Nzokanhyilu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2007
- 1,078
- 101
i) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walienda Ukraine kwa kujilipia ticket zao wenyewe?
ii) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walikataliwa udhamini tangu awali?
iii) Vipi kuhusu madai ya serikali kuwa wanafunzi 17 "walikubali" ushauri wa serikali wa kutafuta shule nyumbani na mikopo yao kuhamishwa? na hivi sasa wanafunzi hao wanaendelea na masomo nyumbani?
iv) Hivi ni wanafunzi wangapi waliokwama maana leo tunasikia ni 26 na siyo 29?
Naogopa kwamba kama maelezo ya serikali sio ya kweli, basi tuna shida kubwa mno maana tunaongozwa na serikali isyoogopa kusema uongo! Itakuwa sio mbaya sana kwa hawa vijana ndio wanaosema uongo, lakini kama ni serikali, mmh!
Tukiendelea na jitihada za ku-raise profile na kuwasaidia hawa vijana, tusiogope kujua ukweli wa jambo lenyewe, in and out. Ukweli hufungua.
HabariLeo; Tuesday,May 29, 2007 @00:01
HATIMAYE Serikali imetoa tamko kuhusiana na hatima ya wanafunzi 29 waliosimamishwa masomo katika vyuo vya elimu ya juu Ukraine kutokana na kushindwa kulipa ada. Katika tamko lililotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestin Gesimba, Serikali imewataka wanafunzi hao kurejea nyumbani mara moja.
Alisema katika mwaka wa masomo wa 2005/06, wanafunzi 130 walipata udahili katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Ukraine na kati yao ni wanafunzi 84 ndio waliokamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na walijiunga na vyuo hivyo.
Kaimu Katibu Mkuu huyo aliendelea kueleza kwamba wanafunzi wengine 46 hawakuweza kukamilisha taratibu hizo na walishauriwa wajiunge na vyuo vya elimu ya juu vya hapa nchini, kwa vile serikali haikuwa na uwezo wa fedha.
Alisema wanafunzi 17 kati ya wanafunzi hao 46 walikubali kutafuta udahili kwa vyuo vya elimu ya juu nchini na wanafunzi 29 ambao ndiyo waliofikwa na matatizo ya ada nchini Ukraine hivi sasa, hawakukubaliana na ushauri huo wa serikali wa kusoma nchini.
Alisema wanafunzi hao wamekwama kulipa ada na sasa wamesimamishwa masomo na wanaulazimisha ubalozi wa Tanzania ulioko Moscow, uiombe Serikali iwasaidie. Wakati Serikali ikitoa tamko hilo, imeripotiwa kwamba wanafunzi hao sasa wamekwenda kuweka kambi katika Ubalozi wa Uingereza mjini Moscow wakiomba Serikali ya Uingereza iwasaidie, kwa vile Serikali ya Tanzania imeshindwa kuwasaidia.
Hatua hiyo imekuja siku chache tangu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na matawi yake walipogoma na kusimamishwa masomo na baadaye kurejeshwa vyuoni kutokana na kuibana Serikali kuwakopesha asilimia 100 ya ada na fedha za matibabu. Pamoja na kuibana kwa kila hali ili Serikali itimize azma yao hiyo, bado Serikali ilisisitiza kwamba haikuwa na fedha za kutosha za kuwakopesha kwa asilimia 100, wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu, hatua ambayo iliwafanya wanafunzi hao kugomea masomo na baadaye kusimamishwa masomo.
Tamko hilo la serikali dhidi ya wanafunzi hawa wa Ukraine, halina ubishi kwamba limetokana na kosa lililofanywa na wanafunzi hao la kudharau ushauri wa serikali yao. Ni wazi kwamba Serikali haikuwa na fedha za kuwakopesha wanafunzi hao ili waende kusoma nje ya nchi na ndiyo maana iliwashauri kutafuta vyuo vya ndani ikiamini kwamba ulipaji wake ni nafuu zaidi.
Ukweli huu unathibitishwa na kitendo cha kushindwa kuwapa asilimia 100 ya mkopo hata kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu vya hapa nchini, hatua iliyowafanya waone kama serikali yao inawanyanyasa na kugomea masomo.
Kwa vile hili limekwisha kutokea ni vizuri kwa wanafunzi hawa wakajifunza kutoka kwa wenzao wa vyuo vya juu nchini ambao pamoja na kuishinikiza serikali kuwapa fedha walizotaka, shindwa kufanya hivyo na wakajikuta wakiingia katika mgogoro uliosababisha kusimamishwa
masomo.
Nazidi kuchanganyikiwa kuhusu hawa vijana. Utaratibu wake uko vipi hasa kati ya serikali yenyewe na bodi ya mikopo.... nani mwamuzi wa nani apewe mkopo ama asipewe.
Kuna maswali mengiune yanajitokeza akilini mwangu!
