Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Wazo zuri,

I always felt this issue was for the government to deal with it. I mean, there is no point in politicians/leaders preaching to Tanzanians abroad (be it in Botswana or other parts of africa, Europe, USA, Canada etc) to go back home and share their education and experiences, while its obvious they have no time to invest on the next generation of Tanzanian leaders (economists, scientists, engineers etc).

Your suggestion is very good, I dont see a better solution for now. Any decision that will result in these students going back home or being refugees (or result in injuries or loss of lives), will send the wrong signals.
 
defunc... nakusikia.. kama serikali iko tayari kutumia shilingi milioni 35 kuwarudisha nyumbani, kwanini isitumie fedha hizo na ziada kidogo kulipia deni lililopo na kuwafanyia utaratibu wa kuendelea na masomo? Unajua kiasi wanachodaiwa kwa muda huu ni karibu shilingi milioni 40?
 
Nimesoma taarifa ya serikali iliyotolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya EJST. Pamoja na mambo mengine taarifa inasema kwamba hawa wanafunzi 29 walikataliwa na serikali udhamini tangu 2005/2006 na kwamba walijisafirisha wenyewe na walitarajiwa kulipia gharama zao wenyewe. Taarifa hii inatofautiana sana na maelezo ambayo tumekuwa tukiyapata hapa. Tulielezwa kwamba hawa vijana walipata udhamini wa serikali kwa ajili ya mwaka wa masomo 2005/2006, lakini hawakwenda mwaka huo na badala yake wakaenda 2006/2007. Kwa sisi wengine tuliona hili ni tatizo dogo la kilogostiki tu ambalo lisingweza kufuta udhamini. Lakini maelezo yaliyotolewa na serikali jana ni tofauti mno.

Kwa kuwa MKJJ umeongea na hawa wanafunzi mara nyingi, naomba uni/utufafanulie kidogo hapa kwa dodoso ya maswali haya

i) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walienda Ukraine kwa kujilipia ticket zao wenyewe?

ii) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walikataliwa udhamini tangu awali?

Naogopa kwamba kama maelezo ya serikali sio ya kweli, basi tuna shida kubwa mno maana tunaongozwa na serikali isyoogopa kusema uongo! Itakuwa sio mbaya sana kwa hawa vijana ndio wanaosema uongo, lakini kama ni serikali, mmh!

Tukiendelea na jitihada za ku-raise profile na kuwasaidia hawa vijana, tusiogope kujua ukweli wa jambo lenyewe, in and out. Ukweli hufungua.
 
i) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walienda Ukraine kwa kujilipia ticket zao wenyewe?

Ndiyo, kwa sababu serikali ilikataa kufanya malipo ya tiketi kutokana na matatizo waliyoyapata huko nyumba ambapo hela ya tiketi ilikatwa toka kwenye mikopo. Ni kwa sababu hiyo serikali iliwataka wanafunzi wenye uwezo wa kukata tiketi wafanye hivyo na kuondoka.
ii) Je, ni kweli kwamba hawa vijana walikataliwa udhamini tangu awali?

Huu ni upotoshaji wa wazi. Wanafunzi hawa siyo tu walikubaliwa mikopo kwa mwaka 2005/2006 bali pia baadhi yao waliandikiwa barua na bodi kwa waajiri wao ili waweze kupata ruhusa ya kwenda kusoma. Kama wanafunzi hawa hawakupata udhamini, serikali iweke hadharani majina ya wanafunzi wote waliopata mikopo ya kwenda Ukraine mwaka 2005 yaliyokuwa kwenye batches 6-8 na tuone kama majina YOTE 26 hayamo.

Niongeze maswali mengine na kuyajibu:
iii) Vipi kuhusu madai ya serikali kuwa wanafunzi 17 "walikubali" ushauri wa serikali wa kutafuta shule nyumbani na mikopo yao kuhamishwa? na hivi sasa wanafunzi hao wanaendelea na masomo nyumbani?

