#COVID19 Serikali yatoa angalizo maambukizi mapya ya Corona

#COVID19 Serikali yatoa angalizo maambukizi mapya ya Corona

Serikali ya Tanzania imesema kuna viashiria vya wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kuingia nchini kutokana na nchi jirani wananchi wake kuzidi kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mkurugenzi wa kinga wa Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi ametoa maagizo kadhaa likiwemo la kuwataka wananchi kuvaa barakoa.

“Wizara inawakumbusha wananchi wote kutopuuza ugonjwa wa Covid-19. Wizara imeanza kuona viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi yetu.”

“Hii ni kutokana na taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huu zinazofanywa na wizara na mwingiliano kati ya watu wetu na mataifa mengine,” amesema Dk Subi.

Amesema idadi ya wagonjwa wanaokutwa na vizuri vya corona barani Afrika imeongezeka ndani ya wiki tano mfululizo zikiwemo nchi jirani na Tanzania, “maambukizi yanaongezeka maradufu kuliko ilivyokuwa wimbi la pili.”

Katika maelezo yake amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Chanzo: Mwananchi
Kuna watu wangependa tupate wimbi la tatu na wanalingoja kwa hamu sana wapate kitu cha kuzungumza! Mungu alishatuponya na corona!! Tahadhari tunaendelea kuchukua! Ila nchi zingine za kiafrika zinadanganya kuwa kuna wimbi la tatu ili wapate mkopo!!! Akili zingine hapa Afrika wala huwezi kuzielewa! Isitokee hapa kwetu!!
 
Acha upumbavu wa kurukia watu usiowajua humu. Nani alikwambia mimi Mzee? Mwenye matatizo ya akili ni wewe wahi Mirembe.
Nikujue mara ngapi wewe kibabu,

Utazeekea huko Canada I am telling you.

Pigwa hiyo chanjo wewe na vitoto na vijukuu vyako.

Kibabu kijinger kabisa hiki.
 
Poleni sana Mkuu I hope hajaambukiza hapo nyumbani.
kibongo bongo kiukweli hakuna aliechukua tahadhari..
hata walioenda kumtoa hospital na kumuosha hawakuvaa mask zaidi ya gloves tuu..mungu atunusuru tuu.
bado tunachukulia poa sana hii kitu
 
Hunijui sikujui unaonyesha jinsi ulivyo mpumbavu na KUKURUPUKA kujifanya unanijua. Wahi mirembe kabla hujaanza kuokota makopo barabarani.
Huna lolote wewe ushazeeka ,
 
Poleni sana.
kibongo bongo kiukweli hakuna aliechukua tahadhari..
hata walioenda kumtoa hospital na kumuosha hawakuvaa mask zaidi ya gloves tuu..mungu atunusuru tuu.
bado tunachukulia poa sana hii kitu
 
Wapi nilipoishabikia wewe? Hebu weka mstari ambao nimeshaibikia Covid. Acha KUKURUPUKA soma kwa kituo uelewe kilichoandikwa.

Wala usishangae, ndiyo wale mburumundu mkuu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mungu baba muumba wa mbingu na nchi tunakushukuru kwa kuiponya nchi yetu na korona. Tunakuomba uendelee kutukinga na corona. Wewe ndiwe kinga yetu na ngome yetu! Mataifa yote yanashangaa jinsi ambavyo umetulinda na corona!! Wengine wanakataa kuamini lakini matokeo ya usalama wa nchi yetu utawalazimisha waamini! Ninakuomba Baba katika Jina lipitalo majina yote Jina la Yesu Kristo na wote wampendao Mungu waseme -AMINAAAA.
 
Uganda walichanjwa lakini wapi, hii Corona dawa ni kutoipa attention tu, kuvaa barakoa nako ni kama bahati nasibu, mimi nikivaa majirani zangu hawana habari nayo, na sidhani kama barakoa zinazuia 100% nyungu nayo haijathibitishwa popote, maombi?! kwani waganda hawamjui Mungu!, au Mungu ana upendeleo!, sijui tunahitaji kitu gani zaidi kuhusu huu ugonjwa ili tujikinge.
Heri Taifa lile ambalo Mungu wa Israel ni Mungu wao
 
Kuna watu wa ajabu sana Mkuu. Utadhani niliandika kichina hivyo hakuelewa kilichoandikwa.

Hao ni the brainwashed. Wamo humo boda boda, wapiga debe, sungu sungu na wa namna hiyo. Unategemea nini hapo mkuu?
 
Back
Top Bottom