1. Kutotambuliwa kwao kunakuja vipi hasa ikiwa wizara imetoa barua za kwenda kuomba visa hali bodi ya mikopo iliwakataa!...
2.Na wao kwa ujinga gani uliowapeleka Ukraine hali wakijua mikopo yao imekataliwa na hawana uwezo wa kujisomesha!...
3. Ilikuwaje serikali itoe maagizo ya hawa vijana kutoweza kwenda mwaka 2005/06 hali hawa vijana wanajisomesha wao wenyewe...
4. Serikali ilihusika vipi ktk swala la hawa vijana mwaka huo wakati wakifahamu hawawatambui hawa vijana hadi kuahirisha masomo yao.. bearing in mind watajisomesha wao wenyewe?
Sidhani kama serikali ina majibu ktk haya zaidi ya kuukana ukweli wa ahadi zake!
HabariLeo; Tuesday,May 29, 2007 @00:02
SERIKALI imewataka wanafunzi wa Tanzania waliosimamishwa masomo Ukraine na kupiga kambi katika Ubalozi wa Uingereza kuomba wasaidiwe, kuondoka ubalozini hapo na kurejea nyumbani mara moja.
Katika hatua yake hiyo, Serikali imewatumia wanafunzi hao tiketi za safari ili warejee nchini na kusema watakaogoma waende vyuoni kuendelea na masomo kwa gharama zao na wazazi wao.
Agizo hilo la Serikali lilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestin Gesimba Dar es Salaam jana. Gesimba alisema katika mwaka wa masomo wa 2005/06, wanafunzi 130 walipata udahili katika vyuo vikuu mbalimbali Ukraine na kati yao ni wanafunzi 84 ndiyo waliokamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na walijiunga na vyuo hivyo.
Alisema wanafunzi wengine 46 ambao hawakuweza kukamilisha taratibu hizo walishauriwa wajiunge na vyuo vya elimu ya juu vya nchini kwa vile serikali haikuwa na uwezo wa fedha wa kuwakopesha wanafunzi wapya nje ya nchi.
Alisema wanafunzi 17 kati ya wanafunzi hao 46 walikubali kutafuta udahili kwa vyuo vya elimu ya juu nchini na wanafunzi 29 ambao ndiyo waliofikwa na matatizo ya ada nchini Ukraine hivi sasa hawakukubaliana na ushauri huo wa serikali.
Alisema badala yake wanafunzi hao waliamua kwenda Ukraine kwa utaratibu wao binafsi na kujiunga na vyuo walivyovipenda wenyewe. "Mwaka wa masomo wa 2006/07, mwongozo wa kupata mkopo ulibadilika. Serikali iliona ni vema ikazingatia kuwakopesha wanafunzi waliopata udahili nchini ambako gharama ni ndogo kuliko vyuo vya nje," alisema Gesimba.
Alisema wanafunzi hao 29 wa Ukraine waliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mkopo na walijibiwa kwamba serikali haikuwa na fedha za kuweza kuwakopesha na walishauriwa watafute udahili katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
"Kwa uamuzi wao waliamua kujilipia nauli na kwenda Ukraine bila idhini ya serikali au ahadi ya maandishi kwamba wangeweza kusaidiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu," alisema Gesimba.
Alisema wanafunzi hao sasa wamekwama kulipa ada na sasa wamesimamishwa masomo na wanaushinikiza ubalozi wa Tanzania ulioko Moscow, uiombe serikali iwasaidie. Alisema wazazi wa wanafunzi hao wanapaswa kuwalipia ada wanafunzi hao kwa vile serikali haiwajibiki na gharama zinazojitokeza kwa elimu ya wanafunzi walio nje ya nchi.
?
Kuhusu hiyo STUDENTS LOAN BOARD inabidi iwe privatised kabisaaa na serikali ikae pembeni iiache hiyo mamlaka ifanye kazi yake hru bila kuingiliwa japo still itakuwa inmulikwa na vyombo bya serikali ili kusijetokea uhuni wetu wa sikuzote (kama vile Udini na Ukabila na uoendeleo mwingineo)
1. OMBI KWA MKJJ,Tafadhali, unaweza kupata barua za offer za hiyo mikopo ya hao vijana, waliyopewa na serikali? please nadhani hii itatuondolea hisia wengi wakina Thomas. Maana, mimi siamini kabisa kwamba serikali inaweza kupeleka watu nje harafu ikawa-disown, mchana kweupe tena kwa confidence ya hali ya juu namna hii (ninayemfahamu aliyekuwa na confidence ya namna hii ni Donald Rumsfield!). Please, hii itatusaidia wengi especially skeptics akina Mkandara and the rest. Maana siamini kwamba Jamhuri yetu na matatizo yake yote..it can commit this crime..bila sababu..Otherwise tuanze kuappeal kuomba msaada kama raia walipa kodi na wapiga kura! After all its still our governement.