Serikali yawaita mezani TFF, TPLB, Yanga na Simba kutafuta suluhu ya Dabi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

1742901939445.png
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Pia, Soma
 
Simba ina mechi muhimu Alhamisi. Wabaya wasije wakatumia hilo chaka kutupiga shoti tukapigwa kimazabemazabe.
 
Na Makomandoo pia napendekeza tuitwe kwenye hicho kikao cha kutafuta suluhu! Kinyume na hapo kwenye mechi ya marudio (kama itakuwepo), tutawazuia tena hao simba kuingia uwanjani siku moja kabla ya mechi! Ili wasusie tena kucheza.

Ubaya uoga! 🥵
 
Na Makomandoo pia napendekeza tuitwe kwenye hicho kikao cha kutafuta suluhu! Kinyume na hapo kwenye mechi ya marudio (kama itakuwepo), tutawazuia tena hao simba kuingia uwanjani simu moja kabla ya mechi! Ilo wasusie tena kucheza.

Ubaya uoga! 🥵
Yanga haina ubavu wa kuivimbia serikali, mechi inarudiwa bila masharti
 
Mimi naongea kwa niaba ya Makomandoo wenzangu tuliozuia lile basi kuingia uwanjani siku ile! Tuitwe pia kuhudhuria hicho kikao. Waziri asipofanya hivyo, tutawazuia tena wakati mwingine hao simba.
 
Hiko Kikao hakitafanikiwa,kwa akili za viongozi wa Yanga,Sidhani.
 
Vijana wengi hamfahamu, uu mpira wa miguu unaochezwa leo apa Tanzania Yanga ndio walio uratibu.
Wali leta mtaalamu kutoka Nje ya Tanzania ili atusaidie ku uratibu, kutengeneza uongozi na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.
Yote ayo yalikua juhudi za katibu wa Yanga, Bandawe na wenzake.

Vilabu vingi vya DAR kwa kipindi icho , Cosmo, Good hope n.k vilikua avikubaliani na utaratibu wa kuleta mtu ili atushauri namna ya kubotesha soka letu.
Ao Simba ni timu iliyokua ikifungamana na watawala kwaiyo hawakuhusishwa na lolote.

Yanga ndio wenye mpira wa Tanzania kama utaki amia Burundi, Hakuna yoyote waku itisha wala kuishusha Yanga katika Soka la Tanzania.

Yanga imetawanyika Nchi nzima na mizizi yake ni mirefu apa Nchini sasa msije kujidanganya wakati kwenye mpira wa nchi hii mmekuja juzibti.
 
Redio siku hizi zinaandika?
 
Serikali inaingilia mambo ya soccer huko CAF na kule FIFA. Sheria zinasemaje
 
Uwezo wanao sana kumbuka FIFA hairuhusu serikali kuingilia mamlaka ya mpira
Narudia kusema hawana huo uwezo.

Pamoja na hizo sheria za FIFA na CAF, nitajie kiongozi yeyote wa klabu za Tanzania anayeweza kuivimbia serikali, au hata kuongoza kikao cha kugomea mechi.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Pia, Soma
Yanga na Simba ni vikundi vya siasa za mpira.
 
Narudia kusema hawana huo uwezo.

Nitajie kiongozi yeyote wa klabu za Tanzania anayeweza kuivimbia serikali, au hata kuongoza kikao cha kugomea mechi.
Sema kiongozi wa Simba au Yanga. Hawa kwenye timu wapo kama vivuli tu. Wanaoamua Yanga au Simba ifanye nini na wakati gani wako mafichoni huko. Ukweli ni kwamba watacheza tu ni suala la muda🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Vijana wengi hamfahamu, uu mpira wa miguu unaochezwa leo apa Tanzania Yanga ndio walio uratibu.
Wali leta mtaalamu kutoka Nje ya Tanzania ili atusaidie ku uratibu, kutengeneza uongozi na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.
Yote ayo yalikua juhudi za katibu wa Yanga, Bandawe na wenzake.

Vilabu vingi vya DAR kwa kipindi icho , Cosmo, Good hope n.k vilikua avikubaliani na utaratibu wa kuleta mtu ili atushauri namna ya kubotesha soka letu.
Ao Simba ni timu iliyokua ikifungamana na watawala kwaiyo hawakuhusishwa na lolote.

Yanga ndio wenye mpira wa Tanzania kama utaki amia Burundi, Hakuna yoyote waku itisha wala kuishusha Yanga katika Soka la Tanzania.

Yanga imetawanyika Nchi nzima na mizizi yake ni mirefu apa Nchini sasa msije kujidanganya wakati kwenye mpira wa nchi hii mmekuja juzibti.
Huu ndio upuuzi wanmashabiki wa Yanga na Somba kujiona wao ndio wamiliki wa mpira. Wanasahau kuwa mpira sasa hivi ni biashara ya dunia nzima na mtu yeyote anaweza kuifanya.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Pia, Soma
Huu ndiyo mda mwafaka wa nchi kufungiwa kisoka, mpira nchi hii umejaa uhun na ujanja ujajanya, haswa pale TFF
 
Back
Top Bottom