kama vile nimeona mtu ameongelea namna watoto wa baba wa TAIFA walivyosoma tabora boys..na wa kawawa pale tabora girls...
sikuhizi hiyo ngumu ...hembu mliopo hapo UK tuambieni maisha anayoishi RIZ...nasikia hiyo apartment anayokaa ipo kiwango si mchezo..rent ya mwezi ingeweza kuwalipia pesa ya kujikimu hao walalahoi vijana wetu 28 hapo kiev...
kuhusu vijana kwenda ubalozi wa uk wako right ..angalia passport yako utaona wameandika kama mtanzania utakuwa mahali ambako ubalozi wetu haupo[ukraine upo lakini hauna msaada]...ukipata tatizo unaweza kuripoti ubalozi wa united kingdom[someni passport zenu.....
hawa watoto walipelekwa na serikali...uhakika huo pia ninao..wako wanaosomeshwa na wazsee wao na hao inawezekana sio miongoni mwao...kwani idani ya wanafunzi wetu pale pamoja na wanaojilipia ni wengi zaidi.....aibu..aibu,,..aibu!!!!!!
hao kama hawatalipiwa bora waombe ukimbizi..you know what ,kale kauhuru kanapotea sasa..kama hawa hapa wamegoma wanaambiwa wakaape kwa WAKILI hawa ambao jk atasema wamemuaibisha atasema wakaape kwa nani...au wakaape kwenye KABURI LA BABA WA TAIFA ,BUTIAMA!!!!!
Nashauri next time watoto ...wawe wanaenda at least once Kuandamana kutembelea kaburi la baba wa TAIFA kumlilia na kumuimbia ule wimbo maarufu...
"kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ...na kikwete angesoma wapiiiiiiii""""" nafikiri kama sio shule jk angekuwa mvuvi mmoja tu kati ya wavuvu au wakwevi..au mgemaji wa tembo .,pale bagamoyo ...au msaidizi pale mlingotini...
sio kwamba natania kama sio nyerere wengi wetu tungekuwa pia wachunga ndama au mbuzi au kwa bahati ngombe.....tumesahau????!!