Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Mwanakijiji:hakuna ushindi mkubwa katika jambo hili kama huu. What I liked about this is the fact that the guys have gone beyond maneno. Huu ndio uongozi, kuonesha njia.

Yaani tungekuwa karibu tunaonana leo ungekunywa Tusker yangu japokuwa nasikia wewe mwenzangu bia hunywi; kwa furaha niliyonayo ingebidi unywe!
 
Yeeeeeesss!

Ama kweli UMOJA ni nguvu, utengano ni Udhaifu!...

Undeni chama kipya naomba KADI!!
 
Under Age Na Uhurubado,

Jamani eeeh kama hamna issue na upeo jaribuni kukaa pembeni.
Sasa ikiwa mnapinga haya ya vijana -ELIMU kwa sababu ya njaa iliyopo nyumbani mnachoomba ni kipi hasa!
Vijana wasipewe mikopo na bado mnalia njaa tumefanya nini?..Nadhani kama mnaweza kuzisoma mada zote zilizomo humu mtaelewa kwamba zimegusia kila shida ya Mtanzania.
Na ni katika kuorodhesha mapungufu hayo ndipo unapojenga hoja kubwa ya waziri kujiuzulu kwani huwezi kusema Msolla ajiuzulu kwa sababu ya maji safi na vyandarua!..
Fungua Mada inayohusu maji na vyandarua utaona watu waki -support vilevile na kama upo ushahidi wa kutosha kuwa waziri fulani kapuuza sera ama agizo la taifa tutaomba pia ajiuzulu.

Mwendo hatua ndugu zangu!
 
Mimi pia kadi tafadhali........
Alute continue........,Mapambano yanaendelea until to the bottom of this.
 
Ni wapi kati ya vijana hao waliopo kwenye Picha wamepatwa na mkasa huo?
Vyama vya upinzani vinafanya nini? kwaninin wasijaribu angalau kuwanunulia tiketi hao vijana kutoka kwenye vyanzo vyao vya fedha kuonyesha wao wapo tofauti na watawala au hilo nalo wanangoja mwalimu kutoka ughaibuni?
Huko nyuma niliandika hivi kuhusu hili swala hata nami nimefarajika na mwanzo waliouonyesha kwenye hili nawashukuruni wote humu mlioshiriki kwenye kujadili hili na kutoa mawazo na ufumbuzi mzuri utapatikana kupitia nguvu ya umma.Shie tuendelee kukaza buti!
 
mkandara. hahaha tulioifahamu tanzania ni sie tuliofunzwa na maisha sio nyie mliofunzwa shuleni. hao vijana kama wanaifahamu kweli tanzania wasingefika kulala hapo nje ya ubalozi wa uingereza.siasa inacheza ngoma na humu jf pia watu wanataka kuanzisha mtaji juu ya hili.upeo wangu ni wa kufahamu namna ya kutatua tatizo bila msaada na hii ndio elimu nilofundishwa katika mitaa bila ya shule. mwenye shida hukimbilia kwao .hawajawa na shida hao wakiwa na shida wataomba deportation.nahisi tu kuna kutaka umaarufu katika kuiendeleza hii issue sio kutatua tatizo.acha nibomoke .sasa akijiuzulu msolla enhee hebu tuelezeeni kinachofatia tukufahamuni vizuri.au ndo tukuapishe wewe mkandara?mmmmh
 
mkandara.
labda nikubaliane na wewe mmejadiliana mengi kuhusu tanznia.je kushawahi kuanzishwa hii petition ya kusaini ili flani ajiuzulu kwa sababu kuna wanafunzi wamenyimwa elimu za sekondari na chini ya hapo kutokana na itikadi zao za kivyama ,mikoa,kidini na mengineyo?? na kuna aliejiuzulu? nipe maupdate , si unajua tena mwanangu mie ni wa juzi! khaaaaaaaaaaa. mukianza kutetea haki anzeni kutetea moja muende mbili mkianza mbili kwenda moja sie wengine tutahisi mna manufaa yenu tu kwenye hiyo issue. hebu naomba mmoja alete petition ya kusaini ili waziri wa elimu ajiuzulu kwa sababu kuna watoto hawapewi nafasi ya kwenda shule za msingi kabla ya kurukia walionyimwa chuo kikuu.hapo nitawaelewa.
 
