Serikali yatoa mwongozo unyonyeshaji wanafunzi waliojifungua hawaruhusiwi kwenda shuleni na watoto wao badala yake wazazi kuwajibika kuwalea

Serikali yatoa mwongozo unyonyeshaji wanafunzi waliojifungua hawaruhusiwi kwenda shuleni na watoto wao badala yake wazazi kuwajibika kuwalea

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali imesema mwongozo wa wanafunzi wanaorejea shuleni baada ya kujifungua hawaruhusiwi kwenda shuleni na watoto wao na badala yake, unawataka wazazi kusaini makubaliano na uongozi wa shule ya kuwajibika kuwalea wanafunzi na watoto wanaorudi shuleni.

Novemba 24, 2021 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza kuruhusiwa kwa wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito kurejea shuleni kwa mfumo rasmi baada ya kujifungua.

Uamuzi huo ulitokana na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli, kupiga marufuku wanaopata mimba shuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari Juni, 2017.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga ameyasema hayo leo Februari 7, 2025 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Najma Giga.

Katika swali la msingi, Najma amehoji Serikali imejipangaje kuhakikisha watoto wachanga wa wasichana wanaoendelea na masomo wananyonya maziwa ya mama zao kwa wakati.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema kulingana na mwongozo wa wanafunzi wanaorejea shuleni baada ya kujifungua hawaruhusiwi kwenda shuleni na watoto wao na badala yake, mwongozo unawataka wazazi kusaini makubaliano na uongozi wa shule ya kuwajibika kuwalea wanafunzi na watoto wanaorudi shuleni.
 
Back
Top Bottom