Serikali yatoa zaidi ya milioni 400 wilaya ya Nyang'hwale kwa ajili ya miradi maendeleo

Serikali yatoa zaidi ya milioni 400 wilaya ya Nyang'hwale kwa ajili ya miradi maendeleo

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
1754460261307.png


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'HWALE


TAARIFA KWA UMΜΑ​
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale inautangazia Umma kuwa imepokea Jumla ya Tsh. 410,000,000 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Utawala, Elimu na Afya kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 kama ifuatavyo;

Kiasi cha Tsh. 100,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya Umaliziaji wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.

Kiasi cha Tsh. 60,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara katika Shule ya Sekondari Igalula.

Kiasi cha Tsh.50,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya Ukamilishaji wa Madarasa 3 (Kila Shule darasa 1) Shule ya Msingi Ng'weja, Shule ya Msingi Mwingiro na Shule ya Msingi Kona.

Kiasi cha Tsh. 100,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya.

Kiasi cha Tsh. 50,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Vituo vya Afya.

Kiasi cha Tsh. 50,000,000 kimepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Zahanati.

Imetolewa na,
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale.
Agosti 04, 2025
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyang'hwale, S.L.P 352, Geita Barua pepe: [email protected]
 
Alafu waje kusema hafanyi kazi, ccm wasimkatae mgombea wao 🤣
 
Back
Top Bottom