mkandara inabidi ajiuzulu kwa yaliyotokea mlimani.
 
wakienda uholazi si ndio basi kabisa
prof wakati wa mapumuziko anajisogeza pembeni analikamua jani.

tukirudi tz
uzinzi
hao maprof na mawaziri mbona ma magari yao hua hayaishi pale Ohio au nawo tuwavizie tukiwakamata tuwafukuze kazi na tuwapeleke rumende

maadili
mbona hao ma prof hua wanakata ulabu hadi wanajikojolea.

Wewe Mkamap kwi kwi kwi,

Yaani nina huzuni lakini hili imebidi nicheke tu. Kukata majani na kwenda ohio sio kidogo!
 
Nyani, alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ya Juu miongoni mwa mambo ya kwanza ambayo angetakiwa kushughulikia ni suala la Mlimani. Ni rahisi kutumia nguvu kuliko kutumia akili!

Unajua wanafunzi wameshazoeshwa kwamba matatizo yao hayawezi kutatuliwa hadi wagome. Na ni kweli mara nyingi wakigoma hupata walichokuwa wakikitaka. So, it is the question of attitudes. Ndio yale yale tunayoongelea hapa kila siku: respect to the rule of law na ustaarabu. Ongeza na cha tatu sasa: ustahimilivu. Jamii yetu imekuwa jamii isiyo na ustahimilivu. Hakuna patience kabisa. Wanafunzi wetu hawawezi kusibiri hata kidogo.

Na kuna udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa wanafunzi. Kuna faslafa ya kijinga kwamba ukiwa kiongozi wa wanafunzi unafuata wanachosema wanafunzi. Hii ni weakness kubwa na sio maana ya uongozi. Ukiwa kiongozi unakuwa na taarifa nyingi zaidi kuliko unaowaongoza kwa hiyo lazima uonyeshe njia. Sitaki kujitolea mfano lakini inabidi. Mwaka 1998 Septemba mara baada ya chuo kufunguliwa niliwahi kugombana na wanafunzi vibaya sana kwa kuwa nilikataa kuongoza mgomo. Nilikuwa nimetoka serikalini kufuatilia mambo ya pesa za chakula na malazi. Baada ya malumbano mengi sana na waziri wa sayansi na katibu wake mkuu kwa muda wa siku nzima, wakakubali kwamba wangekopa pesa NBC. Palepale wakaongea na mkurugenzi wa NBC wakakubaliana kuwa ni sawa. Tatizo likaja kwamba hela zisingepatikana siku hiyohiyo hadi angalau siku tatu zipite ili wafanye clearance na ingebidi a-deploy wafanyakazi kwa kuwa ilikuwa inaingia weekend. Mimi sikuona shida kusubiri siku tatu au hata nne. Niliporudi chuoni nikawapa wanafunzi taarifa wakiwa Nkrumah. Wakagoma, wakaniambie lazima wapate hela yao siku hiyohiyo. Kumbuka hiyo ilikuwa saa 10 jioni na kesho yake ilikuwa ni Jumamosi. Mimi nikakataa, nikawaambia sipo tayari kuongoza mgomo kwa sababu hatuwezi kuvumilia siku tatu wakati kuna watanzania wanashinda njaa kila siku. Nikawaambia wakati sisi tukisema hatuwezi kusubiri siku tatu, kuna watanzania walikuwa wamekufa na njaa kule Gairo. Nikawaambia wanafunzi wenzangu kuwa watanzania wangetudharau kwa kushindwa kuvumilia siku tatu tena tukisubiri utaratibu wa kawaida wa kibenki. Tukalumbana sana na mwisho nikwaambia kama mnaona ni lazima tuandame twende wizarani saa hiyohiyo, basi sikuwa tayari kuongoza huo mgomo na kwamba ningejiuzulu ili wachague kiongozi mwingine. Baada ya hapo wanafunzi wakapoa, wakatawanyika wakabaki wachache kama 20. Nikawaambia wanafunzi walio wengi wameshanielewa. Ilipofika Jumanne wanafunzi wakapapata pesa zao na mambo yakaendelea kama mdundo. Ndio walinidharau sana siku hiyo Nkrumah na kuniona mimi ni traitor, lakini wengi walinishukuru baada ya siku tatu baada ya kutulia na ku-reflect.