Under-Age, kuanzishwa kwa petition its a step ya kuwa huko nyuma hatukuwa tukifanya hivi, ilipofikia sasa nikufanya hivyo. Nani anataka umaarufu hao vijana au? kama watu wa JF hata majina yao hawajulikani..Umaarufu Gani? maisha gani yalokufunza wewe? kitendo cha kujifunza Internet na kujua hata forum ni kuonesha umepitia shule maalum ila unatumika vibaya.wenzako wanatumika kuendeleza nchi yao. Wewe ndie unaefurahia vijana kukosa elim. Step ya vijana walipofikia ni kubwa..kwa vitendo hivi wanavyofanyiwa na serikali, ile ARI ya kutumikia Nchi inaondoka. For ur infomation hakuna mtu anaependa kuwa Nje ya nchi alozaliwa, ni matatizo ndio yanayomfanya awe hivyo. Nikuulize kwanini Kikwete Mwanae anasoma UK, wakati Masters yake ya Siasa ipo UDSM?...Kuna baadhi ya Masters ukifanyia Tanzania bado elim yako inakuwa chini..hasa Engineeing na Medicine...lkn Political Scince au Law ni kitengo cha mdar mrefu..ambayo mtu anaweza somea Bongo...Kimsingi unachotakiwa kuangalia ni wakati gani Governm inahitaji kusifiwa na wakati gani inahitajika kurekebishwa..
 
mkandara. hahaha tulioifahamu tanzania ni sie tuliofunzwa na maisha sio nyie mliofunzwa shuleni. hao vijana kama wanaifahamu kweli tanzania wasingefika kulala hapo nje ya ubalozi wa uingereza.siasa inacheza ngoma na humu jf pia watu wanataka kuanzisha mtaji juu ya hili.upeo wangu ni wa kufahamu namna ya kutatua tatizo bila msaada na hii ndio elimu nilofundishwa katika mitaa bila ya shule. mwenye shida hukimbilia kwao .hawajawa na shida hao wakiwa na shida wataomba deportation.nahisi tu kuna kutaka umaarufu katika kuiendeleza hii issue sio kutatua tatizo.acha nibomoke .sasa akijiuzulu msolla enhee hebu tuelezeeni kinachofatia tukufahamuni vizuri.au ndo tukuapishe wewe mkandara?mmmmh

Nadhani lingekuwa jambo la busara kama ungeleta hiyo habari ya hao waliokataliwa shule kisa itikadi/dini/kabila alafu watu wakajadili. Kuhusu kusomeshwa na serikali, nina uhakika asilimia kubwa ya viongozi wetu wengi wamesomeshwa na serikali maana wengi wao isingekuwa serikali wangekuwa bado wako vijijini mwao wanafuga ng'ombe na kulima kwa kutumia majembe ya mkono.
Shukrani yao ya kusomeshwa na hela za walipa kodi ndio hii tunayoiona leo(kuwatelekeza wanafunzi nje ya nchi). Hili swala lilipofikia ni crisis ya kimataifa imagine walipa kodi wa Uingereza wakianza kuhoji kuhusu hao vijana kuweka makazi kwenye Ubalozi wao unafikiria hilo swali atalijibu Msolla ama mwenyekiti wa bodi ya Mikopo? Mtoto wa Mhe. anasoma bila tatizo lolote na kapangishiwa apartment nzuri tuu nadhani na aliikuta hiko full furnished imagine hayo yangemkuta huyo kijana unafikiria waziri angekuwa na kiburi cha kukata simu?
 
