Serikali yatoa vyakula na vifaa kwa waathirika wa kimbunga Isimani mkoa wa Iringa

Serikali yatoa vyakula na vifaa kwa waathirika wa kimbunga Isimani mkoa wa Iringa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Serikali imetoa msaada wa vyakula na Vifaa mbalimbali Kwa Wananchi 241wa Kata ya Mlenge na Itunundu zilizopo Jimbo la Isimani, Wilayani Iringa mara baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo.

Wananchi hao wameeleza namna mvua hiyo ilivyowaathiri ikiwemo kupoteza makazi na kusababisha Wananchi wenzao Watatu kupoteza maisha na baadhi ya wengine 59 kukosa makazi vilevile wamesema kuwa mvua hiyo imeharibu akiba ya mazao yao mbalimbali ya chakula yakiwemo mahindi, mchele na maharage.

Akiwasilisha salamu za pole na misaada mbalimbali iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Wahanga hao Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James ameeleza mahitaji yaliyokabidhiwa ni mahindi, mchele, maharage, magodoro, mabati na mifuko ya saruji pamoja na kuwapa huduma za matibabu Wahanga hao.

Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wananchi hao kuendelea kuchukua tadhahari katika kipindi hiki cha mvua sambamba kuwa watulivu kwani Serikali ni Sikivu na ipo tayari kutoa msaada muda wowote panapotokea majanga kwa wananchi wake.

Screenshot 2025-03-27 193401.png
Screenshot 2025-03-27 193419.png
 
Back
Top Bottom