Why all this story: Uongozi ni kuonyesha njia na wakati mwingine kuchukua maamuzi ambayo ni unpopular to your constituency. Viongozi wengi wa wanafunzi hawataki kuchukua maamuzi unpopular. Wanataka kushangiliwa na kuonekana ni hero sasa hivi. Wangekuwa wanaweza kuthubutu kuwaambia wenzao ukweli wa mambo migomo mingi ingeepukika. Nilijifunza katika uongozi wangu pale mlimani kuwa ukiwa na kiongozi imara wa wanafunzi unaweza kuepuka migomo ya kusababisha chuo kifungwe. Kiongozi wa wanafunzi lazima aweze kuona mabaya na mazuri ya pande zote: wanafunzi wenzake na utawala. Utawala wakikosoa unawazodoa, wanafunzi wenzako mki-bore pia msisite kujizodoa.

Kwa mfano, katika hili viongozi wa wanafunzi wasingekubali kuingia mkenge wa kuwatetea wenzao walioenda kuvunja majumba ya wafanyakazi. Ambacho wengefanya ni kuwawekea mawakili wazuri mahakamani lakini sio kujaribu kuzuia sheria isichukue mkondo wake wakati criminal offence imefanyika. Ifike mahala wanafunzi wetu waache kujiona wapo juu ya sheria. Narudia tena, tunataka kujenga taifa la watu ambao wanaheshimu sheria kuanzia mdogo hadi mkubwa, mwanamke kwa mwanaume, mwalimu kwa mwanafunzi.

Mwisho, iifike mahala viongozi wa wanafunzi waache kujipima umaarufu wao kwa kuendesha migomo. Ifike mahala sasa wajipime uthabiti wa uongozi wao kwa kuepusha migomo katika kipindi chote cha uongozi wao. This kind of principle helped me very much na hatukufunga chuo muda wote nilipokuwa kiongozi na sikupoteza support ya constituency yangu mpaka naondoka madarakani.
 
Kama wizara iliyofikia uamuzi wa kufukuza wanafunzi iko chini ya prof.kuna haja ya kuangalia upya wana taaluma wetu,wanafikia maamuzi kama wanasiasa washangiliaji na si kama wanataaluma walio kwenye siasa......Prof.Kachemsha
 
Kitila,

Haya unayosema ni kweli na ninaamini kina mtatiro na wenzao wanasoma hapa. Migomo sio lazima itumike hata kwenye mambo ambayo yanaweza kuwa solved kwa mawasiliano mazuri. Kama nimeleewa story yako, angalau wewe serikali ilikuheshimu na kuahidi kukopa pesa toka NBC. Katika hii case sioni kama uongozi wa chuo ulikuwa na nia ya kupata suluhu na wanafunzi na msimamo ulikuwa ni kuwa chuo lazima kiamue nani awe kiongozi.

swali dogo kwako,

Je kipindi chenu uongozi wa chuo ulikuwa unaingilia chaguzi za wanafunzi kama Mkandara anavyotaka kufanya hapa?
 
Kama wizara iliyofikia uamuzi wa kufukuza wanafunzi iko chini ya prof.kuna haja ya kuangalia upya wana taaluma wetu,wanafikia maamuzi kama wanasiasa washangiliaji na si kama wanataaluma walio kwenye siasa......Prof.Kachemsha

ulusungu, Huyu Mkandara ni mshauri wa Kikwete sasa usijiulize kwa nini serikali bado inailipa RIchmond/Dowans mabilioni ya pesa hadi leo hii.
 
Kama nguvu ilitumiwa na mkandala kwa wanafunzi hawa angemshauri raisi wetu akaitumia kwa mafisadi maisha bora kwa kila mtanzania yangewezekana.

Huyu Prof. naona bado anamawazo ya kizamani maana siku hizi kila kitu ni majadiliano yeye anamua kutumia nguvu kutatua mgogoro ambao anajua kabisa athari zake ni kwa taifa na sio mtu mmoja. Hawa vijana wanarudishwa nyumbani wakafanye nini? kama sio kuwa majambazi.
 