Hoja hii inaonesha ni jinsi gani serikali imekurupuka tu bila kufuatilia jambo hili kwa kina. Kuhusu wanafunzi hao 17 ukweli ni huu. Wanafunzi wote hao walikubaliwa wakati mmona na wale 29 kwenda kusoma Ukraine, na wote walitakiwa kujipeleka wenyewe huko Ukraine na fedha zao za mikopo zitafuata. Wanafunzi 29 waliondoka kwa nyakati tofauti wakitanguliwa na wawili kati yao wakiwa na return tickets. Waliondoka kwa ndege za mashirika tofauti (majina ninayo). Wanafunzi 12 kati ya wale 17 ambao Gisema alizungumzia jana wao pia walipata tiketi kwa United Arab Emerites na waliondoka kwa masomo kuelekea Kiev. Wao pia waliondoka wakiwa na matumaini kuwa mikopo yao inawafuata huko Ukraine. Kufika Abu Dhabi walipata matatizo kutokana na tiketi zao kuonesha "one way" na nusura warudishwe pale. Balozi wetu wakati huo Bw. Mustafa Nyang'anyi aliingilia kati na wanafunzi wakaendelea na safari.

Kufika jijini Kiev, wanafunzi hao hawakuruhusiwa kuendelea vyuoni kutokana na kutokamilisha taratibu mbalimbali za kiuhamiaji hadi balozi Chokala naye alipojaribu kuingilia kati. Hata hivyo wanafunzi hao 12 wakarudishwa Tanzania. Hawa mikopo yao ikahamishwa kwenye vyuo vya huko Tanzania, siyo mikopo mipya!! Wale wanafunzi 5 waliosalia hawakuwa na uwezo wa kukata tiketi kuondoka na mikopo yao ikahamishiwa hapo hapo Tanzania. Wanafunzi hao waliendelea na masomo nyumbani kutokana na mikopo ya 2005/2006 kwani mabadiliko ya 2006 yalikuwa hayajaingia bado! Kama wanafunzi wale 12 wangeendelea na masomo Kiev kama hawa wengine basi tungekuwa tunazungumzia 41 waliokwama Ukraine!!!

iv) Hivi ni wanafunzi wangapi waliokwama maana leo tunasikia ni 26 na siyo 29?

mwanzoni mwa sakata hili wanafunzi 29 walikuwa wanahusika. Hata hivyo kutokana na "maajabu ya Musa" wanafunzi watatu kati ya hawa wazazi wao waliweza "kuzungumza kwa herufi kubwa" na viongozi wa bodi ya mikopo na watoto wao wameanza kupewa mikopo! Hawa watatu wanapokea mikopo licha ya kuja pamoja na katika mazingira yale yale na hawa 26, serikali ituambie hawa watatu wamestahili mikopo kwa utaratibu gani ambao haukuweza kuwahusisha hawa 26 wengine? hauendi kati!

Naogopa kwamba kama maelezo ya serikali sio ya kweli, basi tuna shida kubwa mno maana tunaongozwa na serikali isyoogopa kusema uongo! Itakuwa sio mbaya sana kwa hawa vijana ndio wanaosema uongo, lakini kama ni serikali, mmh!

Mwanasiasa, nasikitika kukutangazia kuwa kwa hili serikali imewaongopea wananchi mchana kweupe. Nimechambua mambo haya kwenye makala yangu kesho na kuonesha kuwa jaribio la serikali kutufunga goli la kuotea limeshindwa kwani kibendera changu tayari kiko juu! mpira

Tukiendelea na jitihada za ku-raise profile na kuwasaidia hawa vijana, tusiogope kujua ukweli wa jambo lenyewe, in and out. Ukweli hufungua.

Akaunti imeshafunguliwa na namba tayari zipo na sasa hivi nasubiri swift codes n.k ili tuziweke hadharani. Lengo ni

a. Kutafuta fedha za dharura
b. Kuchangisha kiasi cha kuweza kuwatolesheza kuwasomesha vijana hawa bila ya msaada wa serikali. Kama serikali imeshindwa haina maana Watanzania wameshindwa.
 
