Samvulachole
JF-Expert Member
- Oct 22, 2006
- 413
- 118
Huko nyuma niliandika hivi kuhusu hili swala hata nami nimefarajika na mwanzo waliouonyesha kwenye hili nawashukuruni wote humu mlioshiriki kwenye kujadili hili na kutoa mawazo na ufumbuzi mzuri utapatikana kupitia nguvu ya umma.Shie tuendelee kukaza buti!Ni wapi kati ya vijana hao waliopo kwenye Picha wamepatwa na mkasa huo?
Vyama vya upinzani vinafanya nini? kwaninin wasijaribu angalau kuwanunulia tiketi hao vijana kutoka kwenye vyanzo vyao vya fedha kuonyesha wao wapo tofauti na watawala au hilo nalo wanangoja mwalimu kutoka ughaibuni?
mkandara. hahaha tulioifahamu tanzania ni sie tuliofunzwa na maisha sio nyie mliofunzwa shuleni. hao vijana kama wanaifahamu kweli tanzania wasingefika kulala hapo nje ya ubalozi wa uingereza.siasa inacheza ngoma na humu jf pia watu wanataka kuanzisha mtaji juu ya hili.upeo wangu ni wa kufahamu namna ya kutatua tatizo bila msaada na hii ndio elimu nilofundishwa katika mitaa bila ya shule. mwenye shida hukimbilia kwao .hawajawa na shida hao wakiwa na shida wataomba deportation.nahisi tu kuna kutaka umaarufu katika kuiendeleza hii issue sio kutatua tatizo.acha nibomoke .sasa akijiuzulu msolla enhee hebu tuelezeeni kinachofatia tukufahamuni vizuri.au ndo tukuapishe wewe mkandara?mmmmh
mkandara.
labda nikubaliane na wewe mmejadiliana mengi kuhusu tanznia.je kushawahi kuanzishwa hii petition ya kusaini ili flani ajiuzulu kwa sababu kuna wanafunzi wamenyimwa elimu za sekondari na chini ya hapo kutokana na itikadi zao za kivyama ,mikoa,kidini na mengineyo?? na kuna aliejiuzulu? nipe maupdate , si unajua tena mwanangu mie ni wa juzi! khaaaaaaaaaaa. mukianza kutetea haki anzeni kutetea moja muende mbili mkianza mbili kwenda moja sie wengine tutahisi mna manufaa yenu tu kwenye hiyo issue. hebu naomba mmoja alete petition ya kusaini ili waziri wa elimu ajiuzulu kwa sababu kuna watoto hawapewi nafasi ya kwenda shule za msingi kabla ya kurukia walionyimwa chuo kikuu.hapo nitawaelewa.
HabariLeo; Monday,May 28, 2007 @00:04
VIONGOZI wa vyama vinne vya siasa kwa kushirikiana na Shirika linalohusika na masuala ya Elimu ya Sheria (TANLET) wamefungua akaunti benki kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Tanzania waliokwama Ukraine.
Kwa kuanzia, familia za viongozi hao zimetoa Sh milioni moja na wametoa mwito kwa Watanzania wenye huruma kuwachangia wanafunzi hao.
Tunaomba wachangie kwa kaulimbiu, mwanangu je, angekuwepo ingekuwaje? Wasaidie Watanzania wenzetu. Wanafunzi 29 wamefukuzwa katika vyuo vya Ukraine kwa kushindwa kulipa ada. Wanafunzi hao kwa sasa wanahifadhiwa katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine na iwapo Serikali itashindwa kuwatumia ada wanaweza kunyanganywa hati za kusafiria na kushitakiwa.
Kwa mujibu wa wapinzani hao, suala hilo haliwezi kuingizwa kwenye itikadi za vyama, hivyo wameomba kila mtu mwenye kuguswa achangie kiasi chochote katika akaunti hiyo itakayofunguliwa.
Walisema gharama za vyuo kwa kila mwanafunzi Ukraine ni Sh milioni 3 kwa mwanafunzi mmoja. Wanafunzi hao walikwenda nchini humo baada ya kuhakikishiwa na bodi ya mikopo kuwa watakopeshwa fedha hizo ili mradi wajigharimie nauli ya kwenda na kurudi.
Licha ya kutoa mchango huo, viongozi hao wamemshutumu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla kuwa anatakiwa kujiuzulu, wakidai kwamba amepuuza kushughulikia tatizo la ada linalowakabili wanafunzi hao walioko Ukraine.
Viongozi hao, Augustine Mrema wa TLP, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Freeman Mbowe (Chadema), jana kwa pamoja walitoa tamko wakilalamika kuhusu ukimya wa Serikali juu ya wanafunzi hao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Profesa Lipumba alisema wanavyoona wao, Profesa Msolla haonyeshi kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kuhudumia Watanzania. Anambomoa, hivyo hafai kushikilia wadhifa huo kwani kazi yake kubwa ni kugombana na wanafunzi, alisema Profesa Lipumba na kuongeza kwamba wanataka Waziri Msolla ajiuzulu.
Under Age Na Uhurubado,
Jamani eeeh kama hamna issue na upeo jaribuni kukaa pembeni.
Sasa ikiwa mnapinga haya ya vijana -ELIMU kwa sababu ya njaa iliyopo nyumbani mnachoomba ni kipi hasa!
Vijana wasipewe mikopo na bado mnalia njaa tumefanya nini?..Nadhani kama mnaweza kuzisoma mada zote zilizomo humu mtaelewa kwamba zimegusia kila shida ya Mtanzania.
Na ni katika kuorodhesha mapungufu hayo ndipo unapojenga hoja kubwa ya waziri kujiuzulu kwani huwezi kusema Msolla ajiuzulu kwa sababu ya maji safi na vyandarua!..
Fungua Mada inayohusu maji na vyandarua utaona watu waki -support vilevile na kama upo ushahidi wa kutosha kuwa waziri fulani kapuuza sera ama agizo la taifa tutaomba pia ajiuzulu.
Mwendo hatua ndugu zangu!