Tangu lini mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaamuriwa kuingia darasani? Halafu unamfukuza kwa kutokuingia darasani? Kama uprofesa ni huu, nashukuru mungu sikuzigusa hizo anga tukufu nikabakia fundi mchundo.

Chuo Kikuu gani ambacho hakina wavuta bangi? Clinton alivuta, Obama alitumia mpaka cocaine inasema george W naye haukwa nyuma kwenye haya masuala! Wangapi tumewaona wakitumia hayo majani wakati wa ujana wao na sasa ni viongozi wa kuaminika dunia nzima? Chuo Kikuu kinazuia kubusiana wanafunzi! Hiki ni Chuo Kikuu au shule ya msingi? Ni lazima tuanze kuwa'treat' wanafunzi wa Chuo kikuu kama watu wazima na kuwapa heshima wanayozstahili. Ni lazima tuanze kuheshimu sacrifice na gharama ambayo jamii imeingia kumfikisha huyo mwanafunzi mahali pale. Ni lazima tuanze kutambua kuwa pale na sehemu nyingine kama zile ndiyo font ya vichwa vyetu vya baadae na ni lazima tuwape uhuru wa kutafakhari na kudadisi mambo bila kuwaingilia. Wakitoka hapo, dunia itawaweka sawa lakini wakati wako pale waachiwe waweze kufikia their full potential.

Habari Fundi Mwenzangu:

Ndio kwanza nimerudi kutoka bongo. Moja ya kitu kilichobadilika huko ni vijana wanaoingia vyuoni.

Siku hizi vijana wana umri mdogo sana ukilinganisha na miaka ya nyuma na vilevile katika umri wao mdogo wamekuwa ufunuo wa mambo mengi ya kidunia kuliko wanafunzi wa vizazi vilivyotangulia. Hivyo basi kuna majukumu yaliokuwepo kwa wanafunzi wa vyuo wa miaka ya nyuma sasa hayapo tena.

Kuna watu wanaleta standards zilizotumika miaka ya nyuma kwa wanafunzi wa sasa na kwa maoni yangu hapa tutagonga ukuta.
 
Kama nguvu ilitumiwa na mkandala kwa wanafunzi hawa angemshauri raisi wetu akaitumia kwa mafisadi maisha bora kwa kila mtanzania yangewezekana.

Huyu Prof. naona bado anamawazo ya kizamani maana siku hizi kila kitu ni majadiliano yeye anamua kutumia nguvu kutatua mgogoro ambao anajua kabisa athari zake ni kwa taifa na sio mtu mmoja. Hawa vijana wanarudishwa nyumbani wakafanye nini? kama sio kuwa majambazi.

Mkandara ni dikiteta na fisadi na very soon ataitwa muuaji kwa vifo vilivyotokea hapo mlimani kwenye uongozi wake.
 
Unajua wanafunzi wameshazoeshwa kwamba matatizo yao hayawezi kutatuliwa hadi wagome. Na ni kweli mara nyingi wakigoma hupata walichokuwa wakikitaka. So, it is the question of attitudes. Ndio yale yale tunayoongelea hapa kila siku: respect to the rule of law na ustaarabu. Ongeza na cha tatu sasa: ustahimilivu. Jamii yetu imekuwa jamii isiyo na ustahimilivu. Hakuna patience kabisa. Wanafunzi wetu hawawezi kusibiri hata kidogo.

.

Mzee Kitila nimekukubali sana lakini sentensi hii niliyo-emphasize sikubali. Tatizo si kukosekana kwa ustahamilivu! In fact watanzania we are TOO patient na tunataka vijana wetu wawe hivyovivyo. Haiwezekani and I agree with them, role yao ni kutu-push sisi ambao tumekuwa complacent na comfotrable with the status quo. And since akina Mukandala ndo grown ups ni lazima watambue hilo! And they have to learn to handle that properly allowing the students to channel their frustration ipasavyo.
 
