Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Ni experience tosha! Shukrani kwa waungwana wote. Ila sasa kama hii ndo Jamhuri yetu, kweli we have a long way to go. Infact mimi kwa kweli, nilikuwa siamini kwamba it is possible kwa serikali kudanganya umma, tena umma wasomi. Lakini kwa experience ya huyu bwana na mwalimu Mahalu.....Inaogopesha ati. The whole permanent secretary to come and parade lies before the republic? Jamani basi..............
 

Wakati wa kuhesabiwa umefika!

TANGAZO LA MCHANGO WA KUSAIDIA WANAFUNZI WA KITANZANIA WALIOTELEKEZWA UKRAINE.

Utangulizi:
Kwa vile serikali imeendelea kuwakana vijana hawa licha ushahidi wote ambao upo unaoonesha kuwa serikali ilifahamu na ilitoa baraka zake kwa vijana hawa kwenda nje kusoma, tunajikuta kuwa kuendelea kuibembeleza ni kuendelea kuipa nguvu na uwezo ambao haina. Kuendelea kuisihi serikali kutimiza ahadi yake imekuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hachezi. Kwa vile hakuna dalili kuwa serikali iko tayari kufanya uchunguzi au hata kujaribu kuliangalia jambo hili kwa umakini unaostahili, wazazi, marafiki, na jamaa ya wanafunzi hawa wameamua kufungua akaunti ambayo itatumika kwa ajili ya kulipia dharura na gharama ya masomo ya vijana hawa 26 wa kitanzania.

Kama wazazi wa vijana hawa wangekuwa na uwezo wa kifedha wa kuwasomesha vijana hawa bila ya shaka wasingeendelea kujidhalilisha kwa kuipigia magoti serikali kwani wangeweza “kuchota” tu kiasi kinachotakiwa na kuachana na serikali. Ukweli ni kuwa familia hizi za watanzania zilizotawanyika kila kona ya nchi bara na visiwani hazina uwezo huo hata kidogo. Kwa vile vijana hawa wameenda kusomea fani ambazo ni muhimu sana kwa nchi yetu kama Udaktari,Uhandisi, Sheria ya Kimataifa na Teknolojia ya Mawasiliano, kukatishwa kwao masomo kama serikali inavyopendekeza itakuwa ni kukubali kushindwa pasipo ulazima wowote.

Ni kwa sababu hiyo basi, wazazi na vijana hawa wanawasihi na kuwaomba Watanzania wenzao popote pale walipo bila ya kujali, rangi, kabila, dini, au itikadi zao za kisiasa kuwachangia vijana hawa ili waweze kuendelea na masomo badala ya kurudi wakiwa wameshindwa. Naomba tuwape vijana hawa nafasi ya kupata elimu ambayo vinginevyo hawataweza kuipata kabisa. michango hii itatolewa taarifa mara kwa mara na matumizi yake kwa vijana wetu yatatolewa habari kwa umma. Tuoneshe kuwa sisi ni wamoja hatima yetu ni moja. Ndugu zangu “kidole kimoja, hakivunji chawa”.

Kwa wale walioko Tanzania tafadhali tumia utaratibu huu kutuma mchango wako wowote ule:

Bank: National Microfinance Bank Ltd
Swift Code: NMIBTZTZ
Name of Account: TANLET MICHANGO YA DHARURA
Account number: 2016600043
Currency: TSHS


Kwa wale walioko nje ya nchi na kutegemea nchi walizopo au fedha wanazutumia.

