Serikali yawaita mezani TFF, TPLB, Yanga na Simba kutafuta suluhu ya Dabi

Serikali yawaita mezani TFF, TPLB, Yanga na Simba kutafuta suluhu ya Dabi

Huu ndio upuuzi wanmashabiki wa Yanga na Somba kujiona wao ndio wamiliki wa mpira. Wanasahau kuwa mpira sasa hivi ni biashara ya dunia nzima na mtu yeyote anaweza kuifanya.
Ata mpira ukiwa wa kibiashara una taratibu zake za ku usimamiia, Yanga mara zote wamefuata izo taratibu.

Yanga wakati uo inaitwa Jangwani 1934 ili panda ligi kuu ya mkoa wa DAR iliyokua ikisimamiwa na Wakoloni.
Ikashushwa mwaka 1935 kwa figisu za wakoloni na ilikua timu pekee yenye waafrika tupu ikipambana na timu za Serikali za wakoloni.
1935 lika anziahwa Zengwe kwa kuhongwa baadhi ya viongozi na wachezaji ambao walianzisha iyo simba ikianzia na jina la wakoloni queens.
Yanga ili rudi kwenye ligi na kucheza fainali 1939 wkati uo ikii twa Young boys/ Jangwani boys katika Sun lite cup.
Sasa mambo waliyo fanyiwa Yanga 1934 chini ya Wakoloni hayakubaliki kujirudia 2025 chini yaWallace Karia na Bodi ya ligi.
Uko Yanga ilishatoka.
 
Sio mnataka point za mezani mnamuogopa MPANZU
Na Makomandoo pia napendekeza tuitwe kwenye hicho kikao cha kutafuta suluhu! Kinyume na hapo kwenye mechi ya marudio (kama itakuwepo), tutawazuia tena hao simba kuingia uwanjani siku moja kabla ya mechi! Ili wasusie tena kucheza.

Ubaya uoga! 🥵
 
Vijana wengi hamfahamu, uu mpira wa miguu unaochezwa leo apa Tanzania Yanga ndio walio uratibu.
Wali leta mtaalamu kutoka Nje ya Tanzania ili atusaidie ku uratibu, kutengeneza uongozi na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.
Yote ayo yalikua juhudi za katibu wa Yanga, Bandawe na wenzake.

Vilabu vingi vya DAR kwa kipindi icho , Cosmo, Good hope n.k vilikua avikubaliani na utaratibu wa kuleta mtu ili atushauri namna ya kubotesha soka letu.
Ao Simba ni timu iliyokua ikifungamana na watawala kwaiyo hawakuhusishwa na lolote.

Yanga ndio wenye mpira wa Tanzania kama utaki amia Burundi, Hakuna yoyote waku itisha wala kuishusha Yanga katika Soka la Tanzania.

Yanga imetawanyika Nchi nzima na mizizi yake ni mirefu apa Nchini sasa msije kujidanganya wakati kwenye mpira wa nchi hii mmekuja juzibti.
Pamoja na maelezo yote hayo mazuri bado Yanga watacheza tu mechi dhidi ya Simba bodi ikiwa imetangaza tar mpya
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Pia, Soma
Tutafunga nà FIFA hivi karibuni, serikali wafanye siosà za kumsifia Samia mpira watuache wanamichezo. Kabudi sidhani kama hata anajua timu uwanjani inatakiwa iwe na wachezaji wangapi
 
Back
Top Bottom