mkandara.
labda nikubaliane na wewe mmejadiliana mengi kuhusu tanznia.je kushawahi kuanzishwa hii petition ya kusaini ili flani ajiuzulu kwa sababu kuna wanafunzi wamenyimwa elimu za sekondari na chini ya hapo kutokana na itikadi zao za kivyama ,mikoa,kidini na mengineyo?? na kuna aliejiuzulu? nipe maupdate , si unajua tena mwanangu mie ni wa juzi! khaaaaaaaaaaa. mukianza kutetea haki anzeni kutetea moja muende mbili mkianza mbili kwenda moja sie wengine tutahisi mna manufaa yenu tu kwenye hiyo issue. hebu naomba mmoja alete petition ya kusaini ili waziri wa elimu ajiuzulu kwa sababu kuna watoto hawapewi nafasi ya kwenda shule za msingi kabla ya kurukia walionyimwa chuo kikuu.hapo nitawaelewa.

Sina budi kabla ya mengineyo, nikusifie kwa uchaguzi wako wa jina linaloafikiana vizuri na fikra zako.

Kama ungetumia muda wako kidogo na kusoma kwa makini mambo mengi yaliyojadiliwa katika mijadala mbalimbali kwenye mtandao huu, ungegundua kwamba mengi ya hayo unayoyazungumzia kuhusu siasa na maendeleo ya waTanzania ndio mambo yanayozungumziwa sana humu kila siku, na ungeweza kufahamu kuwa kumtaka Msolla ajiuzuru sio jambo lililorukiwa tu bila ya sababu. Hakuna anayekupinga kuhusu uduni wa maisha ya mTanzania wa kawaida, na hili hukuligundua wewe pekee, sote tunalifahamu vizuri.

Unataka tukuamini kuwa kuna watu humu walio na ajenda zao binafsi, na ndizo zinazoweka msukumo wa kampeni ya Msolla ajiuzuru! Inawezekana mawazo yako hayo yakawa na ukweli ndani yake, lakini pia usisahau kuwa watu humu sio ma-robot. Ninakuhakikishia kuwa nusu, au hata robo tu ya waTanzania tungekuwa tumefikia ufahamu wa mambo yanayoihusu nchi yetu kama uliomo humu hali yetu ya kisiasa na kiuchumi ingekuwa ni tofauti kabisa na ilivyo sasa. Hata hiyo CCM yetu tu ingekuwa na hata moja ya nane ya watu wenye mawazo pevu kama ya watu wengi waliomo humu tungekuwa na ahueni kubwa kisiasa; badala ya chama kilichojaa ma-opportunists tupu wanaolinda maslahi ya kujaza matumbo yao kwanza.

Ungekuwa ni mfuatiliaji wa mambo ungeelewa kuwa sababu ya kumtaka Msolla ajiuzuru sio kwa kushindwa kuwasaidia vijana 29 waliokwama Kiev peke yake. Lakini hata hiyo ni sababu tosha kabisa kwa kiongozi anayejua majukumu yake vizuri kuachia ngazi. Naona labda kwa sababu ya huo 'u-under-age' ulionao unakufanya usiweze kutambua wajibu wa taifa kwa raia zake wakati wanapokuwa nje, na hasa raia waliopewa baraka zote za kuondoka nchini na serikali yenyewe. Kwa bahati mbaya, utakapokuwa mtu wa umri wa kuweza kutambua aibu na karaha zinazoambatana na matukio ya aina hii, ndio utakapofahamu kuwa hata kuutaja utaifa wako huko nje litakuwa ni jambo la kusita na pengine kulionea aibu.
 
