Serikali yawalipia viingilio Maafisa Habari wa Serikali kushuhudia mechi ya Tanzania Vs Uganda

Serikali yawalipia viingilio Maafisa Habari wa Serikali kushuhudia mechi ya Tanzania Vs Uganda

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Wizara ya Habari itawalipia Maafisa Habari wote viingilio vya kwenda kushuhudia mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Mkapa (Jumanne Machi 27. 2023).

Waziri Mkuu amesema hayo wakati akihutubia katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Njerere, Dar es Salaam, leo Jumatatu Machi 27, 2023.

Mbali na kuwalipia kiingilio cha mchezo huo, Msemaji wa Serikal, Gerson Msigwa amesema Wanahabari hao wataandaliwa usafiri pia wa kwenda na kurudi.

Mchezo huo wa kuwania Kufuzu Michuano ya Afrika AFCON ni wa marudio baina ya timu hizo baada ya Tanzania kushinda goli 1-0 katika mchezo uliopita wa Kundi F.
View attachment 2567447

View attachment 2567448
The Cranes tunawacheki tu
 
Amewalipia yeye au wanalipiwa na serikali; watu hawa wana vyeo na mishahara mikubwa wanaweza kujinunulia tiketi zao wenyewe.
 
Back
Top Bottom