NASHANNGAA HAKUNA ALIYEKUJA NA STATISTICS ZINAZOELEZA KUWA:

Serikali inasomesha wanafunzi wangapi nje? kwa gharama gani? wangapi wanazamia? wangapi walirudi? na ufanisi wao tangu waliporudi ni upi? wanatoka kwenye backgrounds zipi?

zaidi ya hayo mimi nitapropose radical measures na kubwa zichukuliwe na serikali mojawapo ni:

-SERIKALI IFUTE NA IJIONDOE KABISA KUWASOMESHA WATU NJE YA NCHI

-WANATAKIWA KUIPRIVATISE HIYO BODY YA KUTOA MIKOPO

-SERIKALI IACHANE NA MIRADI MIKUBWA MIKUBWA YA KUJENGA UNIVERSITY(kwani private bodies wanafanya hivyo na kazi ya serikali iwe ni kuregulate tu standards)

-WALIOPO NJE KAMA HAWA WALIOPO UKRAINE WALIPIWE ...hata kama ni mwaka ao wa kwanza LAKINI HUU NDIO UWE MWAKA WA MWISHO KUSPONSOR WATU KWENDA KUSOMA NJE
 
DrWho, mapendekezo yako mengine nakubaliana nayo ila hilo la kujiondoa moja kwa moja kusomesha wanafunzi. Mwanzoni nilikuwa nafikiria jambo kama hilo lakini nikakumbuana na matatizo kadhaa.

a. Tatizo la Kikatiba.
Serikali haiwezi kutunga sheria yenye kuonesha ubaguzi wa aina yoyote wa moja kwa moja au wa taathira yake. Kama inajitoa kusomesha wanafunzi basi ijitoe kote kwa kote, yaani isisomeshe nyumbani au nje ya nchi!

b. Serikali ikijitoa kabisa kusomesha wanafunzi basi utaona kuwa wale watakaosoma wataendelea kutoka kwenye familia chache na hivyo elimu itazidi kuwa bidhaa ambayo wale wenye uwezo zaidi ndio watakaoinunua!

Nakubaliana na wewe kuwa utaratibu mzuri na wa kisasa wa kutoa mikopo ya elimu ubuniwe na mojawapo ni kuivunja kabisa hii bodi ya mikopo ilivyo sasa na badala yake iundwe "mamlaka ya mikopo ya elimu" na ambayo itashughulikia mikopo ya elimu kwa kiwango chochote kile. Kwa vile hii ni mikopo basi mambo ya kusema mtu hapewi kabisa mkopo ni jambo la kipuuzi. Kila mwenye uwezo wa kukopa na kulipa apewe mkopo.

Kumbuka kuwa wanafunzi hawa hawaombi fedha za dezo (grants) wanaomba mkopo! Kama serikali inaweza kutafuta fedha za kuwakopesha nauli ya kurudi bila ya shaka wanaweza kabisa kutafuta fedha za kuwasomesha kwa mkopo.
 
Cha msingi na kwa faida ya kila mtu kuielewa hii ishu ipo vipi, itakuwa vizuri kama itawekwa wazi ilikuwaje wao waende kusoma nje, je walipokuwa wanaenda huko walijua kama serikali itawalipia au walikuwa wa wadhamini ( sponsor ) wa kuwalipia,. na kama serikali ilikubali kuwalipia then mimi nitaunga mkono kila kitu kinachosemwa hapa kwa ni LAZIMA serikali iwalipie LA HASHA kama hawakuwa na MAKUBALIANO na SERIKALI basi naona SI LAZIMA kwa serikali kufanya tunachoomba wafanye ( kwani ni OMBI ) na ombi sio lazima kukubaliwa angalau hapa TUNASISITIZA tukubaliwe !!

Nitashukuru kama mtaweka kila kitu wazi tokea mwanzo hadi hapa walipo ili kila mtu apate kuelewa picha halisi inayochezwa otherwise watu watakuwa wanafuata tu bandwagon !
 
Nazidi kuchanganyikiwa kuhusu hawa vijana. Utaratibu wake uko vipi hasa kati ya serikali yenyewe na bodi ya mikopo.... nani mwamuzi wa nani apewe mkopo ama asipewe.
Kuna maswali mengiune yanajitokeza akilini mwangu!

1. Kutotambuliwa kwao kunakuja vipi hasa ikiwa wizara imetoa barua za kwenda kuomba visa hali bodi ya mikopo iliwakataa!...
2.Na wao kwa ujinga gani uliowapeleka Ukraine hali wakijua mikopo yao imekataliwa na hawana uwezo wa kujisomesha!...
3. Ilikuwaje serikali itoe maagizo ya hawa vijana kutoweza kwenda mwaka 2005/06 hali hawa vijana wanajisomesha wao wenyewe...
4. Serikali ilihusika vipi ktk swala la hawa vijana mwaka huo wakati wakifahamu hawawatambui hawa vijana hadi kuahirisha masomo yao.. bearing in mind watajisomesha wao wenyewe?

