Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

Serikali yawatelekeza wanafunzi 29 Ukraine

ni rahisi kupongezana kwa kauli nzuri kuliko kwa vitendo vizuri. Habari ambazo zinatiririka sasa hivi ni kuwa afisa mmoja (ngazi za juu) amezungumza na kusema serikali inawataka vijana hao "kurejea chuoni mara moja, wale wenye uwezo wa kurudi nyumbani warudi, na wale wasio na uwezo waombe watu wawasaidie nauli ya kurudi"..... !!! habari zaidi baadaye..

I'm trying to make sense out of that nonsense even though I know good and well that you can't make sense out of nonsense! That high ranking official can't be serious......Mwanakijiji are you sure you're not making this up?
 
Serikali yetu imezoea vitisho, mimi wala sishangai kauli hiyo. Pengine wanapanga mkakati wa kuwatumia FFU huko waliko au kuwafikisha mahakamani mara wakiamua kurejea Tz.
 
Nakubaliana na wote waliosema kwamba si wakati wa kupongezena huu.

Lakini nachukua fursa hii kukupa shukrani za awali Mwanakijiji. Nikuombe radhi pia niliyachukua mahojiano yako na kuwapelekea wakuu wa vyama yatumike kama ushahidi bila kibali chako.

Masikitiko yangu ni kuwa pamoja na waandishi kupewa ushahidi wa CD za mahoajiano yao bado wameepa kuita panga-PANGA. Wameendelea kuita PANGA, KISU KIKUBWA.

Imani yangu ni kuwa kama Magazeti yangetoka na vichwa- SAKATA LA KUTELEKEZWA KWA WATANZANIA UKRAINE- Waziri Mkuu akataa kuzungumzia, asema aachwe aendelee kula; Msolla-akata simu; Kikwete arejesha suala kwa Nkono! Naamini kesho yake serikali ingechukua hatua-ama ya kuwasaidia vijana hawa au kuwakana moja kwa moja na hivyo kutangaza rasmi mwito kwa watanzania wengine kuweza kuwasaidia kutokana na serikali kutangaza kushindwa kutimiza wajibu wake. Hayo yalikuwa matarajio yangu, na kama mstari huo ungepitiwa jitihada za mwanakijiji na wengine zingezaa matunda zaidi.

Lakini waandishi wetu kwa mara nyingine wame-water down hili suala ingawa nawashukuru kwa kulipa kipaumbele.

Kauli zako mwanakijiji zimemliza mmoja wa wakina mama wenye watoto Ukraine. The whole press conference was soul touching!

Hata hivyo, si haba. Ni mwanzo mzuri. Aluta continua!

Limetajwa suala la kuchangia, sasa naona kuna waratibu wa pande mbili.

Viongozi wa upinzani waliomba TANLET isaidie kuratibu harambee.

Humu napo naona kuna ambao wameitisha harambee.

Lini linahitaji kujadiliwa: Je, wote waendelee, ama tuchague chombo kimoja? na kwa utaratibu upi? Kwa kadiri ya makubaliano nitafikisha ujumbe kwa wakuu wa vyama.

Nimeondoka DSM kwa sasa, lakini nipo bado kwenye mawasiliano na kama kuna suala urgent basi tutafutane simuni.

Hakuna kulala, Mpaka Kieleweke

JJ
 
What a hell.

Serikali imesema kuwa hao wanafunzi walijipelekA WENYEWE NA HIVYO KUWATAKA WAONDOKE KWENYE UBALOZI HUSIKA MARA MOJA ,NA KEUENDELEA NA MASOMO KWA GRARAMA ZAO NA KWA WALE AMBAO HAWANA NAULI WATAJAZA FOMU MAALUUM ILI WAPEWE MKOPO WA KUWARUDISHA NCHINI.

ANOTHER DRAMA SERIKALI YA AWAMU YA NNE ,UAMUZI HUO UMETOLEWA NA N.KATIBU MKUU WA WIZARA .