Hi! Hi! Hi Mwe!
Sielewi ni lini mtu amevaa kibwaya kujivunia kuto kwenda shule.
Pengine maana ya shule kwako Underage ni kusoma sekondari na chuo tu.
Shule ya msingi na yale uliyo jifunza kwa wazazi wako pia kupitia kila mtu unaye changamana naye kwako si shule.
Mtu akisoma mpaka chuo anaendeleza elimu yake katika upana wake tu.
Hata hapa tunaporumbana ni shule tosha.
Uzuri wa marumbano haya ya mtandaoni ni kwamba watu wanaweka wazi hisia zao bila woga kama kumwaga radhi kwenye mdundiko.
Hii inatusaidia kujua wote kwa pamoja tukitafuta mwafaka wamawazo yetu kitazaliwa nini.
Kimsingi mawazo yote ni sahihi na wasemaji wote wanahaki sawa.
Lakini kwenye mzani wa mtandaoni si kila mmoja ana uzito sawa.
Wengine tukipimwa na mzani wa mtandao mawazo yetu yana uzito wa unyoya na wengine mawazo yao ni mazito kiasi cha kuuvunja mzani wenyewe. Lakini kwa vile uzito nio uzito haidhuru hata kidogo.
Labda tuchukulie kwamba kweli shule ni kwenda Chuo kikuu.
Hivi wewe unadhani ujanja mwingi wa mtaani umezaliwa mtaani? Ujanja mwingi ulianzia vyuoni miaka kibao iliyo pita ukasambaa mtaani sasa ulipo kutana na wewe, wewe unadhani ni mtaa ulio zaa ujanja huo.
Pamoja na kuusifia mtaa kwa kukupa ujanja bado mtaa unategemea unacho kiita shule.
Kwa mantiki ndefu shule ni kila kitu unacho jifunza kwamba kinakujenga au la bado ni shule.
Lakini hata hivyo bado tutahitaji watu kadhaa kwenda nje ya mipaka yetu kuleta ujanja mpya utakao mwagwa mitaani miaka 30 ijayo ili wale walio kosa kwenda vyuoni waone ni ujanja wa mitaani tu. Zoezi hili litaendelea kujirudia tena na tena.
Kuhusu kwamba mtu akiwa na matatizo anakimbilia kwao kama suruhisho la mwisho mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia 49 kwa asilimia 51 na kupinga kabisa. Hapo tanzania kuna Wakimbizi kibao wana matatizo kwa nini wasichukue jukumu la kikimbilia kwao kama suruhisho la mwisho?
Wahindi wamejazana Bongo na wengine wanazidi kuja nasikia wanafanya hivyo kwa vile kwao kuna matatatizo kwa nini wasikimbilie India?
Wazungu matatizo yalipowazidi kwao walianza kutafuta mahali pa kutatulia matattizo yao wakaja kwetu wakatutawala kwa nini wasibaki kwao kama suruhisho la mwisho?
Dar ina watu kibao kutoka mikoa yote ya bara wengine hawana hata mahali pa kulala wengine wanalala kwa zamu kwenye vibanda vyao huku kwao madongo wameacha nyumba zenye nafasi. Kwa nini watu hawa wanazidi kutaabika dar wasikimbilie kwao madongo kama suruhisho?

Hawa vijana walioko Ukraine wamekwenda Ughaibhuni huku wakiwa na kwao sawa kabisa na mtu anaye acha nyumba kubwa na shibe ya futari ya mihogo na ufuta kwao madongo na kuja kusotea chochote hapa Dar.

Sisi tunawatetea hawa vijana wa Ukraine kwa hoja kama ni suala moja wapo lililo jitokeza na siyo kama suala pekee. Tunafanya hivyo kwa vile huo mtaa unao usema tunaujua fika na shule tunaijua pia.

Naomba kutoa hoja.
 
mwiiiiiiiiiiii nimerudi. hili porojo mnalotia looooooooooote bado hamjaonekana kufahamu lolote kutoka kwangu.na ndio tatizo la wasomi wa kileo mnaitazama siasa na dunia kwa mtazamo wa kisomi tu na kusahau kwamba jamii imejengeka kwa wasomi na wasiokuwa wasomi.