Sidhani kama serikali ina majibu ktk haya zaidi ya kuukana ukweli wa ahadi zake!
 
nimesoma kule tanzatl kwamba wanafunzi hao waliondoka tz na kuwaaga wazazi wao kwamba wana private sponsorship ( kumaanisha serikali haihusiki ) ( UNAONA HAPO UTATA UNAPOTOKEA !! ) Sasa basi permanent secretary katoa taarifa aidha wanafunzi warudi nyumbani na watalipiwa ticket ya ndege ( lakini watarudisha hizo fedha pindi tu watakapofika tz ) au waendelee kusoma huko ukraine kwa gharama zao wenyewe !

Duh, hadi hapa ndugu zangu sina la kusema, kilichobaki ni kuombea usalama wao na afya njema ! Hilo ndilo jambo kuu mengine yatafuata baadae !
 
Wanafunzi wa Ukraine wajifunze kutoka kwa wenzao wa UDSM
OSCAR MBUZA
HabariLeo; Tuesday,May 29, 2007 @00:01

HATIMAYE Serikali imetoa tamko kuhusiana na hatima ya wanafunzi 29 waliosimamishwa masomo katika vyuo vya elimu ya juu Ukraine kutokana na kushindwa kulipa ada. Katika tamko lililotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestin Gesimba, Serikali imewataka wanafunzi hao kurejea nyumbani mara moja.

Alisema katika mwaka wa masomo wa 2005/06, wanafunzi 130 walipata udahili katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Ukraine na kati yao ni wanafunzi 84 ndio waliokamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na walijiunga na vyuo hivyo.

Kaimu Katibu Mkuu huyo aliendelea kueleza kwamba wanafunzi wengine 46 hawakuweza kukamilisha taratibu hizo na walishauriwa wajiunge na vyuo vya elimu ya juu vya hapa nchini, kwa vile serikali haikuwa na uwezo wa fedha.

Alisema wanafunzi 17 kati ya wanafunzi hao 46 walikubali kutafuta udahili kwa vyuo vya elimu ya juu nchini na wanafunzi 29 ambao ndiyo waliofikwa na matatizo ya ada nchini Ukraine hivi sasa, hawakukubaliana na ushauri huo wa serikali wa kusoma nchini.

Alisema wanafunzi hao wamekwama kulipa ada na sasa wamesimamishwa masomo na wanaulazimisha ubalozi wa Tanzania ulioko Moscow, uiombe Serikali iwasaidie. Wakati Serikali ikitoa tamko hilo, imeripotiwa kwamba wanafunzi hao sasa wamekwenda kuweka kambi katika Ubalozi wa Uingereza mjini Moscow wakiomba Serikali ya Uingereza iwasaidie, kwa vile Serikali ya Tanzania imeshindwa kuwasaidia.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na matawi yake walipogoma na kusimamishwa masomo na baadaye kurejeshwa vyuoni kutokana na kuibana Serikali kuwakopesha asilimia 100 ya ada na fedha za matibabu. Pamoja na kuibana kwa kila hali ili Serikali itimize azma yao hiyo, bado Serikali ilisisitiza kwamba haikuwa na fedha za kutosha za kuwakopesha kwa asilimia 100, wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu, hatua ambayo iliwafanya wanafunzi hao kugomea masomo na baadaye kusimamishwa masomo.

Tamko hilo la serikali dhidi ya wanafunzi hawa wa Ukraine, halina ubishi kwamba limetokana na kosa lililofanywa na wanafunzi hao la kudharau ushauri wa serikali yao. Ni wazi kwamba Serikali haikuwa na fedha za kuwakopesha wanafunzi hao ili waende kusoma nje ya nchi na ndiyo maana iliwashauri kutafuta vyuo vya ndani ikiamini kwamba ulipaji wake ni nafuu zaidi.

