Matukio ya aina hii yanasikitisha, yanaudhi, yanakatisha tamaa, yanaaibisha.......
Ni matukio ya aina hii ndio yanayopelekea wakati mwingine mtu kuanza kujiuliza maana ya uTanzania ni nini. Lakini tunaelewa kuwa ubovu katika uongozi wa nchi sio ubovu wa utaifa wenyewe.
Hakuna sababu yoyote ile inayoweza kuwa justification ya tendo hili la aibu kubwa sana katika historia ya taifa la Tanzania. Hivi kweli rais wetu baada ya aibu hii anaweza tena kutembea kifua mbele kati ya viongozi wenzie wa kimataifa?
Hata kama serikali haikuwa na uwezo wa kifedha kuwasaidia vijana hawa, angalau hata hiyo ya kuwarudisha nyumbani tu, lilikuwa ni jukumu la serikali yenyewe kufanya mipango ya kutatua tatizo hili kwa njia yoyote ile, hata kama ni kuomba msaada wa huo ubalozi wa Uingereza uwasaidie kuwarudisha vijana nyumbani, kuliko kuwatelekeza hivi hivi tu kana kwamba hawana taifa. Kwa njia hii sasa aibu ya taifa na serikali itatapakaa dunia nzima.
Hata kama kosa ni la vijana