MSOLLA YUPO IRINGA KWENYE KAMPENI ZAKE ZA KUWANIA UJUMBE WA NEC NDANI YA CCM.

naishia hapa.
 
Mwanakijiji,

Mbona ujumbe nilokutumia Jumamosi bado hujajibu?

Tafadhali confirm kama umepata.

Kupongezana ni jadi yetu wala tusiogope kufanya hivyo ili mradi tu iwe pongezi ya kweli. Kwa hatua hii bado kunahitajika pongezi.
 
SERIKALI imetoa tamko la kuwakana wanafunzi wa Ukraine. Mwenye taarifa kamili atuwekee. Ilikua katika habari ya saa 2 ITV
 
Nimesikiliza maelezo ya Naibu Waziri kuhusu suala la wanafunzi hawa. Hatimaye najua nani ana majibu... namtafuta.. Mnaweza kusikiliza sehemu ya maelezo hayo na majibu ya vijana kwenye www.voa.gov nenda kwenye lugha ya Kiswahili
 
"c. Jitihada za wanafunzi hawa kuwasiliana na viongozi wa wizara zimekwama. Kila mara wanaishia kuzungushwa zungushwa na viongozi wa wizara hiyo akiwemo Waziri wa Wizara hiyo Prof. Msolla ambaye amefikia kukata simu kila wanafunzi hao wanapompigia simu. Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mhe Augustino Mrema alimuandikia Raisi Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la wanafunzi hawa tangu tarehe 23/1/2007. Hii inamanisha kuwa Wizara hiyo hiyo imeshindwa kushughulikia matatizo ya wanafunzi hao. Habari tulizozipata zinaonesha kuwa wanafunzi wengine walioko nje ya nchi wanaokabiliwa na matatizo yanayolingana au kukaribiana na yale ya Ukraine ni wale wanaosoma nchini Cuba, na Urusi. Inamithilika sasa kuwa Wizara na Bodi ya Mikopo wanayo sera za kibaguzi dhidi ya nchi zilizokuwa zikifuata siasa za kijamaa. Hatujapata habari kama wanafunzi wanaosoma katika nchi za kibepari na hata wanaosoma nchi jirani kama vile Uganda na Kenya wanafanyiwa kama wanafunzi walio nchini Ukraine."

I still think this sudden interest is politically motivated just because these guys are in a critical condition;

If Mrema wrote the letter on '23/1/2007', within 14 days, or at most 28 days he should have expected a reply, or he should have followed up. At most, give it 3 months. April 23. BUT OOH NOO, people had to wait until students were sleeping outside, then it was ante-up!!

Hypocrisy, opportunism and just plain slow. For the opposition, this was one way to score big, and there are many other ways they can score big. Lakini wapo wapo tu.

Kweli, wabongo tuna mambo.
 
"c. I still think this sudden interest is politically motivated just because these guys are in a critical condition;

If Mrema wrote the letter on '23/1/2007', within 14 days, or at most 28 days he should have expected a reply, or he should have followed up. At most, give it 3 months. April 23. BUT OOH NOO, people had to wait until students were sleeping outside, then it was ante-up!!

Hypocrisy, opportunism and just plain slow. For the opposition, this was one way to score big, and there are many other ways they can score big. Lakini wapo wapo tu.

Kweli, wabongo tuna mambo.

Mheshimiwa defunkadelic, naona hili jambo umelirudiarudia mara nyingi sana, sasa mimi naomba utupe ushauri wako, katika hali hii ambapo hawa vijana wamo, unafikiri sisi katika forum na upinzani tungefanyeje ili tusionekana tunajipendekeza na wakati huohuo sauti zetu ziendelee kusikika?
 
Mwanasiasa,

Nakubaliana na wewe, ndugu yetu defuncadelic apendekeze njia anayoona inafaa.