Ukweli huu unathibitishwa na kitendo cha kushindwa kuwapa asilimia 100 ya mkopo hata kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu vya hapa nchini, hatua iliyowafanya waone kama serikali yao inawanyanyasa na kugomea masomo.

Kwa vile hili limekwisha kutokea ni vizuri kwa wanafunzi hawa wakajifunza kutoka kwa wenzao wa vyuo vya juu nchini ambao pamoja na kuishinikiza serikali kuwapa fedha walizotaka, shindwa kufanya hivyo na wakajikuta wakiingia katika mgogoro uliosababisha kusimamishwa
masomo.

Maoni yangu:
Uandishi wa kutofanya uchunguzi! Hivi bw. Oscar anaeleza kwanini ameamini kuwa serikali imesema kweli?

KadaMpinzani:
Serikali inaweza kwa njia rahisi kabisa kuthibitisha kuwa haiwatambui kwa kutoa hadharani barua au "ushauri" uliotolewa kwa wanafunzi hawa. Tunawaomba waoneshe barua, au taarifa iliyotumwa kwa vijana hawa kuwa serikali haina fedha na wasiende Ukraine. Hiyo barua yenye maagizo ambayo vijana "17" waliyasikiliza na kuyafuata!!
 
Nazidi kuchanganyikiwa kuhusu hawa vijana. Utaratibu wake uko vipi hasa kati ya serikali yenyewe na bodi ya mikopo.... nani mwamuzi wa nani apewe mkopo ama asipewe.
Kuna maswali mengiune yanajitokeza akilini mwangu!

1. Kutotambuliwa kwao kunakuja vipi hasa ikiwa wizara imetoa barua za kwenda kuomba visa hali bodi ya mikopo iliwakataa!...
2.Na wao kwa ujinga gani uliowapeleka Ukraine hali wakijua mikopo yao imekataliwa na hawana uwezo wa kujisomesha!...
3. Ilikuwaje serikali itoe maagizo ya hawa vijana kutoweza kwenda mwaka 2005/06 hali hawa vijana wanajisomesha wao wenyewe...
4. Serikali ilihusika vipi ktk swala la hawa vijana mwaka huo wakati wakifahamu hawawatambui hawa vijana hadi kuahirisha masomo yao.. bearing in mind watajisomesha wao wenyewe?

Sidhani kama serikali ina majibu ktk haya zaidi ya kuukana ukweli wa ahadi zake!

Unadhani serikali hii ya JK ipo tayari kupata lawama kwa kitu ambacho walihitaji kufanya hata kabla hili zogo halijaija, ila ninachofahamu ni kwamba serikali hii ya JK ipo tayari kupata lawama iwapo tu viongozi husika watanufaika ( mfano, richmond ) lakini kwa wanafunzi wa ukraine, wanajua kabisa hamna dili unadhani muda woooote huo wamekaa kimya ndio waanze kujishughulisha now ? are u kidding me ?

Msinielewe vibaya, ila sina imani KABISA kwamba serikali itaweza kuwasomesha huko na ikitokea hivyo basi ni miujiza !
Come on people, je tumefungwa vitambaa usoni mwetu ? leo hii tunadhani hatuijui gov't ya JK ? .....
 
Oscar Mbuza
HabariLeo; Tuesday,May 29, 2007 @00:02

SERIKALI imewataka wanafunzi wa Tanzania waliosimamishwa masomo Ukraine na kupiga kambi katika Ubalozi wa Uingereza kuomba wasaidiwe, kuondoka ubalozini hapo na kurejea nyumbani mara moja.

Katika hatua yake hiyo, Serikali imewatumia wanafunzi hao tiketi za safari ili warejee nchini na kusema watakaogoma waende vyuoni kuendelea na masomo kwa gharama zao na wazazi wao.

Agizo hilo la Serikali lilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestin Gesimba Dar es Salaam jana. Gesimba alisema katika mwaka wa masomo wa 2005/06, wanafunzi 130 walipata udahili katika vyuo vikuu mbalimbali Ukraine na kati yao ni wanafunzi 84 ndiyo waliokamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na walijiunga na vyuo hivyo.

Alisema wanafunzi wengine 46 ambao hawakuweza kukamilisha taratibu hizo walishauriwa wajiunge na vyuo vya elimu ya juu vya nchini kwa vile serikali haikuwa na uwezo wa fedha wa kuwakopesha wanafunzi wapya nje ya nchi.

