Wakati wa kuhesabiwa umefika!
TANGAZO LA MCHANGO WA KUSAIDIA WANAFUNZI WA KITANZANIA WALIOTELEKEZWA UKRAINE.
Utangulizi:
Kwa vile serikali imeendelea kuwakana vijana hawa licha ushahidi wote ambao upo unaoonesha kuwa serikali ilifahamu na ilitoa baraka zake kwa vijana hawa kwenda nje kusoma, tunajikuta kuwa kuendelea kuibembeleza ni kuendelea kuipa nguvu na uwezo ambao haina. Kuendelea kuisihi serikali kutimiza ahadi yake imekuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, hachezi. Kwa vile hakuna dalili kuwa serikali iko tayari kufanya uchunguzi au hata kujaribu kuliangalia jambo hili kwa umakini unaostahili, wazazi, marafiki, na jamaa ya wanafunzi hawa wameamua kufungua akaunti ambayo itatumika kwa ajili ya kulipia dharura na gharama ya masomo ya vijana hawa 26 wa kitanzania.
Kama wazazi wa vijana hawa wangekuwa na uwezo wa kifedha wa kuwasomesha vijana hawa bila ya shaka wasingeendelea kujidhalilisha kwa kuipigia magoti serikali kwani wangeweza kuchota tu kiasi kinachotakiwa na kuachana na serikali. Ukweli ni kuwa familia hizi za watanzania zilizotawanyika kila kona ya nchi bara na visiwani hazina uwezo huo hata kidogo. Kwa vile vijana hawa wameenda kusomea fani ambazo ni muhimu sana kwa nchi yetu kama Udaktari,Uhandisi, Sheria ya Kimataifa na Teknolojia ya Mawasiliano, kukatishwa kwao masomo kama serikali inavyopendekeza itakuwa ni kukubali kushindwa pasipo ulazima wowote.
Ni kwa sababu hiyo basi, wazazi na vijana hawa wanawasihi na kuwaomba Watanzania wenzao popote pale walipo bila ya kujali, rangi, kabila, dini, au itikadi zao za kisiasa kuwachangia vijana hawa ili waweze kuendelea na masomo badala ya kurudi wakiwa wameshindwa. Naomba tuwape vijana hawa nafasi ya kupata elimu ambayo vinginevyo hawataweza kuipata kabisa. michango hii itatolewa taarifa mara kwa mara na matumizi yake kwa vijana wetu yatatolewa habari kwa umma. Tuoneshe kuwa sisi ni wamoja hatima yetu ni moja. Ndugu zangu kidole kimoja, hakivunji chawa.
Kwa wale walioko Tanzania tafadhali tumia utaratibu huu kutuma mchango wako wowote ule:
Bank: National Microfinance Bank Ltd
Swift Code: NMIBTZTZ
Name of Account: TANLET MICHANGO YA DHARURA
Account number: 2016600043
Currency: TSHS
Kwa wale walioko nje ya nchi na kutegemea nchi walizopo au fedha wanazutumia.
NMB CORRESPONDENT BANKS FOR FOREIGN CURRENCY TRANSFERS
BANK: CITIBANK N.Y.
SWIFT CODE :CITIUS33
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 36142828
CURRENCY: USD
BANK: DEUTSCHE BANK TRUST COMPANY AMERICAS - NY
SWIFT CODE:BKTRUS33
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 04416097
CURRENCY: USD
BANK: DEUTSCHE BANK AG FRANKFURT AM MAIN DE
SWIFT CODE: DEUTDEFF
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER:100 9575481 0000
CURRENCY: EURO
BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE: RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 EUR
CURRENCY: EURO
BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE: RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 GBP
CURRENCY: GBP
BANK: RABOBANK NEDERLAND
SWIFT CODE:RABONL2U
ACCOUNT NAME: NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD
ACCOUNT NUMBER: 3908.86.327 USD
CURRENCY: USD
NB:
Tafadhali soma makala yangu kwenye Tanzania Daima
http://www.freemedia.co.tz (Jumatano) ambapo najibu maelezo ya serikali kuhusu suala hili.