DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
Wanafunzi hao walikwenda Ukraine kwa udhamini wa serikali au ki vyao?
Mzee Kichuguu unanikumbusha mbali,wakati huo Shule zile zilikuwa zinaitwa Warsar na Berlin, sina shaka ni wakati wa Msaki (RIP) na Ndeki (RIP).Nilikuwa nataka kukutaarifu tu kuwa Balozi wetu huko ni Patrick Chokala!Heshima mbele Mzee.
mwanakijiji!Balozi Chokala amefanya kila awezalo na wiki iliyopita amebakia kusema "mwombeni Mungu". Mikuki, wanafunzi 29 wote waondoke nyumbani kwa ahadi ya mdomo tu...? ingekuwa mmoja ningesema inawezekana. Vipi kuhusu wanafunzi wa Cuba ambao nako kwenye situation kama hiyo? Vipi wale wa Urusi ambao wanaishi kwa kubangaiza wakipewa dola 200 kwa mwezi (ikilipia chakula, mavazi, dawa n.k). Malipo ambayo ya mwisho yamepokewa mwezi uliopita na sasa wameletewa barua kuwa hakuna malipo mengine hadi mwezi wa tisa? miezi hii minne wataishi vipi?
mwanakijiji!
Usimtetee Balozi Chokala,Kwanini yeye ameshindwa kuwasaidia raia wake ugenini hata kwa chakula hata kuwapa malazi pale ubalozini moscow ktk hali ya kishida hivyo hivyo na kibinadamu,wanafunzi hao wa kitanzania na hatimaye wakasaidiwe kwenye Ubalozi wa kigeni.Jibu la Kwamba waombe mungu si Jibu makini kwa mtendaji kwani yeye ni sehemu ya kutoa msaada kwa jamii anayoingoza,Mungu tunamuomba kwa wale tunaoamini hivyo Lakini yeye kama mwakilishi wa Nchi amesaidia vipi kuhakikisha wananchi wake wanapata angalau huduma ya Mlo na Malazi.Hivi wangekuwa wanae wa Kuzaa angewajibu jibu la namna hiyo na kumwaga manyanga?Nini faida ya nchi kuwa na Balozi Nchi Nyingine ikiwa haiwezi hata kusaidia Raia wake wanapofikwa na shida na kuhitaji msaada?
kama vile nimeona mtu ameongelea namna watoto wa baba wa TAIFA walivyosoma tabora boys..na wa kawawa pale tabora girls...
sikuhizi hiyo ngumu ...hembu mliopo hapo UK tuambieni maisha anayoishi RIZ...nasikia hiyo apartment anayokaa ipo kiwango si mchezo..rent ya mwezi ingeweza kuwalipia pesa ya kujikimu hao walalahoi vijana wetu 28 hapo kiev...
kuhusu vijana kwenda ubalozi wa uk wako right ..angalia passport yako utaona wameandika kama mtanzania utakuwa mahali ambako ubalozi wetu haupo[ukraine upo lakini hauna msaada]...ukipata tatizo unaweza kuripoti ubalozi wa united kingdom[someni passport zenu.....
hawa watoto walipelekwa na serikali...uhakika huo pia ninao..wako wanaosomeshwa na wazsee wao na hao inawezekana sio miongoni mwao...kwani idani ya wanafunzi wetu pale pamoja na wanaojilipia ni wengi zaidi.....aibu..aibu,,..aibu!!!!!!
hao kama hawatalipiwa bora waombe ukimbizi..you know what ,kale kauhuru kanapotea sasa..kama hawa hapa wamegoma wanaambiwa wakaape kwa WAKILI hawa ambao jk atasema wamemuaibisha atasema wakaape kwa nani...au wakaape kwenye KABURI LA BABA WA TAIFA ,BUTIAMA!!!!!
Nashauri next time watoto ...wawe wanaenda at least once Kuandamana kutembelea kaburi la baba wa TAIFA kumlilia na kumuimbia ule wimbo maarufu...
"kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ,kama sio juhudi zako nyerere ...na kikwete angesoma wapiiiiiiii""""" nafikiri kama sio shule jk angekuwa mvuvi mmoja tu kati ya wavuvu au wakwevi..au mgemaji wa tembo .,pale bagamoyo ...au msaidizi pale mlingotini...
sio kwamba natania kama sio nyerere wengi wetu tungekuwa pia wachunga ndama au mbuzi au kwa bahati ngombe.....tumesahau????!!
Waambie wafanye kweli sio wafike pale wakipewa mlo na kupangashiwa hotel au hosteli na visenti kidogo waone wamefika Lazima wawatumie hawa wazee kuwafundisha uongozi wetu nini wanatakiwa kufanya kwa wananchi wao.sasa hivi nazungumza na kiongozi wa msafara wakiwa ndani ya treni kuelekea Kiev... safari ya karibu masaa 10 hivi.... stay tuned...
Amesikia vilio vyao.............................Huoni Balozi wa Uingereza Hakuweka Ngumu! Kwani siku zote hamtupi mja wake ni sisi waja huwa kuna wakati hasa wa raha tunamtumikia shetani..............tunajisahau!Aisee machozi yananitoka kabisa nikijiaribu kujenga taswira ya adha walizopata watoto hawa huko waliko; Mungu awasidie huko waliko.
Aisee machozi yananitoka kabisa nikijiaribu kujenga taswira ya adha walizopata watoto hawa huko waliko; Mungu awasidie huko waliko.