Alisema wanafunzi 17 kati ya wanafunzi hao 46 walikubali kutafuta udahili kwa vyuo vya elimu ya juu nchini na wanafunzi 29 ambao ndiyo waliofikwa na matatizo ya ada nchini Ukraine hivi sasa hawakukubaliana na ushauri huo wa serikali.

Alisema badala yake wanafunzi hao waliamua kwenda Ukraine kwa utaratibu wao binafsi na kujiunga na vyuo walivyovipenda wenyewe. "Mwaka wa masomo wa 2006/07, mwongozo wa kupata mkopo ulibadilika. Serikali iliona ni vema ikazingatia kuwakopesha wanafunzi waliopata udahili nchini ambako gharama ni ndogo kuliko vyuo vya nje," alisema Gesimba.

Alisema wanafunzi hao 29 wa Ukraine waliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mkopo na walijibiwa kwamba serikali haikuwa na fedha za kuweza kuwakopesha na walishauriwa watafute udahili katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
"Kwa uamuzi wao waliamua kujilipia nauli na kwenda Ukraine bila idhini ya serikali au ahadi ya maandishi kwamba wangeweza kusaidiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu," alisema Gesimba.

Alisema wanafunzi hao sasa wamekwama kulipa ada na sasa wamesimamishwa masomo na wanaushinikiza ubalozi wa Tanzania ulioko Moscow, uiombe serikali iwasaidie. Alisema wazazi wa wanafunzi hao wanapaswa kuwalipia ada wanafunzi hao kwa vile serikali haiwajibiki na gharama zinazojitokeza kwa elimu ya wanafunzi walio nje ya nchi.

Maoni yangu:

Tunaomba Bw. Gesimba watuoneshe majina ya wanafunzi waliokubaliwa mikopo kwenda Ukraine mwaka 2005/2006. Zaidi ya yote, watuoneshe agizo la serikali la kushindwa kufanya hivyo kwa maandishi lililotumwa kwa wanafunzi!
 
Unajua Mwanakijiji mimi sian imani na waandishi pamoja na magazeti ya nyumbani

Bwana Mwanakijiji unajua wewe bado kuna kitu hukielewei kuhusu hawa waandishi. Unajua wao huwa wanakuja humu kunyonya kisha wanaongezea chumvi zao kisha wanalipwa kwa habari walioandika

lakini tukirudi kwenye point ya awali ni kwamba nakubali serikali KUSOMESHA RAIA WAKE NI BASIC HUMAN RIGHT pamoja na ya KIKATIBA

Lakini still sikubaliani ulazima wa serikali kuwasomesha WANAFUNZI pamoja na FANAYAKAZI WAKE NJE YA NCHI

HIVI UNAJUA WIZARA NGAPI ZA SERIKALI ZINASOMESHA WAFANYAKAZI WAKE NJE KUPITIA GOVT SPONSORPHIP?

ninachokisema kuwa VYuo tunavyo na dawa ni kuvipatia vifanyia kazi kwa pesa tunazosevu kuwasomesha LULUKI la watu wa serikali huko Nje

Kama kuna mwanafunzi anazo private funds then fair enough lakini siyo eti mtu anatoka huko hataki kusoma Bongo naye ataka aende ulaya kwa pesa za serikali hiyo NINAIPINGA na NITAENDELEA kuipinga

Kuhusu hiyo STUDENTS LOAN BOARD inabidi iwe privatised kabisaaa na serikali ikae pembeni iiache hiyo mamlaka ifanye kazi yake hru bila kuingiliwa japo still itakuwa inmulikwa na vyombo bya serikali ili kusijetokea uhuni wetu wa sikuzote (kama vile Udini na Ukabila na uoendeleo mwingineo)

Nasema tena serikali iachane na miradi ya kujenga vyuo vikuuu kwani financially siyo viable wakati organisations mbali mbali zinaweza kujenga hivyo vyuo..inshort its about time serikali ikaachia mambo haya na ikawa ina regulate tu na siyo kuembark kwenye hizi big time projects wakati huo huo nasomesha watu nje
 
?