Hivi nikikwambieni hawa vijana hayo matatizo wamejitafutia mtakataa? nchi yenyewe inakopeshwa halafu na wewe ukategemee kupata mkopo kwa nchi inayokopeshwa si utakuwa chizi wewe? wale walobaki makwao wakalala wao hawajui thamani ya elimu? au ndo mnapigania haki? tetea haki ya mnyonge kabla haki ya msomi! kumeanzishwa account maalum hapa ya kuwasaidia vijana hao 29,ingekuwa la maana ikaanzishwa account ya kuwasaidia wasiokuwa na maji wakajengewa visima hapa bongo?

okoa maisha kabla ya kuokoa kinachopamba maisha. Watu wameongea na rais hapa kuhusu hao vijana 29, ningependa nimsikie mtu huyo huyo ajigharamie kuongea na rais kuhusu walokosa elimu ya msingi kabla ya waliokosa vyuo vikuu. Tatizo lenu nyinyi sio kuwatetea hawa vijana bali ni kuwapa headline na umuhimu ambao mngeliwapa wanaostahiki kutetewa umuhimu kama huu basi nadhani tanzania ingekuwa ishakomboka zamani.

Mnaweza mkasema ndo mnaanza sasa lakini naona mmeanza chuo kikuu kabla ya shule ya msingi. Wengie wenu hapa mna maisha ya kusoma magazeti kwenye internet ndo mkajua yaliojiri duniani. Hamna ukweli wowote kuhusu wanyonge zaidi ya siasa za kusoma magazeti. Hebu ingieni mitaani na vichochoroni muone hali halisi ya maisha ndo mtajua nani apewe umuhimu kwanza? Mwanafunzi alokwenda Ukraine kwa hiari yake? Au raia Mtanzania anaekosa pa kula na kulala bila hiari yake?

Mpigie simu raisi leo mwambie kuna wapemba waliachishwa masomo shule za Chake Chake wakiwa kidato cha pili kutokana na itikadi zao za kisiasa halafu anzisheni account wanafunzi hawa waendelezwe kabla ya wanafunzi wa Ukraine, anzisha mfuko wa kusaidia mayatima leo wasome hapa JF, nitakufahamu, kinamama wanauza miili yao na kuihatarisha na maradhi ili tu wapate kijio cha siku moja,saidia hawa kabla ya wengine.

Kama hamjaskia hayo basi mjue ni wanasiasa wa magazetini nyie na hamjui lolote kuhusu maisha.mkiona wenzenu wa ulaya wanauzulu watu kwa mambo kama haya ni kwasababu washayakamilisha ya msingi katika maisha ya binadamu, wana umeme, maji na mahitaji muhimu ya binadamu. Hakuna atakaekukatazeni kutetea hapa ninachokuambieni angalieni lipi la kulipa umuhimu kwanza?

Hivi hao vijana leo wakiomba warejeshwe makwao hawatorejeshwa? Si msomi lakini nadhani ukitaka deportation basi kwenu utarejshwa hata kama huna nauli. Hivyo vijipesa mlivyokusanya kama vipo katafuteni mayatima muwape angalau wapate kijielimu cha kuandika a na b. Ushauri wa bure. Khaaaaaaaaaaa ndo maana nikaambiwa na mzee adhabu ya kaburi aijua maiti. Ni kweli adhabu tunayoipata wanyonge tunaijua wanyonge tu.

Kama mngeijua basi mngetuchangia na sisi. Aaaaaaaaaaakh hebu ntoke zangu weee ulimwengu wa wasomi niwaachie wasomi wenyewe nisije nikaadhirika.
 
madela.
suala si kuwatetea bali ni umuhimu mnaowapa.hakuna nilichokiona zaidi ya watu kutafuta umaarufu kupitia hawa vijana.
 
Shadrack Sagati
HabariLeo; Monday,May 28, 2007 @00:04

VIONGOZI wa vyama vinne vya siasa kwa kushirikiana na Shirika linalohusika na masuala ya Elimu ya Sheria (TANLET) wamefungua akaunti benki kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Tanzania waliokwama Ukraine.

Kwa kuanzia, familia za viongozi hao zimetoa Sh milioni moja na wametoa mwito kwa Watanzania wenye huruma kuwachangia wanafunzi hao.