NMB CORRESPONDENT BANKS FOR FOREIGN CURRENCY TRANSFERS

BANK: CITIBANK N.Y.
SWIFT CODE :CITIUS33
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 36142828
CURRENCY: USD

BANK: DEUTSCHE BANK TRUST COMPANY AMERICAS - NY
SWIFT CODE:BKTRUS33
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 04416097
CURRENCY: USD

BANK: DEUTSCHE BANK AG FRANKFURT AM MAIN DE
SWIFT CODE: DEUTDEFF
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER:100 9575481 0000
CURRENCY: EURO

BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE: RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 EUR
CURRENCY: EURO

BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE: RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 GBP
CURRENCY: GBP

BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE:RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 USD
CURRENCY: USD

NB:
Tafadhali soma makala yangu kwenye Tanzania Daima http://www.freemedia.co.tz (Jumatano) ambapo najibu maelezo ya serikali kuhusu suala hili.
 
Mmh! Jee Lyatonga naye ni signatory? hata hivyo nilikuwa nauliza tu.
 
Basi Mzee, kama ni hivyo wacha nione ndani ya hii pochi kuukuu kuna nini tusaidie vijana wetu maana kama sio sisi nani atafanya? Labda ingekuwa Two month before election ungeona mwenyewe MM huo mshike mshike.
 
mimi nawaambia si walitamba kuwa Kikwete alishinda kwa asilimia 80? wangoje 2010, kwa hili watalipa kwenye masunduku ya kura.. nyie subirini tu...!!
 
Nitofautiane na wewe.......hakuna mtu atakayelipa 2010....Watanzania hawako 'sophisticated' namna hiyo na ni wepesi mno wa kusahau. Kama kulipa hao wenye kulipa wangekuwa wameshalipa tokea 2000 au 2005. Usishangae 2010 Kikwete akashinda kwa zaidi ya ailimia 90......hapo yakhe ndo utazimia kabisa......
 
Nyani, sitaki kukuapia.. lakini mark my words... CCM italipa kwa kitendo chao hiki... kwa mzimu wa Nyerere, na mizimu ya mababu zangu... !! na mizimu ya wale wote ambao wamejitahidi kuwasomesha watoto wao na wale ambao watoto wao wamesomeshwa na serikali.. CCM italipa... and na kama nitakuwa peke yangu kuwafanya walipe.. watalipa!! Niombee uhai na afya njema tu..!
 
Haya kaka....Mnyazi Mungu na akujalie siha njema, akuongezee busara nyingi, akili nyingi, na nguvu za kuwalipisha hao ma 'imla'. Na mimi binafsi nitakuweka katika sala zangu za kila siku na kumuomba Mola akubariki katika jitihada zako za kujenga taifa la kisasa na la asali na maziwa.
 
Mwanakjj good attempt..ila usiape kwa miungu binaadamu....Yule mwenye Kumiliki uhai wa kila mtu nae ni mmoja na hana wa kumfananisha nae.....ila sikutishi usiweke hizo statement za jazba mapema hawa jamaa hawaaminiki.....Ila we need to do the best, this things not happen in future....kama GOV wangeweza kufanya dinner moja tu..na kuwaita wenye nazo..on the same day wangepata hizo pesa..lkn ndio hivyo....wametia pamba....
 
Mwanakijiji na Wanabodi.
Naomba mumtafute Mengi kama kweli ni rafiki wa wakati wa shida, pia Dioniz Malinzi huyu alimpa Sumaye billioni moja kama mchango wa kampeni kwa ajili ya sumaye.
wenye simu za watu hao wampatie mwanakijiji.
 
Mwanakijiji na Wanabodi.
Naomba mumtafute Mengi kama kweli ni rafiki wa wakati wa shida, pia Dioniz Malinzi huyu alimpa Sumaye billioni moja kama mchango wa kampeni kwa ajili ya sumaye.
wenye simu za watu hao wampatie mwanakijiji.



Ah hao matajiri wetu wa kibongo kama hakuna mkono wa Serikali watasaidia kitu kweli?

Hawa matajiri wetu wanachangia pale ambapo wanaona kutakuwa na maslahi na wao hapo baadae, lakini katika michango kama hii!! sijui wacha tuombe Mungu.
 