Kuhusu hiyo STUDENTS LOAN BOARD inabidi iwe privatised kabisaaa na serikali ikae pembeni iiache hiyo mamlaka ifanye kazi yake hru bila kuingiliwa japo still itakuwa inmulikwa na vyombo bya serikali ili kusijetokea uhuni wetu wa sikuzote (kama vile Udini na Ukabila na uoendeleo mwingineo)

Yaani sasa ndugu yangu DrWHO hii serikali itakuwa kila kitu haiwezi kufanya kwa ufanisi, sasa kazi yake hasa ni nini?
 
MKJJ: Nashukuru kwa ufafanuzi ambao kusema kweli umekwenda deep sana. Sasa sijui hawa ndugu zangu serikalini ambao wanalipwa kwa kazi hiyo kwa nini hawawezi kutoa maelezo wakaeleweka. Jamani tunaumia kwa kuwa na viongozi waliochaguliwa kiujanjaujanja na hivyo wanaongoza kwa ujanjaujanja. Umakini katika CCM ni tatizo kubwa, uropokaji tuuu!
 
1. OMBI KWA MKJJ,Tafadhali, unaweza kupata barua za offer za hiyo mikopo ya hao vijana, waliyopewa na serikali? please nadhani hii itatuondolea hisia wengi wakina Thomas. Maana, mimi siamini kabisa kwamba serikali inaweza kupeleka watu nje harafu ikawa-disown, mchana kweupe tena kwa confidence ya hali ya juu namna hii (ninayemfahamu aliyekuwa na confidence ya namna hii ni Donald Rumsfield!). Please, hii itatusaidia wengi especially skeptics akina Mkandara and the rest. Maana siamini kwamba Jamhuri yetu na matatizo yake yote..it can commit this crime..bila sababu..Otherwise tuanze kuappeal kuomba msaada kama raia walipa kodi na wapiga kura! After all its still our governement.

Na wengine wote humu tafadhali take note, serikali ya Tanzania haina wajibu wa kusomesha mtu yeyote........ Katiba inakupa haki ya kupata elimu kadri ya uwezo wako ila sio serikali kukusomesha. Uwepo wa haki na upatikanaji wake ni vitu viwili tofauti.
 
1. OMBI KWA MKJJ,Tafadhali, unaweza kupata barua za offer za hiyo mikopo ya hao vijana, waliyopewa na serikali? please nadhani hii itatuondolea hisia wengi wakina Thomas. Maana, mimi siamini kabisa kwamba serikali inaweza kupeleka watu nje harafu ikawa-disown, mchana kweupe tena kwa confidence ya hali ya juu namna hii (ninayemfahamu aliyekuwa na confidence ya namna hii ni Donald Rumsfield!). Please, hii itatusaidia wengi especially skeptics akina Mkandara and the rest. Maana siamini kwamba Jamhuri yetu na matatizo yake yote..it can commit this crime..bila sababu..Otherwise tuanze kuappeal kuomba msaada kama raia walipa kodi na wapiga kura! After all its still our governement.

Mikuko.. kabla ya mimi kufanya hivyo unafikiri kuna mwanafunzi aliyepokea barua iliyomuonesha kuwa amepokea mkopo toka bodi, au ni jinsi gani wanafunzi wanajulishwa kuwa wamekubaliwa mkopo?
 
Mkuu, mimi nadhani uwaulize hawa jamaa walijuaje kama wamepewa scholarship? walipewa barua au walitumiwa ujumbe mfupi/mrefu wa kilonga mbali? Mi nilipewa barua iliyoonyesha kwamba nimepata udhamini wa serikali. By the time naingia chuo.

Aksante
 
Mkuki,

Kama nilivyoandika mwanzoni mimi nalifananisha sana hili suala na yale yaliyotokea Poland mwaka 1996/97. Hata case hiyo serikali iliwakataa
wanafunzi kwa matamko mbalimbali.

Wanafunzi walipata scholarship mwaka 1995 wakati Mkapa yuko kwenye kampeni ya kuwa rais na wakati huo alikuwa waziri wa hiyo wizara ya elimu ya juu. Majina ya wanafunzi yalitangazwa kwamba wamepata scholarship lakini ilipofika wakati wa kuondoka wizara ikasema haina pesa na serikali iko kwenye uchaguzi. Wakaambiwa wajitahidi kutafuta pesa za tiketi na waende na serikali baadaye itawarudishia hizo pesa pamoja na pesa za mambo mengine.