Mimi niliwahi kusema mara nyingi, mtu anayetafuta sifa kwa kutenda yaliyo mema, huyo mwache na aipate hiyo sifa. Hata kama viongozi wa upinzani ni opportunists lakini angalau wanataka kutatua tatizo.

Yebo Yebo, Mbona mwanakijiji anaendesha michango, kama hiyo jumuia inaweza kuchangia si wangewasiliana na yeye. Nafikiri ni rahisi kumwamini Mwanakijiji maana kwa hili katumia nguvu zake na muda wake wote.
 
Ni kweli kwamba Serikali ya Awamu ya NNe Imetoa tamko rasmi kwamba "Vijana 29 waliopo kwenye Ubalozi wa Uk huko Kiev Hawawatambui".Maelezo hayo yametolewa na Naibu katibu Mkuu,Wizara ya Elimu ya Juu Ndg. Celestine Gesimba,katika Taarifa Rasmi iliyotolewa na Wizara (Serikali) kwenye vyombo vya habari kufuatia Taarifa ya Vyama vya upinzani kuomba Maelezo kuhusu sakata la Vijana hao.
Naibu katibu Mkuu huyu aliwaamuru vijana hao warudi mara moja vyuoni mwao,na kwa wale ambao hawana Fee ya shule waombe mikopo ya nauli kwa serikali ili warudishwe Tanzania (nyumbani).Kwa kupata habari hiyo zaidi ingia kwenye www.voa.gov na upata maelezo ambayo yanaripotiwa na Dina Chahali kutoka Dar-es-salaam.
 
"c. Jitihada za wanafunzi hawa kuwasiliana na viongozi wa wizara zimekwama. Kila mara wanaishia kuzungushwa zungushwa na viongozi wa wizara hiyo akiwemo Waziri wa Wizara hiyo Prof. Msolla ambaye amefikia kukata simu kila wanafunzi hao wanapompigia simu. Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mhe Augustino Mrema alimuandikia Raisi Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la wanafunzi hawa tangu tarehe 23/1/2007. Hii inamanisha kuwa Wizara hiyo hiyo imeshindwa kushughulikia matatizo ya wanafunzi hao. Habari tulizozipata zinaonesha kuwa wanafunzi wengine walioko nje ya nchi wanaokabiliwa na matatizo yanayolingana au kukaribiana na yale ya Ukraine ni wale wanaosoma nchini Cuba, na Urusi. Inamithilika sasa kuwa Wizara na Bodi ya Mikopo wanayo sera za kibaguzi dhidi ya nchi zilizokuwa zikifuata siasa za kijamaa. Hatujapata habari kama wanafunzi wanaosoma katika nchi za kibepari na hata wanaosoma nchi jirani kama vile Uganda na Kenya wanafanyiwa kama wanafunzi walio nchini Ukraine."

I still think this sudden interest is politically motivated just because these guys are in a critical condition;

If Mrema wrote the letter on '23/1/2007', within 14 days, or at most 28 days he should have expected a reply, or he should have followed up. At most, give it 3 months. April 23. BUT OOH NOO, people had to wait until students were sleeping outside, then it was ante-up!!

Hypocrisy, opportunism and just plain slow. For the opposition, this was one way to score big, and there are many other ways they can score big. Lakini wapo wapo tu.

Kweli, wabongo tuna mambo.