Mikuki


Are you serious?
 
unataka wachangie waambie wanachangia upinzani then kitakachofuata ni kumwagiwa ngano, kufutwa ipp, waarabu kupokonywa biashara zao n.k !!
ccm ni kama family business uende against nayo unalimwa, yaani ni umafia juu ya umafia ! kasheshe hapo !!
 
Mwanakijiji na Wanabodi.
Naomba mumtafute Mengi kama kweli ni rafiki wa wakati wa shida, pia Dioniz Malinzi huyu alimpa Sumaye billioni moja kama mchango wa kampeni kwa ajili ya sumaye.
wenye simu za watu hao wampatie mwanakijiji.

Mtalii,

si lazima yote afanye mkjj, kila kitu tunamtupia mwanakijiji tu sisi wengine tunafanya kazi gani? kupiga simu sio lazima apige mkjj hata wewe mtalii unaweza - tumsaidia mkjj kwa vitendo na wala sio kumsupport kwa maneno tu, action speak louder than ............
 
Wakati wa vitendo ni huu ndugu zangu. Tuchangie.

Mtalii:

Kwa mara ya kwanza na kuunga mkono(in a light touch teh teh)

Jj
 

MKJJ,
Kama alivyosema Nyani,hawa mabwana sio wa kuwekea nadhili,wamesha tucheza shele mara ngapi?unahisi kulikua na ushindi wa 80% NO!
"Wamefanya fanya....tu....." kama wenyewe wanavyosema or let me say mwenyewe alivyo sema pale bandarini.
Muombe Mungu watanzania waamke kama Hapa JF na waone nini tunachokifanya toward Tanzania iliyo bora kwa watu wote.
Shime Jamaani michango,i cut off my bugdet for brown bottles for a week,to support what we/you have started.
Hamuoni wakiandika kile tunacho fanya,ngoja tushindwe (God forbid) wataandika kwenye magazeti yote kama swala lile la upatu.
TUCHANGE.... MPAKA.... KIELEWEKE..!
 
KIla mtu anajua Mengi anachangia jamii, wa kutafutwa ni hao akina Malinzi,
Manji, huyo wa miss Tanzania (Ludenge) na wengine wengi.

Nina uhakika Mengi anaweza kuchangia, muhimu ni kwa wale wenye contacts zao kuwasiliana nao maana tukimwachia kila kitu Mwanakijiji itakuwa balaa si
na yeye atashindwa hata kufanya kazi zake?
 
Atakaye mpigia Manji ampe ujumbe wangu huu `Kusomesha watoto kwa Taifa ni jambo la Lazima na fahari kuliko kununua mechi ya kandanda ili watu waingie bure kuona starehe hiyo ambayo wanaimudu kuilipia. Afanye yaliyo ya muhimu pengine tunaweza kufikiria kusahau BAADHI ya tuliyoyasikia'
 
mimi ndio nataka nione kama kweli jambo forums inaweza kuaminiwa kuonesha mfano na uwawajibikaji wa wananchi au ni kijiwe cha porojo tu... Tunapotaka viongozi wa wawajibikaji hatuna budi kuwaunga mkono... Endapo suala hili litashindikana kwa vile watu ni bahili na hawako tayari kujitokeza basi ni kweli Tanzania tutakuwa tumelaaniwa! Hili la kusubiri na kuwapigia simu matajiri halina umuhimu wowote! kwanini tuwakimbilia matajiri na kuwalilia!!? Huo ndio utakuwa mwanzo wa kujidhalilisha na kujifanya watumwa. Kama wao wenyewe kwa dhamira zao hawataamua kuchangia, kuna umuhimu gani wa kuwapigia na kuwabembeleza?

Jana baada ya habari hizi kupatikana nyumbani Bibi wa miaka 84 tayari amejicommitt shilingi laki mbili kusaidia mfuko huu, kwani anaelewa umuhimu wa vijana kusoma (watoto wake walisomeshwa na serikali) na amewaambia wamlipie kiasi hicho!! Watanzania msisubiri matajiri wawafanyie kila kitu!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…