Wanafunzi wakanunua tiketi na kuondoka. Mkapa akaingia Ikulu na serikali mpya ikaingia madarakani. Baada ya kufika kule wanafunzi wakasubiri wee bila
bila kutumiwa pesa na hali yao ikawa mbaya. Uongozi wa wanafunzi ambao mimi nilikuwemo ukaingilia kati lakini bila mafanikio.

Wanafunzi wakaanza kufukuzwa hosteli, wakanyimwa visa, wengine wakaishia mitaani. Tukaandika magazetini na kwa wakati huo nafikiri ilikuwa case ya kwanza kwa serikali kukataa wanafunzi wake. Serikali ikasema haiwatambui
na kwamba waliondoka kwa mapenzi yao. Mshika panga hapo alikuwa ni prof. Mahalu.

Kuna kipindi mimi nilienda likizo na kukutana na prof. Mahalu, wakati huo tulikuwa tumeongea na wizara ya elimu ya Poland pia na kuwaomba wawapatie hao wanafunzi full scholarships ambazo wengine ndio tulikuwa nazo. Tukaambiwa kama serikali yetu itaandika kwamba haina uwezo na inaomba hao wanafunzi wapewe scholarship basi watapewa. Hizo ndio njia ambazo nchi zingine walitumia kuokoa wanafunzi wao. Ilikuwa inatosha hata hiyo barua kuandikwa na ubalozi.

Basi mimi na kujiamini kote nikajua tutapata hiyo barua, kukaa na Mahalu akasema ni aibu kwa serikali kuomba halafu tukakataliwa. Nikamwambia nina uhakika hawatakataa maana tumeshatayarisha mazingira mazuri na tunajua hawatakataa. Akasema serikali haiwezi kufanya kitu hicho, ni aibu. Nikamwambia mheshimiwa kipi aibu, kujifanya una pesa unaweza kuwalipia wanafunzi na kuwadanganya au kukiri wizara yako haina pesa? Akasema hawezi na kuondoka. Toka siku hiyo heshima yangu kwa mahalu ilishuka na sikushangaa juzi niliposikia kaiba mamilioni ya pesa. Huyo ni jamaa ambaye mimi nilipokuwa pale mlimani hall 5 alikuwa yeye Dean wa facult ya Law akiwa na nyumba juu kidogo ya hall 5. Nilikuwa namheshimu kama msomi, mpole na mtanashati kweli kweli, kumbe kwa ndani ni jangili.

Karibu wanafunzi wote walipoteza mwaka, ukiachia wawili ambao waliendelea shauri ya wazazi/ndugu zao kuwasaidia. Mungu mkubwa baada ya Mahalu kuondoka pale kupelekwa ubalozi Ujerumani, serikali ikaja kubali kuendelea kuwalipia wanafunzi ambao bado walikuwa wapo wanahangaika mitaani Poland.
Wengi wa hao vijana sasa wako TZ wakilitumikia taifa lao.

Nilipomsikia huyo naibu katibu mkuu akisema hawatambui, yakaja maneno yale yale ya akina Mahalu. Binafsi sina wasiwasi hata kidogo kwamba kuna viongozi
pale wizarani waliwaambia hao wanafunzi wajitafutie tiketi na kuondoka na kwamba serikali itawatumia pesa.

Haiji kichwani kwamba wanafunzi wote 29 wangekiuka amri ya wizara kwamba wasiende. Nina uhakika hawa walikuwa ndio wale wenye unafuu ambao angalau wazazi wao waliweza kuwanunulia tiketi.

Kuhusu board ya mikopo nijuavyo mimi hakuna anayepewa barua na badala yake majina yanatangazwa kwenye web site ya board kwamba nani wamekubaliwa sponsorship.

Hiyo ndio experience ninayoijua mimi ya hiyo wizara ya elimu ya juu.
 
mkulima... nilitaka bwana Mikuki apate hilo jibu la jinsi gani wanafunzi wanajua kuwa wamepatiwa mikopo... na nimependa maelezo yako kuhusu wanafunzi wa Poland...
 
Back
Top Bottom