Hapa sasa ni hukumu mbovu. Mimi si msemaji wa Mrema lakini najua kwamba baada ya kuaandika hii barua alifuatilia na ndiye kiongozi pekee senior wa upinzani aliyeendelea kutoa tamko mara kwa mara kuhusu suala hili toka awali. Na baadaye Mvungi na Mbatia wakaanza kufuatilia na wamefanya vikao vya mara kwa mara na wazazi wa hawa watoto. CHADEMA tulikuwa kimya wakati wote katika hatua za awali. Na ilikuwa deliberate. Sakata la hawa wanafunzi lilianza toka mwaka jana, Dr ambae ni mmoja wa aliyeratibu kuwapeleka Ukraine alinifuata ofisini tukazungumza kwa kina sana na kukubaliana kuchukua hatua mapema kabisa. Kabla sijaanza mchakato wenyewe kichama akanifuata na kunieleza kwamba wazazi wa watoto wameomba CHADEMA kama chama cha siasa kisiingilie kwa kuwa serikali imeonyesha nia ya kusaidia na kwamba tukiingilia kati litachukua sura ya kisiasa. I advised the party to back off. Tumerejea katika suala hili baada ya kuona limefikia acute stage. Ambayo mtanzania yoyote mwenye kujali anapaswa kuingilia kati. Namshangaa Lowasa anasema aachwe anakula wakati vijana wa kitanzania wako ughaibuni hawana uhakika wa chakula. Kula gani huko kusikokishwa au anakula 'nchi'?

Kuna mambo ambayo unaweza usiingilie kati ukiipa muda serikali kutenda; lakini serikali ya Tanzania inaelekea kutopenda kutenda mpaka panapotokea mivutano. Ndio Managament by Crisis hiyo!

JJ
 
Ni mawazo yake ambayo kweli yanatakiwa kwa viongozi wetu kuyaamkia na kulala nayo kila siku ya Mungu. Ni wazo zuri sana kama viongozi wetu wa Upinzani watajifunza kuwa mbele ya matatizo. Sio jambo rahisi kabisa na mara nyingi ni bora kusubiri usije kufanya vitu ambavyo tayari vimeisha tafutiwa suluhisho.
Tukumbuke tu kwamba hata Mungu kaleta aya zake (NENO) baada ya maasi kuzidi.
 
Uhurubado,
samahani mkuu kwa lugha yangu labda hukunielewa kwamba nilichokuwa nikisema ni issue na Upeo unayohusiana na mada hii. Hii haina maana wewe huna upeo mkubwa bali hukuweza kuizamia ndani mada hii na kuelewa malengo yake na nini hasa malengo yake.

Hili sio swala la mfumo kabisa ila ni maamuzi ya mtu mmoja ama baadhi wanaokiuka sheria. Vijana hawa wana kila vibali vinavyotakiwa na hakuna mahala inapingana na mfumo wa elimu ya juu nchini ina maana mfumo umewekwa wazi na ndio maana sisi tunaweka ushahidi wetu kupitia mfumo huohuo.. Sasa mnaposhindwa kuelewa ni kwamba siku zote kila kitu huwa na mwanzo!..na mwanzo huo ndio ufunguzi wa mada hii kwetu kwa sababu hatuwezi kujadili kitu ambacho hakipo. Yalianza ya Chuo Kikuu kisha yamefuatiwa na haya! pole pole viongozi wanapata salamu zetu wanapokiuka sheria.

Ilikuwa ni katika kujibu hoja yenu kwamba Tanzania ina matatizo mengi sana iweje hili lipewe kipaumbele?
Nadhani nikaendelea kuwafahamisha kuwa matatizo mengine yote yanazungumziwa humu kila siku na kila mmoja wetu huchangia kwa hiyo unapoona swala la maji muhimu lipe kichwa ( fungua mada) na sio kusema kwamba hawa wanafunzi 29 sio kitu na hawastahili debe hili.
Kumbuka tu tukisimamisha hili kesho wengine na pengine wanao watakuwa wamesafishiwa njia na hawa vijana 29 ktk mikopo ya elimu ya juu haki Kiyama!.
Karibu babu usiondoke ndio lugha tena wengine hapa hatuna uzoefu wa kuchonga maneno matamu ktk uandishi.
 
