Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Anaitwa Thobias Andengenye, kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Anasema hiiii
 
Miundo mbinu sio rafiki, hata magari ya kuzima moto ni machache mno.

Na lini soko kubwa hilo kongwe lilifanyiwa ukarabati wa viashiria vya moto?

Pole waliopoteza bidhaa zao kwa moto, serikali ikarabati soko hilo na kuboresha mfumo wa umeme, pamoja na kuweka vifaa vya kisasa vya kubaini dalili za moto na kuzima moto wenyewe.
 
Huo moto kuendelea kuwaka mpaka asubuhi hii ni uthibitisho bado tuna upungufu mkubwa wa vitendea kazi.

Hiyo kamatI ni muendelezo ule ule wa majibu mepesi kwenye maswali magumu, kamati itakuja na mapendekezo yake, yawekwe kapuni, maisha yaendelee.
 
Makao makuu ya Fire ni pua na mdomo na soko kuu la Kariakoo

Kwa daladala nauli ni tsh 300 tu!
Just a walking distance not more than 10 min. Watoto wanaoishi maeneo ya Fire hawajawahi kupanda daladala kwenda shule Benjamin Mkapa au Uhuru Mchanganyiko mbali kuliko Sokoni Kariakoo penyewe kutoka ilipo HQ ya Zimamoto.
 
Waseme tu biashara nyingi mijini zimekosa utaratibu!! Kwa maneno ya Mkuu wa mkoa watu wanatembea na mitungi ya Gesi bila utaratibu na kujiita wanyonge mama lishe.
 
Atuambie bajet imetwengwa bei gani kwajili ya majanga.
 
Huo moto kuendelea kuwaka mpaka asubuhi hii ni uthibitisho bado tuna upungufu mkubwa wa vitendea kazi.
Serikali haijawahi kuwa serious linapokuja suala la majanga kuanzia tetemeko hadi Covid. Mizaha hutawala zaidi kuliko umakini. Tujiandae kudanganywa tena.
 
Huo moto kuendelea kuwaka mpaka asubuhi hii ni uthibitisho bado tuna upungufu mkubwa wa vitendea kazi.

Hiyo kamatI ni muendelezo ule ule wa majibu mepesi kwenye maswali magumu, kamati itakuja na mapendekezo yake, yawekwe kapuni, maisha yaendelee.
Hivi ina maana moto haujazima
 
Hapo wamekosea kuunda kamati. Kawaida Fire wanapaswa wasubmit investigation report. Na wanapaswa waweke wazi fire inspection ya mwisho ilifanywa lini hapo kariakoo, na mapendekezo maana kwa layman pale kulikuwa na mambo mengi tu ya kurekebisha. Waweke wazi certificate kama walipewa na fire fighting training ilifanywa mwisho lini.

Serikali double standards wanavyochunguza makampuni same procedures should apply. Waache siasa...
 
Huyo waziri Mkuu aache utapeli wa kujifanya anaunda tume zisizo na tija. Aseme taarifa ya ile tume ya moto wa lori la mafuta iliishia wapi. Kama kweli hizo tume zina tija kwenye hayo majanga, mbona alificha taarifa ya lile janga la moto ya lori la mafuta Morogoro, hata baada ya kusema hiyo ripoti itawekwa wazi? Wafanyabishara huyo waziri Mkuu hana jipya hapo, bali anaweletea usanii tu lakini hana msaada wowote.
 
Siasa hizi, kwa hiyo baada ya uchunguzi mtawalipa, poleni sana wafanyabiashara wa kariakoo mali za mabilioni zimeteketea mule ndani
 
Dah hizi social media bana,kila mtu amegeuka kuwa mkosoaji cku hz.Sasa ajali imetokea serikali imeunda kamati ya wataalam watu mnakosoa,cjui mnataka life liendelee as if hakijatokea kitu au
 
Kwani Zimamoto wao wanasemaje!!? Maana kutoka pale [emoji602] to Sokoni sio mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…