“Tunaomba wachangie kwa kaulimbiu, mwanangu je, angekuwepo ingekuwaje? Wasaidie Watanzania wenzetu.” Wanafunzi 29 wamefukuzwa katika vyuo vya Ukraine kwa kushindwa kulipa ada. Wanafunzi hao kwa sasa wanahifadhiwa katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine na iwapo Serikali itashindwa kuwatumia ada wanaweza kunyang’anywa hati za kusafiria na kushitakiwa.

Kwa mujibu wa wapinzani hao, suala hilo haliwezi kuingizwa kwenye itikadi za vyama, hivyo wameomba kila mtu mwenye kuguswa achangie kiasi chochote katika akaunti hiyo itakayofunguliwa.

Walisema gharama za vyuo kwa kila mwanafunzi Ukraine ni Sh milioni 3 kwa mwanafunzi mmoja. Wanafunzi hao walikwenda nchini humo baada ya kuhakikishiwa na bodi ya mikopo kuwa watakopeshwa fedha hizo ili mradi wajigharimie nauli ya kwenda na kurudi.

Licha ya kutoa mchango huo, viongozi hao wamemshutumu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla kuwa anatakiwa kujiuzulu, wakidai kwamba amepuuza kushughulikia tatizo la ada linalowakabili wanafunzi hao walioko Ukraine.

Viongozi hao, Augustine Mrema wa TLP, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Freeman Mbowe (Chadema), jana kwa pamoja walitoa tamko wakilalamika kuhusu ukimya wa Serikali juu ya wanafunzi hao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Profesa Lipumba alisema wanavyoona wao, Profesa Msolla haonyeshi kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kuhudumia Watanzania. “Anambomoa, hivyo hafai kushikilia wadhifa huo kwani kazi yake kubwa ni kugombana na wanafunzi,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza kwamba wanataka Waziri Msolla ajiuzulu.
 
Nawapa pongezi kwa kulifanyia hili kazi nA KAMA UKILIANGALIA TAMKO UTAJUA KWAMBA WALIOANDIKA WAMETUMIA MANENO YALIYOWEKWQA HUMU NA MWANAKIJIJI.

hilo inatuonyesha kuwa wakina mnyika na wengine wanafanyia kazi mawazo yaliyopo humu na hii ni ushindi kwa JF wote.

Naambiwa kuwa pia mahojiano yaliyofanywa na mwjj,yaliwekwa kwenye CD na waandishi wote walipewa kama ushahidi na kuna utata mkubwa hivi sasa kwani aliyesema kwamba anakula huu umekuwa ni mzigo mzito kwenye kauli yake na kuna taarifa kwamba ameitisha kikao na wahariri leo jioni,
 
Under Age Na Uhurubado,

Jamani eeeh kama hamna issue na upeo jaribuni kukaa pembeni.
Sasa ikiwa mnapinga haya ya vijana -ELIMU kwa sababu ya njaa iliyopo nyumbani mnachoomba ni kipi hasa!
Vijana wasipewe mikopo na bado mnalia njaa tumefanya nini?..Nadhani kama mnaweza kuzisoma mada zote zilizomo humu mtaelewa kwamba zimegusia kila shida ya Mtanzania.
Na ni katika kuorodhesha mapungufu hayo ndipo unapojenga hoja kubwa ya waziri kujiuzulu kwani huwezi kusema Msolla ajiuzulu kwa sababu ya maji safi na vyandarua!..
Fungua Mada inayohusu maji na vyandarua utaona watu waki -support vilevile na kama upo ushahidi wa kutosha kuwa waziri fulani kapuuza sera ama agizo la taifa tutaomba pia ajiuzulu.

Mwendo hatua ndugu zangu!

Samahani, sikujuwa kuwa huu ni ukumbi kwa wale wenye upeo mkubwa tu! Sie wenye upeo mdogo huwa tunaamini mara nyingi tatizo huwa ni mfumo na siyo mtu mmoja, ndo maana hatuwezi kurupuka kuomba mtu mmoja atoke, kwa vile hata huyo ataekuja lazima atakunjwa kuendana na mfumo uliopo. Kwaheri!
 
Back
Top Bottom