Hapa sasa ni hukumu mbovu. Mimi si msemaji wa Mrema lakini najua kwamba baada ya kuaandika hii barua alifuatilia na ndiye kiongozi pekee senior wa upinzani aliyeendelea kutoa tamko mara kwa mara kuhusu suala hili toka awali. Na baadaye Mvungi na Mbatia wakaanza kufuatilia na wamefanya vikao vya mara kwa mara na wazazi wa hawa watoto. CHADEMA tulikuwa kimya wakati wote katika hatua za awali. Na ilikuwa deliberate. Sakata la hawa wanafunzi lilianza toka mwaka jana, Dr ambae ni mmoja wa aliyeratibu kuwapeleka Ukraine alinifuata ofisini tukazungumza kwa kina sana na kukubaliana kuchukua hatua mapema kabisa. Kabla sijaanza mchakato wenyewe kichama akanifuata na kunieleza kwamba wazazi wa watoto wameomba CHADEMA kama chama cha siasa kisiingilie kwa kuwa serikali imeonyesha nia ya kusaidia na kwamba tukiingilia kati litachukua sura ya kisiasa. I advised the party to back off. Tumerejea katika suala hili baada ya kuona limefikia acute stage. Ambayo mtanzania yoyote mwenye kujali anapaswa kuingilia kati. Namshangaa Lowasa anasema aachwe anakula wakati vijana wa kitanzania wako ughaibuni hawana uhakika wa chakula. Kula gani huko kusikokishwa au anakula 'nchi'?

Kuna mambo ambayo unaweza usiingilie kati ukiipa muda serikali kutenda; lakini serikali ya Tanzania inaelekea kutopenda kutenda mpaka panapotokea mivutano. Ndio Managament by Crisis hiyo!

JJ

Aha!! Mnyika, asante sana, na samahani sana, na maswali yangu nafanya makusudi kabisa kuuliza kwa nia njema (hadi nimeweza kupata info ambayo watu hawakujua hapa). Kuna sehemu nimemwuliza Samvulachole kama anaamini serikali haikujua. Ofcourse walikuwa wanajua, na maneno yako yameoshenya kwamba hata opposition mlijua na mlikuwa mnashughulikia. Mwanasiasa ambaye ni member wa Chadema, inaonekana hakujua hii. Yeye anaongelea kutoka angle ya jamboforum. Tatizo jamboforum watu wako anon, na kuleta mabadiliko wakati watu mko anon, ni taratibu mno kuleta mabadiliko. Lakini opposition mna nafasi ya kuchambua mengi zaidi bila kujificha. Mwanakijiji anafanya kazi nzuri na ngumu hadi anawatia aibu nyie opposition, na mashambulizi yake yanatoka marekani.

Mnyika, Chadema mna gazeti lenu, je ma-journalist wenu walikuwa wapi? Au Mwanakijiji kweli ni Chadema? Opposition, mna miaka 4 ijayo muweke misingi mizuri, vitu kama hivi, serikali inapojivuta vuta, basi fanyeni kweli. Ndio maana nauliza kwanini makele wakati watu wanalala nje?

I/we did not know Mrema was on it, and you need to understand me, I cant figure out why from the begining of the year, up to now nothing was done (yaani mpaka ishu iwe critical). I AM NOT UNDERMINING WHAT IS BEING DONE NOW...PLEASE UNDERSTAND THAT. As much as everyone asks question about the government, we also need to be selfcritical of our failings.

Where was the pressure? Thats all I am asking. Me asking question, shouldnt take away the efforts at hand.
 
kwa maoni yangu suala la wanafunzi Ukraine laweza kutatuliwa hivi:

Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru ambayo itapewa mamlaka ya kuchunguza ukweli wa madai ya vijana hawa na kuchukua hatua mara moja ya kutatua suala hili. Pendekezo langu ni kuwa, kabla ya lolote kufanyika serikali ikubali kuwadhamini vijana hawa kwa mwaka ujao wa masomo (kwani tayari wameshaanza masomo miezi hii yote) na iachane kabisa na wazo la kuwanunulia tiketi warudi nyumbani. Wazo la kuwarudisha nyumbani ni wazo la watu walioshindwa! Endapo vijana hawa watarudi nyumbani itakuwa ni ishara ya viongozi wetu kushindwa kabisa kutatua matatizo na badala yake kung'ang'ania visivyong'ang'anika. Kama tumeweza kuvumilia na kuwapa muda watendaji wengi wabovu wajirekebishe, nina uhakika serikali inaweza kabisa kuwavumilia na kuwadhamini vijana hawa kwa mwaka huu wakati tume inachunguza ukweli. Tume iwe na uhuru na uwezo wa kumuita na kumhoji kiongozi yeyote na ifanye kazi zake hadharani au mbele ya vyombo vya habari. Endapo baada ya uchunguzi kufanyika itagundulika kuwa kuna makosa yalifanyika basi serikali inaweza aidha kuwaambia vijana hivyo lakini kuendelea kuwasomesha hadi wahitimu kwa makubaliano mapya au kuwarudisha nyumbani kwa mpango wa kuwapa nafasi ya kuendelea na masomo yao nyumbani. Kwa kufanya hivyo wanafunzi hawapotezi, na serikali haishindwi.

Na endapo itaonekana kuwa viongozi kule bodi ya mikopo na wizarani waliboronga basi hatua za kinidhamu zichuliwe dhidi yao. Jambo la maana ni kuunda tume huru ambayo itakuwa na uwezo wa kumhoji kiongozi yeyote hadharani na kuita vielelezo vyovyote. Kwa kufanya hivyo, serikali itaonesha kulipa uzito unaostahili suala hili badala ya kutulazimisha tukubali matamshi yake tu hata kama matamshi hayo yanazua maswali zaidi kuliko majibu.

Ni matumaini yangu kuwa serikali itaonesha busara na si papara na itatumia hekima ya hali ya juu ili kuhakikisha kuwa vijana wetu wanaendelea na masomo, taratibu zinafuatwa na Taifa letu linaendelea kuheshimu elimu ya juu bila ya kujali hadhi au hali ya mtu.

Wenzangu mnapendekeza litatuliwe vipi hadi kufikia win win situation? badala ya Lose-win situation ambayo serikali imependekeza?
 
Mwanakijiji,

Hili tatizo linafanana sana na tatizo lililo wakumba wanafunzi wa Tanzania nchini Poland mwaka 1996/97 ambapo mimi nilihusika kuwasaidia kama kiongozi.

Na wenyewe waliambiwa hivyo hivyo hawatambuliwi na warudi nyumbani. Waliorudi ndio hawakusoma tena labda baadaye sana. Kuna vijana wengine wakazamia West.

Bahati nzuri baada ya kama mwaka tatizo lao likatatuliwa na wote waliokuwa bado wako Poland, wakasoma na sasa wamemaliza masomo na wanaitumikia serikali yao.

Jitihada zifanywe ili hawa wanafunzi wamalizie masomo yao huko huko waliko
maana wakirudi TZ kwanza kwa mwaka 2007/8 hawawezi kwenda vyuoni maana muda umepita. Hata huko mbele itakuwa ngumu na itabidi wagombanie hizo nafasi na wanafunzi wengine wa miaka ijayo.

Hata kama kuna kosa limefanyika, solution iliyo rahisi na kuwasaidia hao vijana wamalizie masomo yao huko huko Ukraine.

Mtu aliyekuwa anawakwamisha ni Prof. Mahalu, kumbe yeye mwenyewe ni jambazi anaiba mamilioni huku anawaminya watoto wa wakulima washindwe hata kupata elimu ambayo ni halali yao. Wakati hupo alikuwa mkurugenzi wa elimu ya juu.
 
Mwanakijiji na Mkulima:

Nawaombeni nitumie sehemu ya mawazo yenu niyawasilishe kwa umma mpana na panahusika.

