Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

Serikali yatoa siku 3 FCC itoe ripoti kwanini bei za Soda zimepanda, pia imetoa siku 7 ijulishwe kwanini Vifaa vya Ujenzi vimepanda Bei

coca cola ni maintenance problem kutokana na ngozi nyeupe walikwenda likizo ya mwisho wa mwisho wa mwaka pia mkanda ukazingua kiwandani. hivyo unatumika mkanda mmoja ndio maana wanazalisha soda aina moja kila baada ya siku kadhaa.walioko hawana ujuzi mpaka warudi ngozi nyeupe.

imepelekea pepsi kutumika kwa wingi kuliko uzalishaji wake. pia jua linachangia watu kunywa vinywaji baridi kwa wingi. tar 20 ngozi nyeupe watakuwepo kwenye nchi ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake
 
Dr. Ashantu namkubali sana ni miongoni mwa Mawaziri Serious kwenye kazi, mfuatiliaji mzuri sana mwenye kujitoa kwa ajili ya wananchi.
naamini kuna jambo litayokea.

Inasikitisha sana kuona tuna wataalamu wa kutosha ktk kila idara za Serikali lkn wamekaaa kimya bidhaaa zinapanda bei ovyoo, bidhaa zinaadimika......wao wapo kimya kama vile hawapo.

watanzania mlio pewa dhamana ktk nafasi mbalimbali badilikeni.
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei...
Mimi siku wakisema kwa nn bei ya chuma imepanda ndipo nitawaelewa
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei...
Yeye mwenyewe Rais wa nchindiye aliamashisha kuwa kila mbuzi ale urefu wa kamba yake, sasa anataka wafanyabiashara wafanyeje?
 
Mimi siku wakisema kwa nn bei ya chuma imepanda ndipo nitawaelewa
Vyuma havishikiki kaka. Kuanzia nondo, hollow, nk.. ni hatareee. Watu wanarudi kwenye mbao tena sasa ivi... milango ya grill na madirisha yanapoteza demand kwa kasi
 
Dr. Ashantu namkubali sana ni miongoni mwa Mawaziri Serious kwenye kazi, mfuatiliaji mzuri sana.
mwenye kujitoa kwa ajili ya wananchi.
naamini kuna jambo litayokea.

Inasikitisha sana kuona tuna wataalamu wa kutosha ktk kila idara za Serikali lkn wamekaaa kimyaaa.........bidhaaa zinapanda bei ovyoo, bidhaa zinaadimika......wao wapo kimya kama vile hawapo......!!!

watanzania mlio pewa dhamana ktk nafasi mbalimbali badilikeni.
Huyu waziri ana mda mrefu,hii nchi imeisha rudi mikononi mwa wafanyabiashara,subiri kidogo utasikia,zile kauli za ninaongea na mwenye mbwa,siongei na mbwa ndio Wakati wake, wengine walishaanza kuitwa viroboto 🤣🤣🤣
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Sida na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.

Source: ITV habari

Kila mtu na ale kwa urefu wa kamba yake
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameitaka tume ya ushindani FCC kutoa ripoti kwa serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Waziri ametoa siku 3 kwa ripoti ya Sida na siku 7 kwa vifaa vya ujenzi ziwe zimemfikia kwani inashangaza kusikia Soda zimeadimika ghafla soda zimerudi na bei iko juu.

Source: ITV habari

Hivi navyo vichekesho vingine! Hivi ina maana hivi vitu vinavyosemwa vimepanda leo?si ni toka budget iliyopita? Hivi mtu kama huyu anakuwaje waziri anashindwa kujua sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa na vitu vingi? Waziri huyu ameshindwa kujua kuwa serikali ndio sababu ya kupanda kwa bei ya bidhaa hasa vifaa vya ujenzi na bidhaa z nishati na gas kwa kuongeza kodi? Hivi huyu waziri hakuwa bungeni? Au na yeye ni mbumbumbu tuu hajui kama wale wanao lala bungeni?

Tume ya ushindani anataka ifanye nini zaidi ya kutaka kuwalazimisha watoe adhabu kwa wafanya biashara kwa kuwaumiza? Kila mtu anajua mafuta yakishapanda kila bidhaa inapanda bei maana anayeumia ni mlaji wa mwisho?

Hivi tume ya ushindani itaweza kutoa lawama kwa serikali kufuatia kusababisha kupanda bei za bidhaa na vifaa vya ujenzi na kilimo kwa kuongeza kodi?

Mbona huyu waziri kama amechanganyikiwa kabisa?
 
Hiyo ni kazi ya wizara ya fedha na benki kuu.
 
Sababu ni hizi..
1. Uhaba wa maji
2. Mgao wa umeme.
3. Kupanda kwa bei za nishati (gesi na petrol)
4. Kodi, ushuru na tozo.
Sababu ya 4 ndio yenye mashiko ila hizo zingine hamna kitu kama hicho
 
coca cola ni maintenance problem kutokana na ngozi nyeupe walikwenda likizo ya mwisho wa mwisho wa mwaka pia mkanda ukazingua kiwandani. hivyo unatumika mkanda mmoja ndio maana wanazalisha soda aina moja kila baada ya siku kadhaa.walioko hawana ujuzi mpaka warudi ngozi nyeupe.

imepelekea pepsi kutumika kwa wingi kuliko uzalishaji wake. pia jua linachangia watu kunywa vinywaji baridi kwa wingi. tar 20 ngozi nyeupe watakuwepo kwenye nchi ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake
Elezea vifaa vya ujenzi sasa.
 
Kupanda kwa vifaa vya Ujenzi kumechangiwa na kutokuwepo kwa msamaha wa kodi kwenye miradi mingi ya Kiserikali inayotekelezwa nchi nzima.
Sababu nyingine ni kutokuwepo kwa bei elekezi ya vifaa vya Ujenzi hasa Nondo, Saruji, Vioo,bati,vyuma/pipes/n.k,Aluminium profiles, vigae, rangi, vifaa vya umeme,sanitaries/bomba na mbao kulingana na ubora.
Ikiwezekana FCC itumie agizo la Mh. Waziri kufanya review ya bei za bidhaa kwa kushirikiana na AQRB/Quantity Surveyors ili kuweka uzani wa bei kulingana na ubora, upatikanaji wake na jiographia ya nchi.
 
coca cola ni maintenance problem kutokana na ngozi nyeupe walikwenda likizo ya mwisho wa mwisho wa mwaka pia mkanda ukazingua kiwandani. hivyo unatumika mkanda mmoja ndio maana wanazalisha soda aina moja kila baada ya siku kadhaa.walioko hawana ujuzi mpaka warudi ngozi nyeupe.

imepelekea pepsi kutumika kwa wingi kuliko uzalishaji wake. pia jua linachangia watu kunywa vinywaji baridi kwa wingi. tar 20 ngozi nyeupe watakuwepo kwenye nchi ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake

Siku wazungu wakiamua kubaki kwao ndio akili zitafanya kazi…wenye nchi wako busy wanakula mikopo kwa urefu wa kamba zao…badala ya kujengea uwezo wananchi kufungua viwanda mbalimbali vya uzalishaji…
 
Back
Top Bottom