BTW,

nimekumbushwa kuwa jina halisi na mkuu wa chuo (VC) ni Mukandala kwa hiyo kuanzia sasa nitamuita hivyo. Samahani kwa wale wote niliowakwaza kwa kubofya kwenye hilo jina.
 
Bravo Prof. Mukandala and the UDSM to chess the rabbish! The Profs and the ADMN have been there for about 40yrs solving problems of the like-Enough Experience!Hao vijana ni rabbish & Tabula RASAs (Empty Buckets Upstairs). They are driven by emotions but not thoughts. Wajue kuwa wako ktk bus safarini na kila mmoja atashuka mahala pake! Sifa nzao: Failures,VILAZAs Nomoney, Frustrates and Stupid Puppets! They wanna be the losers eventually!.Confused and noise makers. Wanaotaka kusoma watasoma tu no matter the commotion. Hao wegine wata-vanish logically.
 
Wewe na Chenge mnasitahili kuwa kwenye selo moja pale Keko!
 
wanashida gani wakati watoto wao wamejaa huku UK na US wanasoma colleges wakitoka huku wanawekwa bank kuu, kwanza nataka kujua watoto wa magembe wanasoma wapi,mwenye taarifa zao azilete hapa
 
Mwl Kitila

Mimi ninakubali kabisa wanafunzi wameingia staili isiyostaila ama kuweka sawa ni kua wametafuta majibu kwa njia ya mkato sana.

Ila pamoja na hayo yote mimi nalia na huo utawala wa Kinazi ,Maana jinsi utawala ulivyo li-aprochi tatizo ni kama hata shule ya msingi hawakupita.

Ndio nikatoa mfano kua mwanako akikuibia fedha zako na wewe ukanyanyuka ukabeba mikuki,mapanga, na mishoka ukamshambulia

Mimi kwa akili yangu nyepesi kabisa nita ko-femu kua Mwl Kitila atakua na matatizo na wenda ndio sababu ya mwanae kumuibia nitamwachia huyu mwanako na wewe nakutia kitanzi.

Ktk hili la hawa akina mkandala na maghembe inatakiwa watiwe kitanzi kwanza ndio tuje tuangalie tatizo la wanafunzi.
 
Bravo Prof. Mukandala and the UDSM to chess the rabbish! The Profs and the ADMN have been there for about 40yrs solving problems of the like-Enough Experience!Hao vijana ni rabbish & Tabula RASAs (Empty Buckets Upstairs). They are driven by emotions but not thoughts. Wajue kuwa wako ktk bus safarini na kila mmoja atashuka mahala pake! Sifa nzao: Failures,VILAZAs Nomoney, Frustrates and Stupid Puppets! They wanna be the losers eventually!.Confused and noise makers. Wanaotaka kusoma watasoma tu no matter the commotion. Hao wegine wata-vanish logically.

mwafrika wa kike usihangaike na huyu mgonjwa wa Dr Ayoub wa magonjwa ya akili pale muhimbili
 
Bravo Prof. Mukandala and the UDSM to chess the rabbish! The Profs and the ADMN have been there for about 40yrs solving problems of the like-Enough Experience!Hao vijana ni rabbish & Tabula RASAs (Empty Buckets Upstairs). They are driven by emotions but not thoughts. Wajue kuwa wako ktk bus safarini na kila mmoja atashuka mahala pake! Sifa nzao: Failures,VILAZAs Nomoney, Frustrates and Stupid Puppets! They wanna be the losers eventually!.Confused and noise makers. Wanaotaka kusoma watasoma tu no matter the commotion. Hao wegine wata-vanish logically.

Tunafahamu ya kuwa wap ambao wana sifa ulizotaja hapo juu lakini kushabikia vijana wetu kupigwa, kuwekwa rumande na kutolewa mimba, si sahihi! Pia naomba nikuulize ni kwa nini wanafunzi wa Chuo kikuu ni Vialza kama unavyodai? Who are they and how did they become like that? They were NOT born like that. Ni mazingira. Sasa kama mfano wanaoona ni kwamba viongozi wetu wa nchi wanaiba na kutufilisi, na ni vihiyo na wababe, unafikiri what type of role models do they have to look up to? Acha kumwaga propaganda hapa!
 
Back
Top Bottom