Mkulima-naomba kama una details la sakata la Poland nitumie kwenye mnyika@yahoo.com ili niweze kuoanisha masuala haya.

Wote:

Mpaka sasa hamjanijibu ombi langu: kwamba tuache waratibu wawili wa kukusanya michango au tuchague mmoja? Kama mmoja yupi? Mwanakijiji au TANLET?

Ni wakati wa vitendo sasa; serikali imeshatoa msimamo wake japo umetolewa na mtendaji; wanasiasa kama Msolla mpaka sasa wako kimya! Huyu lazima ajiuzulu, by crooks and nails. I will see what I can do nikirejea DSM

Jj
 
Oscar Mbuza
HabariLeo; Tuesday,May 29, 2007 @00:02

SERIKALI imewataka wanafunzi wa Tanzania waliosimamishwa masomo Ukraine na kupiga kambi katika Ubalozi wa Uingereza kuomba wasaidiwe, kuondoka ubalozini hapo na kurejea nyumbani mara moja.

Katika hatua yake hiyo, Serikali imewatumia wanafunzi hao tiketi za safari ili warejee nchini na kusema watakaogoma waende vyuoni kuendelea na masomo kwa gharama zao na wazazi wao.

Agizo hilo la Serikali lilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Celestin Gesimba Dar es Salaam jana. Gesimba alisema katika mwaka wa masomo wa 2005/06, wanafunzi 130 walipata udahili katika vyuo vikuu mbalimbali Ukraine na kati yao ni wanafunzi 84 ndiyo waliokamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na walijiunga na vyuo hivyo.

Alisema wanafunzi wengine 46 ambao hawakuweza kukamilisha taratibu hizo walishauriwa wajiunge na vyuo vya elimu ya juu vya nchini kwa vile serikali haikuwa na uwezo wa fedha wa kuwakopesha wanafunzi wapya nje ya nchi.

Alisema wanafunzi 17 kati ya wanafunzi hao 46 walikubali kutafuta udahili kwa vyuo vya elimu ya juu nchini na wanafunzi 29 ambao ndiyo waliofikwa na matatizo ya ada nchini Ukraine hivi sasa hawakukubaliana na ushauri huo wa serikali.

Alisema badala yake wanafunzi hao waliamua kwenda Ukraine kwa utaratibu wao binafsi na kujiunga na vyuo walivyovipenda wenyewe. “Mwaka wa masomo wa 2006/07, mwongozo wa kupata mkopo ulibadilika. Serikali iliona ni vema ikazingatia kuwakopesha wanafunzi waliopata udahili nchini ambako gharama ni ndogo kuliko vyuo vya nje,” alisema Gesimba.

Alisema wanafunzi hao 29 wa Ukraine waliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mkopo na walijibiwa kwamba serikali haikuwa na fedha za kuweza kuwakopesha na walishauriwa watafute udahili katika vyuo vya elimu ya juu nchini.

“Kwa uamuzi wao waliamua kujilipia nauli na kwenda Ukraine bila idhini ya serikali au ahadi ya maandishi kwamba wangeweza kusaidiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,” alisema Gesimba.

Alisema wanafunzi hao sasa wamekwama kulipa ada na sasa wamesimamishwa masomo na wanaushinikiza ubalozi wa Tanzania ulioko Moscow, uiombe serikali iwasaidie. Alisema wazazi wa wanafunzi hao wanapaswa kuwalipia ada wanafunzi hao kwa vile serikali haiwajibiki na gharama zinazojitokeza kwa elimu ya wanafunzi walio nje ya nchi.
 
Tanlet iendelee kufanya shughuli hizo mimi nilikuwa nasaidia kwa dharura tu... pindi akaunti ikiwa tayari (nimeambiwa iko tayari tunasubiri swift codes n.k) basi wao waendelee na mimi nitasogea pembeni.
 
Back
Top Bottom